Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Nadhani "katangaza nia ya kuachia ngazi..Kwa vile Mh.Muungwana hajatamka neno...basi bado Lowassa ni PM.'Vinginevyo tusubirie hadi kikao kitakapoendelea Saa 11 jioni.Hii itakuwa historia mpya Tanzania.

Kutokana na ukubwa wa kashfa yenyewe na kwasababu yeye mwenyewe ametamka wazi bungeni kwamba ameomba kujiuzulu, sioni uwezekano wa rais kukataa kujiuzulu huko. Labda kama badala yake anataka kumfukuza/kumfuta kazi.

Rais atakuwa mjinga kweli kuhamisha mabomu kutoka kwa Lowassa na kuyaleta kwake ili yammalize.

Nafikiri hili suala la kujiuzulu ni final na sasa tuanze kufikiria politics za TZ bila Lowassa, Ze Comedy inabidi waanze kufanya maandalizi mapya.

Hivi kuna mtu ana speech nzima ya Lowassa bungeni leo?
 
Wasiwasi wangu ni kuwa, Mafisadi siku zote wana mbinu nyingi za kughilibu umma. Isije ikawa hii ni janja yao kutaka kutuchanganya ifikapo saa kumi na moja wabadilishe maamuzi. Inawezekana walitaka kupima joto!
 
Majingaombwe ya CCM inabidi tuwe macho. Inawezekana kabisa ikifika jioni mbunge mmoja akasimama ni kumuomba EL asijiudhuru halafu mambo yakabadilika. Si ajabu akapewa nafasi ya kujitetea kwanza!!! Usanii wa CCM mpaka nitakaposikia JK amekubali au amejunja balaza la mawaziri ndiyo nitaamini.
 
Chenge,

Atie maji...anajua kipengele kile cha ofisi ya mwanasheria mkuu kutokuwa na msaada kwa serikali, kinamuhusu moja kwa moja na kama JK yupo makini basi hawezi kumwacha Chenge kwenye cabinet kwani anahusika moja kwa moja na mikataba yote ambayo serikali ilisaini ukiondoa huu wa Richmond. Hivyo mapepe yake binafsi nilikuwa nayategemea.
 
Chenge,
atie maji...anajua kipengele kile cha ofisi ya mwanasheria mkuu kutokuwa na msaada kwa serikali, kinamuhusu moja kwa moja na kama JK yupo makini basi hawezi kumwacha Chenge kwenye cabinet kwani anahusika moja kwa moja na mikataba yote ambayo serikali ilisaini ukiondoa huu wa Richmond. Hivyo mapepe yake binafsi nilikuwa nayategemea.
 
Aaaah!! mi nimechoka kusikia mambo kama haya ati wabunge wapige kura!!!?
Why..? Kwani kujiuzulu kwa Lowassa si ni suala binafsi lenye maslahi kwa taifa letu? Ivi huyu Chenge anatafuta nini au na yeye yumo ndani ya circle ya Ufisadi...anaficha nini?

Every individual shuold be responsible for what they did kwa nini Chenge achukue hii kutoka kwa EL!!!!

Bunge letu linatakiwa kutenda kulingana na matakwa ya wananchi na mimi kama mmoja wao nasema sikubaliani na suala la kumuomba huyu mbunge wa Richmonduli abadilishe uamuzi wake wa kujiuzulu...yeye ajuzulu tu.
 
Hapo ndio haja ya kuwepo waziri asiye na wizara maaalum au naibu waziri mkuu inakuwepo. Ila ni washenzi tu hakuna haja ya kuweweseka nani aongoze shughuli za serikali bungeni Batilda Buriani si yupo? yeye si ndio mwakilishi wa waziri mkuu bunge?

Naam mi ndio maana hapa JF niliwahi kuwaambia kile kitabu cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA alichoandika nyerere kina unabii mule,hakuna mtu anayekichambua lakini ipo siku,tusipoangalia mambo haya yalosemwa mule yatatimia.

Lowassa hana haja ya kusema hakupewa nafasi ya kujitetetea. Kamati haikuwa imemtuhumu mtu wala kuform chaji zozote,kamati ilialika watu kwenda mbele yake na kujieleza au kueleza lolote wanalolijua mbona hakwenda? Kisheria kujiuzulu kwa waziri mkuu hakutokani tu na kwamba yeye anahusika na hilo sakata bali ni ministerial responsibility, yeye kama kiranja wa baraza na mawaziri wake wameboronga bado alipaswa kujiuzulu hata kama asingehusika moja kwa moja.

Kama anadai hakupewa nafasi ya kujitetea ama kama anavyodai kuhojiwa? hakupaswa kuwasilisha barua ya kujiuzulu badala yake angewasilisha maelezo ya kujiteteta ili bunge lililomuidhinisha kuwa waziri mkuu lijadili utetezi wake na hatimaye litoe maamuzi,kwa nini kakimbilia kujiuzulu?

Afahamu kamati haikupendekeza aondoke ilimwambia atumie busara zake,sasa kama kujiuzulu na kulalamika ndio busara basi poa
 
Hivi katiba inasemaje kama Waziri mkuu akijiuzulu? Je, is it automatic that balaza lake linakuwa dissolved au ni Rais ndiye anaamua kulivunja?

Naomba kuuliza.
 
Katiba haiko wazi kuhusu hilo,ila waziri mkuu akijiuzulu uwezekano mkubwa kwa rais ni kuvunja au kubadili baraza zima la mawaziri kama ilivyotokea kwa mwinyi miaka ya 1990. Lakini kwa hali ya sasa uamuzi ni wa Rais barza halivunjiki automatically labda kwa nchi ambayo waziri mkuu ndiye kama rais
 
Nampongeza sana EL kwa kuwa mtu wa kwanza PM kuweza kujiudhuru wazifa wake. Hata kama ni kwa kshifa lakini wangapi wanatajwa na kashifa lakini utasikia sing'atuki ng'00

Tuwe na moyo huo wa Tz
 
Karamagi bado yupo tuu? yeye mbona hajiuzuru maana huyu ndio mwizi mkubwa!
 
Uchumi wa nchi unapaa, kumbe yeye uchumi wake binafsi ndio ulikuwa unapaa kutokana na kupokea milungula! Hata kama akipono cha moto anakiona, at least sasa hivi anaweza kuona kuwa bungeni si wote vilaza!!!
 
Sishangai kwa nini PM kajiuzulu kwa sababu kwa kila aliye na akili timamu alitegemea! mimi nafurahi tu!
Lakini nina wasiwasi kujiuzulu kwake kusije kukawa ni changa la macho kwa wa tz, tukasikie eti rais amekataa au hajajibu barua hiyo na kumlazimu huyu bwana kutengua uamuzi wake huku anajua ilikuwa geresha tu!!

Pili, sijui kama tunatakiwa kufurahi tu kwa kuambia PM kajiuzulu au baada ya kusikia kachukuliwa hatua zipi za kinidhamu na kisheria kwa kusaidia kuliingiza taifa kwenye matatizo makubwa, sijui sheria lakini naona kama hili linafanana sana na kosa la jinai!! Wenzetu kule ASIA kama China na Japan tumesikia tu mtu hasa viongozi akidhibitishwa kuhusika na rushwa ni kunyogwa!!

Naomba wa tz tusichekelee hatua hii pekee, bali tuangalia huyu bwana atachukuliwa hatua zipi ili liwe fundisho na kwa yeyote atakaye fuata hapo na viongozi wote kwa ujumla! Pia ripoti ya Mwakyembe imetoa mapendekezo ya kufanya mabadiliko kwenye taasisi kama TAKUKURU, Wizara ya Nishati, wizara ya fedha na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria wote walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mchakato wa kuipata RICHMONDULI!! Watu kama akina Arthur Mwakapugi, D.Yona, Karamagi na Msabaha na wote walio toa ushahidi wa wongo kwa kamati teule wachukile hatua kali kwa kukosa maadlili na uzalendo!!

Hivyo kwa maoni yangu tunacho taka kuona wana JF na watz wenye mapenzi mema, ni kwamba mapendekezo yote kwenye repoti ya Mwakyembe yamefanyiwa kazi!! HAPO NDIPO TUTAHEMA KWA FURAHA KIDOGO

festog
 
Hivi katiba inasemaje kama waziri mkuu akijiuzuru?? Je is it automatic that balaza lake linakuwa dissolved au ni rais ndiye anaamua kulivunja?? Naomba kuuliza.

Katiba haiko wazi kuhusu hilo,ila waziri mkuu akijiuzulu uwezekano mkubwa kwa rais ni kuvunja au kubadili baraza zima la mawaziri kama ilivyotokea kwa mwinyi miaka ya 1990. Lakini kwa hali ya sasa uamuzi ni wa Rais barza halivunjiki automatically labda kwa nchi ambayo waziri mkuu ndiye kama rais

Yes,Baraza linavunjika Automatically kwa mujibu wa Ibara ya 57 (2)(e)

Nanukuu...

Yes,Baraza linavunjika Automatically kwa mujibu wa Ibara ya 57 (2)(e)
Nanukuu...

57.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.

(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(a) Endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia;

(b) Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;

(c) Ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;

(d) Iwapo atachaguliwa kuwa Spika;

(e) Iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;

(f) Ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;

(g) Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Back
Top Bottom