Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571




Ni kuwa mjadala wa Richmond ndio unaanza japo mbunge wa Kigoma Mjini ndugu Peter Serukamba alimtaka spika kumpa ufafanuzi kwanza kuwa ni kwanini Waziri mkuu hakupewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati husika.

Waziri mkuu kaamua kujitoa kwenye meza na amekuwa mchangiaji wa kwanza kuchangia, nitawaambia kile ambacho yeye amechangia binafsi.

A Mchango wa Waziri Mkuu*

Ameanza kwa kumpongeza Mwakyembe na kusema amekuwa na mbwembwe nyingi sana .

Anasema hakuridhika na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa na anamponda sana mwakyeme kwa yeye ni mwqanasheria na hakumfanyia Natural Justice, yeye binafsi kwani hawakumhoji hata siku moja.

Analalamika Waziri Mkuu kuwa hakupewa Natural Juctice kwani hakuitwa na anasema kuwa alikuwa tayari kwenda hata kwa miguu kwenye kamati husika za bunge.

Anasema kuwa ameonewa sana na amedhalilishwa sana na kamati na kuwa ametuhumiwa bila hata ya kuulizwa hata jambo moja.

Anasema kuwa yeye ameonewa na anasema kuwa kwenye taarifa yao hakuna hata taarifa moja iliyotoka kwenye ofisi ya waziri mkuu , na anasema kuwa ingekuwa heshima kama angepewa nafasi ya kujitetea.

Analaumu kuwa kama wanaweza kumponda Waziri Mkuu kiasi hicho je?mwananchi wa kawsaida anaweza kutendewa haki?

Waziri mkuu ametangaza kuwa amejiuzulu na amemwandikia barua Rais Kikwete.

Zitto anataka mwongozo wa spika juu ya Waziri Mkuu kujiuzulu na anasema kuwa kama Waziri Mkuu amejiuzulu basi na baraza zima lazima lijiuzulu kwani Rais aliteua baraza kwa kushauriana na Waziri Mkuu.

Spika anakataa kuwa baraza zima haliwezi kujiuzulu , mpaka apate barua ya Rais.

Ni kuwa bunge bado linajikanganya sana na hali inawatisha hata wabunge na kwa sasa spika anajiuliza anawezaje kuliendesha bunge kaomba kupewa ushauri na wabunge .

Kuna hali ngumu sana kwa spika na haswa baada ya Zitto kutaka baraza zima lijiuzulu ili kuwweza kumpa rais muda wa kutangaza baraza jipya la mawaziri .

Mbunge wa CCM masilingi anasema kuwa jambo hilo lipelekwe kwenye kamati ya wabuinge wa kamati ya CCM ili wakajadili sijui kama hapo kuna mwelekeo kwa sasa .

Masilingi anatak bunge liahirishwe ili wakajadili kwenye kamati ya CCM .

Zitto anatoa hoja kuwa bunge liahirishwe kwa muda kwanza ili kuweza kuijadili hoja hiyo hapo baadae ,kamnyima mdee halima nafasi ya kutoa taarifa .

Ni kuwa bunge limeahirishwa hadi saa kumi na moja jioni na wabunge wa CCM wameenda kujipanga sijui watakuja na ajenda ipi na rais bado hajajibu barua ya Lowassa ya kujiuzulu.

Naitafuta barua hapa nikiipata tuu naiweka wakuu kaeni mkao wa kula humu leo.

Hakuna waziri ambaye ameenda kumpa pole isipokuwa Batilda tu, hapa kuna ujumbe mzito sana na umejificha.

Nitaendelea kuwapa yanayojiri hapa

B. Hotuba Kamili ya Mheshimiwa Edward Lowassa


Lowassa Ngoyai Edward 2008.

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli. Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawahukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".


==================
C. Vyombo vya Habari vya Kimataifa
Tanzania PM tenders resignation

Dar es Salaam, Tanzania 07 February 2008 01:19

Tanzania Prime Minister Edward Lowassa told Parliament Thursday he had tendered his resignation to the president after being implicated in a corruption scandal over an energy deal.

"Because I have been linked to this scandal, I have decided to write to the president asking to be relieved of my duties," the premier told lawmakers during a session of the Dodoma-based Parliament broadcast live on television.

The speaker adjourned the session and explained he was awaiting a decision by President Jakaya Kikwete on Lowassa's resignation letter.

The premier's decision came after a report was submitted to Parliament over a deal signed between the government and Texas-based firm Richmond for emergency power supply.

According to a probe into the contract, the prime minister, as well as two other government ministers and several other officials, allegedly meddled in the tender to favour the United States company.

The emergency power-supply deal aims at providing electricity to the East African nation in case of drought.

According to the report, the deal contravened laws and rules on procurement and costs the country $140 000 a day. --

AFP

D. Rais wa JMT aridhia maombi ya Waziri Mkuu Kujiuzulu
Rais akubali kuondoka kwa Waziri Mkuu

Taarifa za hivi punde kutoka Dodoma, mji mkuu wa Tanzania zasema Rais Jakaya Kikwete amekubali barua ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kufuatia madai ya kashfa.

Akitangaza hatua yake katika bunge Alhamis asubuhi, Bwana Lowassa alisema: "Nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumuomba niachie ngazi."

Mawaziri wengine wawili wamefuata nyayo zake Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa na kuamua kujiuzulu baada kuhusisha na kashfa ya ufisadi mkubwa.

Sakata hiyo inahusu zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura.

Mawaziri wengine walioomba kujiuzulu ni Nazir Karamagi wa Nishati na Madini pamoja na mwenzake wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ibrahim Msabaha.

Bwana Lowassa aliteta kwamba kamati teule ya bunge iliyomhusisha na kashfa ya Richmond ilimnyima haki ya kujieleza.

Alisema alikuwa ametafakari kwa makini kuhusu shutuma hizo na kufikia uamuzi kwamba, "tatizo ni uaziri mkuu."

"Kwamba ionenekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe."

Akielezea hatua yake ya kujiuzulu, Bwana Lowassa aliongeza "ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu."

Zabuni hiyo ilipewa kampuni ya Richmond Development group yenye makao yake nchini Marekani.

Kamati teule ya bunge kwenye ripoti yake iliyowasilishwa hapo Jumatano, ilipendekeza kujiuzulu au kuchukuliwa hatua kali kwa wahusika.

Ripoti hiyo iliwasilishwa bunge na Mwenyekiti wa kamati hiyo teule, Harrison Mwakyembe.

Kuhusu Waziri Mkuu, ripoti hiyo inasema: "Uamuzi wa serikali kuizuia Tanesco ( Shirika la umeme Tanzania) isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote za kisheria kuwepo ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyojuu ya wizara ya nishati na madini."

"Kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa kimdomo inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu."

Kikatiba ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji na utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za serikali.

Yeye pia ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
"Kamati teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond."

Mawaziri wengine walioshutumiwa katika ripoti hiyo ni yule anayehusika na nishati na madini, Nazir Karamagi, mtangulizi wake Dr. Ibrahim Msabaha ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru, ilikuwa motoni kwa kutoa maelezo ya uongo kwa kamati hiyo.

Mbunge Mwakyembe alisema kamati yake ilitaka kuweka wazi kwamba mchakato wa zabuni ya kuzalisha nguvu za umeme kwa dharura wa megawati 100 ulighubikwa na vitendo vya ukiukwaji taratibu, kanuni na sheria za nchi."

"Na hivyo kujenga kiwingu cha mashaka ya upendeleo, ubadhirifu na rushwa ambavyo vimechangia kumwongezea mwananchi mzigo wa gharama za umeme."

Taifa lilikuwa limetumbukizwa kwenye hasara kubwa kutokana na mkataba huo wa Richmond kinyume na taarifa iliyotolewa na Takukuru (taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa).

Kwa nini kamati ya wataalamu haikuihoji Richmond kuhusu uongo huo bayana? Ilishutumiwa kwa kujiharibia sifa yenyewe baada ya kutoa ushahidi wa uongo ikisema mchakato wa zabuni hiyo ulikuwa wazi, shirikishi na ulizingatia kanuni na kwamba dosari zilizojitokeza hazikuhitimu kuiletea taifa hasara.

"Taarifa hiyo imemong'onyoa kwa kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana ya kupambana na rushwa na siyo kuipamba ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo."

Mbunge Harrison alisema kwenye tovuti yake, kampuni ya Richmond "ilikuwa inajitangaza kimataifa kipindi hicho kuwa kampuni yenye miradi mikubwa Tanzania ya ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha michezo, ujenzi wa bomba la mafuta la kilomita 1150 na ukarabati wa viwanja kadhaa vya ndege nchini."

Kamati teule ilishindwa kuelewa "kwa nini kamati ya wataalamu haikuihoji Richmond kuhusu uongo huo bayana ambao uliokuwa ushahidi wa kutosha kuipotezea sifa za kuwa mzabuni?"
Chanzo: BBC Swahili


E ****************** Maoni ya wanaJF *******************

Hapo ndio haja ya kuwepo waziri asiye na wizara maaalum au naibu waziri mkuu inakuwepo. Ila ni washenzi tu hakuna haja ya kuweweseka nani aongoze shughuli za serikali bungeni Batilda Buriani si yupo? yeye si ndio mwakilishi wa waziri mkuu bunge?

Naam mi ndio maana hapa JF niliwahi kuwaambia kile kitabu cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA alichoandika nyerere kina unabii mule,hakuna mtu anayekichambua lakini ipo siku,tusipoangalia mambo haya yalosemwa mule yatatimia.

Lowassa hana haja ya kusema hakupewa nafasi ya kujitetetea. Kamati haikuwa imemtuhumu mtu wala kuform chaji zozote,kamati ilialika watu kwenda mbele yake na kujieleza au kueleza lolote wanalolijua mbona hakwenda? Kisheria kujiuzulu kwa waziri mkuu hakutokani tu na kwamba yeye anahusika na hilo sakata bali ni ministerial responsibility, yeye kama kiranja wa baraza na mawaziri wake wameboronga bado alipaswa kujiuzulu hata kama asingehusika moja kwa moja.

Kama anadai hakupewa nafasi ya kujitetea ama kama anavyodai kuhojiwa? hakupaswa kuwasilisha barua ya kujiuzulu badala yake angewasilisha maelezo ya kujiteteta ili bunge lililomuidhinisha kuwa waziri mkuu lijadili utetezi wake na hatimaye litoe maamuzi,kwa nini kakimbilia kujiuzulu?

Afahamu kamati haikupendekeza aondoke ilimwambia atumie busara zake,sasa kama kujiuzulu na kulalamika ndio busara basi poa


Kutokumhoji Lowassa nafikiri ni katika mapungufu machache ya hiyo kamati. Hivyo hivyo pia kushindwa kumhoji Karamangi.

Nina uhakika baadaye Dr. Mwakyembe ataelezea kwanini hawakufanya hivyo.

Labda kwasababu hawa jamaa wametunyanyasa sana, sio muhimu tena kuangalia wameangukaje, ila in future kama kuna tuhuma ni vizuri kuwahoji wahusika wote kabla ya hukumu.

Pia kamati ilishindwa kupendekeza adhabu kali kwa Yona na Rostam kwa kukataa kwenda kutoa ushahidi kwenye kamati.

Muhimu kwasasa ni kuondoka kwa Lowassa na fundisho kwa mawaziri wengine. Ukihusika kwenye kashfa utaondoka maana hata PM aliondoka.

F
SWALI
Hivi katiba inasemaje kama Waziri mkuu akijiuzulu? Je, is it automatic that balaza lake linakuwa dissolved au ni Rais ndiye anaamua kulivunja?

Naomba kuuliza.

JIBU
Yes, Baraza linavunjika Automatically kwa mujibu wa Ibara ya 57 (2)(e)

Nanukuu...

Yes,Baraza linavunjika Automatically kwa mujibu wa Ibara ya 57 (2)(e)

Nanukuu...

57.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.

(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(a) Endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia;

(b) Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;

(c) Ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;

(d) Iwapo atachaguliwa kuwa Spika;

(e) Iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;

(f) Ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;

(g) Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

G. Naziri Karamagi na Dr. Msabaha nao wajiuzulu
MugoThe Great;137099 said:
Msabaha na Karamgai nao wameamua Kujiuzulu. Ila Lowassa anasisitiza kuwa Tume ya Mwakyembe imesema uongo. Sasa hivi wabunge wa CCM "Mh. Joseph Selukemba (Mb-Kigoma) et al" wanasema EL ni shujaa. Hii ni AIBU kubwa kwa wabunge wa aina hiyo.

Tayari Waziri Mkuu Lowasa alitangaza nia ya kujiuzulu asubuhi, kisha akafuatiwa na Nazir Karamagi, Waziri wa Nishati na Madini ambaye katika uchangiaji wa hoja yake alionekana kuzungumza madudu matupu na kwa kiasi kikubwa aliunga mkono ripoti ya Mwakyembe.

Baadaye alijifananisha na Yesu kwa kujifanya eti hakuwa na dhambi na kwamba anawajibika ili kusudi Watanzania wasife kwa dhambi. Inachekesha.

Aliutumia muda wake mwingi kuzungumzia mambo ya vichekesho huku mara kadhaa akirusha mpira kwa mwenzake Dk Msabaha. Naye Msabaha baada ya kupewa nafasi alitumia muda wake mwngi kufanya mzaha wa matani ya Wazaramo na Wanyamwezi, lakini hakutoa hoja ya msingi ili mradi tu alisimama kutamka nia yake ya kujiuzulu.

H
Wakuu wote JF nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kazi nzito ya muda mrefu, kuipigania Richimonduli mpaka leo kuuona mwisho wake. Wakuu naomba niseme kwa dhati kwamba nilikuwa ninaijua power ya JF, lakini sivyo kama ninavyojua sasa, Oh! my God jana sikulala, simu na messages kutoka kila kona ya dunia wananchi wanataka kujua kilichotokea, na huku JF kuna nini maana kulikuwa hakuingilinki kabisaa, siku nzima ya leo. JF kwa kweli ni political power kama sio tool, wakuu tuzidishe mapambano maana sasa tulipofikia ni pakubwa sana katika kuelimisha na kuwasilisha ishus muhimu kwa taifa.

Pia ningemuomba ndugu Robot Invisible, kwamba ajitahidi iwezekanavyo na hasa kwa kwa kusaidiana na sisi members kuuimarisha mtambo unaoisukuma hii JF maana ukweli ni kwamba bado kunahitajika nguvu zaidi ili uweze kubeba wananchi wengi kwa wakati mmoja, leo kuna wakati ilikuwa impossible kuingia, kulikuwa na wananchi 510 kwa wakati mmoja, sasa mkuu Robot tuwasiliane kuangalia nini kinaweza kufanyika ili kuongeza nguvu.

Waziri Mkuu wa zamani, Lowasssa, ameondoka, huu ni ushindi mkubwa sana kwetu wananchi na hasa JF, kwa sababu hakuondoka kwa wema, ameondoshwa na nguvu ya wananchi, yaaani sisi wanyonge. Hakupenda kuondoka, tunajua jinsi alivyojaribu ku-lobby sana kwa Muungwana, kwa visingizio kuwa hakupewa Due-Process, mimi ninasema kuwa hakukuwa na haja ya kupewa hiyo haki kwa kiongozi asiyekuwa muaminifu kama yeye, hiyo tunawapa wananhi au viongozi ambao wanaonekana kuwa ni waadilifu na labda kuna hisiaa za kuonewa katika tuhuma zao, lakini sio yeye, kwanza Mwalimu alisema na ushahidi akaonyeshwa jinsi alivyokula hela za magari ya wabunge akiwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu, Muungwana akaombwa sana na viongozi wa juu wa CCM kuwa asimpe huyu u-PM, na sasa haya ya aibu, sasa huyu tunampa hiyo haki ya nini? Ukweli ni kwamba by now alitakiwa awe anongelea Ukonga au Segerea, lakini sio bungeni!

Tunajua kuwa toka juzi usiku, alikuwa ameshambiwa wazi uso kwa uso na Muuungwana kuwa atoke mwenyewe, kabla hajamtoa, ndio maana jana hakuwepo pale airport, na pia tunajua kuwa ilikuwa atoke toka pale aliponyimwa u-makamu wa CCM, na kwamba ana mkono kwenye umwagiwaji waaandishi wa habari tindikali, kwa sababu wale waandishi walikuwa tayari wameshapata habari kuwa anatakiwa atoke wiki ile ile aliyowamwagia hiyo sumu, akafanikiwa tu ku-delay the process. Wakuu JF hebu fanyeni kazi ya utafiti wa kweli mjue mali alizojilimbikizia huyu mkuu in the last two years, maana wengi wetu hapa inaonekana hatujui how much damage the man amefanya kwa taifa, angalia mtoto wake asiyezidi umri wa miaka hata 30, mali alizokusanya in the last two years, hayo maneno ya kunyimwa haki anayatoa wapi? Hivi hana aibu? Kwa nini mwishoni mwa ripoti Mwakyembe anawapa pole waandishi wa habari waliomwagiwa acid? Ninasema huyu fisadi belongs to prison na sio kupewa haki, hao waandishi anatakiwa awalipe makovu na majeraha na vilema aliyowapatia, Yes I said it I do not care anymore huyo ni jambazi, he belongs to prison kama sio Rumande, lakini sio haki ya sheria zetu, absolutely NO!

Enough!, sasa tumejua kuwa nguvu ya wananchi haiwezi kuchezewa na majahili, hata kama ni marafiki wa rais, they all fall kama panzi and that is what they deserve, kuondoka kwa nguvu ya wananchi, tena wapigwe mrufuku kuingia tena kwenye siasa hawa maana ninajua kuwa sio wajinga hao wana plan B hao, they are not done hawa, sasa hivi mtawasikia Yes I said kwa sababu I know it kuwa hawawezi kukubali kutoka hivi hivi tu, lazima watakufa na wengi very sooon, and wakifanya hivyo itakuwa ni kuvuja kwa pakacha furaha yetu wananchi! Sasa wataingia kwenye vyama au watajificha nyuma ya vibaraka wao na baadaye watajitokeza mbele, Yes ndio tabia ya fisadi hiyo huwa hawatosheki.

Lakini for now heshima mbele kwa wananchi wote hapa JF kwa kazi nzito, na bado wakuu mbele kuna kazi zaidi, ninasema kuwa bado kuna viporo vingi sana havijamalizwa, ninasema kuwa Hosea naye aondoke, huko Usalama atueleze alikuwa wapi haya yakitendeka? kama hana ya kutosha naye aende sasa, mwanasheria mkuu naye alikuwa wapi, kama hana maelezo naye aende, waziri wa polisi alikuwa wapi? Ubalozi wetu DC walikuwa wapi? Halafu huyu Lowassa na wenziwe wapelekwe kwenye mkono wa sheria, na pia Mwakyembe apewe new assignment ya kumfuatilia Rostam na kuweka mambo yake wazi, anafanya nini? Mbona yuko kila kona ya nchi yetu yeye ni nani? Halafu Spika naye ana mengi ya kujibu huyu naye, maana haeleweki kabisa.

Wakuu heshima mbele tena, tusilale, ujumbe kutoka hapa unafika panapotakiwa, salaam kwa wajumbe wote JF wembe ni ule ule, tumejionea wenyewe kuwa inawezekana, sasa kazi!

Ahsante Wakuu!

Mzee Mkapa kaachonjo, wananchi wanakuja haoooooooo!
 
Last edited by a moderator:
Amesema sababu, hakuhojiwa na kamati teule. Katika report ya Dr Mwakyembe hakuna ushahidi hata mmoja kutoka ofisi za waziri mkuu.
 
Naona jamaa ameanza kwa jazba sana na kukandia report mwishoni kaishia kubwaga manyanga!!!
 
Bunge sasa limesimama, wanatafuta mwongozo nani aongoze shighuli za serikali Bungeni. Baada za mweshimiwa Lowasa Kujiuzulu.
 
Wakuu,
Naomba wenye ndikali, banana na vijoge watuletee hapa sokom kuu Bukoba.

Tunaanza maandalizi ya Rubisi ya kutosha kwa ajili ya sherehe ya kumng'oa karamagi na Lowassa.

Dokezo kwa JK: Tunaomba usimpe uwaziri Balozi Sued Kagasheki hata kama utakosa mtu toka Kagera anayefaa. Huyu ni fisadi wa Kimataifa WIPO wanamfahamu.
 
Mzee wa viwango ameshtuka na ameomba mwongozo wa wabunge jinsi za kuongoza Bunge. Kinachojadiliwa sasa je baada ya Lowasa kujiuzulu je mjadala uendelee au la?

Masilingi anashauri Bunge liahirishwe na waende kutafakari.
 
Hata akiponda ripoti ya tume,yeye apumzike tu kwa amani.Enough is enough.Haya tunakusubiri karamagi,msabaha rostam na wengine.
 
Wajumbe Bunge limehairishwa ghafra mpaka Saa 5pm. Spika ameomba kwenda kutafuta mwongozo wa Kisheria.
 
Waziri mkuu Edward Lowassa katangaza kujiuzulu.

Masilingi kamtetea hataki ajiuzulu.

Bunge limeahirishwa hadi saa 11 jioni.

Siasa imeanza kuingizwa kupindisha hali halisi.

AIBU AIBU AIBU......

UFISADI ...UFISADI ....UFISADI...
 
Bado Karamagi,Msabaha,na Wengineo.

Cha Msingi Ni Namna Atakavyoweza Kurudisha hizo hela.
 
Hata akiponda ripoti ya tume,yeye apumzike tu kwa amani.Enough is enough.Haya tunakusubiri karamagi,msabaha rostam na wengine.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom