Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Hata akiponda ripoti ya tume,yeye apumzike tu kwa amani.Enough is enough.Haya tunakusubiri karamagi,msabaha rostam na wengine.
 
Spika amechanganyikiwa, inaonekana hakuna namna bora ya kushughulikia hili suala kwa wakati huu ambao EL ametangaza kumuandikia JK kujiuzulu, anaahirisha kikao
 
Hili ni fundisho kwa serikali kuwa mawazo ya upinzani yasipuuziwe.Mnaonaje waziri mkuu akiwa Bernadi Membe?
 
Haki imetendeka kidumu chama cha mapinduzi.

Hiki ni kweli chama cha mapinduzi na sasa ni wakati wa mapinduzi halisi ya chama chetu mafisadi tuwasfishe.
 
Waziri mkuu amejiuzulu kutokana na kashfa ya RICHMONDULI.

Masilingi anamtetea kuwa hajajiuzulu.

Wabunge wa CCM wameitana hivi sasa hapa Dodoma ofisi za mkoa white house.

Waziri Chenge anapiga kampeni Edward Lowasa asijiuzulu.

Wanataka kura ya wazi ipigwe bungeni kukubali au kukataa uamuzi wa kujiuzulu kwa EL.

Jamani tuutokomeze UFISADI na URICHMONDULI
 
Hili nilitarajia kwa kiongozi anayeamini katika demokrasia japo lilitakiwa liwe limetokea siku nyingi
 
Hatimaye, maombi ya Watanzania yamesikika!!


SteveD.

Steve, mimi naona bado sana na natoa wito tuendelee kumuomba Mungu!

Dr. Mwakyembe amesema live kuwa Richmonduli ni mfano wa mikataba mingi mibaya kama vile IPTL, Agreko nk.

Hawa Richimonduli wanalipwa shilingi miloni 200 kwa siku! Wahta a shame na WaTz ndiyo wanaolipia!

Kama alivyosema EL mwenyewe, naungana naye kuwa hajatendewa haki na Kamati ya Mwakyembe maana hawakumuhoji (naamini asingewakwepa kama Mshirika wake wa Kibiashara- Rostam Azizi) maana Msabaha na wengineo walimtaja Waziri Mkuu kama ndiye Mshinikizaji; kwa nini hawakumhoji? LAbda naye angewataja wengine naamini kabisa kuwa angemtaja bosi wake maana vyanzo vyangu vinadai kuwa Richmonduli ulikuwa Mradi wa EL na Bosi wake! HAKI HAIJATENDEKA
 
Kutokumhoji Lowassa nafikiri ni katika mapungufu machache ya hiyo kamati. Hivyo hivyo pia kushindwa kumhoji Karamangi.

Nina uhakika baadaye Dr. Mwakyembe ataelezea kwanini hawakufanya hivyo.

Labda kwasababu hawa jamaa wametunyanyasa sana, sio muhimu tena kuangalia wameangukaje, ila in future kama kuna tuhuma ni vizuri kuwahoji wahusika wote kabla ya hukumu.

Pia kamati ilishindwa kupendekeza adhabu kali kwa Yona na Rostam kwa kukataa kwenda kutoa ushahidi kwenye kamati.

Muhimu kwasasa ni kuondoka kwa Lowassa na fundisho kwa mawaziri wengine. Ukihusika kwenye kashfa utaondoka maana hata PM aliondoka.
 
Alah Akbar...Alah Akbar...Mungu Mkubwa.

Matumaini yamejitokeza...enogh is enough JK sasa tupe Baraza lenye kujali na kupenda nchi yetu..Mungu akujalie ujasiri wa kutekeleza yale uliyoahidi wakati wa kampeni.

Waliokupa hela za kampeni wamesharudisha hela zao...sasa simamia maendeleo ya nchi yetu.
 
hili ni fundisho kwa serikali kuwa mawazo ya upinzani yasipuuziwe.mnaonaje waziri mkuu akiwa bernadi membe?

Mzee, post ya kwanza tu unapendekeza waziri mkuu. Au ndiyo kupima maji. Anyway, Membe is too junior for that post. Nafikiri hata Confidence hana, atakuwa anamuworship JK tu. Si unakumbuka alimtetea kuhusu u-Vasco dagama wake. Mimi nafikiri apewe hat mzee Malecela atuonyeshe alichokuwa anang'ang'ania urais. No mzee mno. May be Mwandosa. Mtu atakayeweza kufanya kazi bila kumtegemea JK. Otherwise, tutakuwa tumeruka mkojo na kukanyaga mavi.
 
Tanzania iliishi kwenye giza kwa muda wa mwaka mzima bila umeme?

Wale waliohusika katika richmond wafirisiwe kwa sababu richmond ilikuwa ikilipwa mil 152 kwa mwezi?/ je hizi hela si zingetengeza na kupanua mabwawa yetu pia hata kukodi umeme uganda kama kenya wanavyofanya.

Kamati tunaipongeza,Na spika azidi kuumbuka kwani alikuwa akizuia kila jambo la wapinzani?

Watanzania tuamke? Waziri anajilimbikizia mali,je wa chini huku halmashauri wataacha?

Tanzania tuamke hasa kanda ya ziwa tumelala sana!

CCM mnaona ya 2008.

Peace!!
 
Mzee, post ya kwanza tu unapendekeza waziri mkuu. Au ndiyo kupima maji. Anyway, Membe is too junior for that post. Nafikiri hata Confidence hana, atakuwa anamuworship JK tu. Si unakumbuka alimtetea kuhusu u-Vasco dagama wake. Mimi nafikiri apewe hat mzee Malecela atuonyeshe alichokuwa anang'ang'ania urais. No mzee mno. May be Mwandosa. Mtu atakayeweza kufanya kazi bila kumtegemea JK. Otherwise, tutakuwa tumeruka mkojo na kukanyaga mavi.

Mkuu,

Tuachane na haya mawazo ya junior au hana uzoefu. Tumeona duniani kote kwamba argument kama hiyo sio ya kweli. Kinachotakiwa ni uwezo wa mtu na
mambo mengine yatakuja tu maana kuna wasaidizi wengi ambao wana uwezo na watamsaidia mhusika pale mwanzoni.

Watu kama akina Blair hawakuwa na experience yoyote na bado walifanya makubwa mno kiuchumi. Pia tuna viongozi wengi sana vijana hapa duniani ambao wameingia bila uzoefu mkubwa.

Hao wazee hawatatusaidia lolote, we need change to our country, real changes, sio recycling ya baadhi ya policies ambazo hata huko nyuma zilifeli. Tunahitaji watu wenye innovative ideas na sio usanii wa akina Lowassa kwamba unaweza kuongeza shule kwa asilimia 200 kwa mwaka bila kuangalia resources zingine.

Mimi nitakuwa tayari kumkubali hata mbunge ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na hata kama hana uzoefu wa kuwa waziri ili mradi awe na uwezo.
 
Tanznia iliishi kwenye giza kwa muda wa mwaka mzima bila umeme??
Wale waliohusika katika richmond wafirisiwe kwa sababu richmond ilikuwa ikilipwa mil 152 kwa mwezi?/ je hizi hela si zingetengeza na kupanua mabwawa yetu pia hata kukodi umeme uganda kama kenya wanavyofanya.

Kamati tunaipongeza,Na spika azidi kuumbuka kwani alikuwa akizuia kila jambo la wapinzani??

Watanzania tuamke?? Waziri anajilimbikizia mali,je wa chini huku halmashauri wataacha??

Tanzania tuamke hasa kanda ya ziwa tumelala sana!1

CCM mnaona ya 2008.

Peace!!


Correction ni Millioni 152 kwa SIKU.
 
is this trueeeeeeeeeeeee? leta evidence bwana..


Wewe mtu habari huna wenzio wanakueleza juu ya Mamvi kumwaga manyanga ngoma nzito unakurupuka na kutaka ushahidi .Jamani mambo mengine si kukimbilia ushahidi wacha utaona ukweli mbele.Hapa ni JF hakuna kulala kitu .
 
Nadhani "katangaza nia ya kuachia ngazi..Kwa vile Mh.Muungwana hajatamka neno...basi bado Lowassa ni PM.'Vinginevyo tusubirie hadi kikao kitakapoendelea Saa 11 jioni.Hii itakuwa historia mpya Tanzania.
 
is this trueeeeeeeeeeeee? leta evidence bwana..


Wewe mtu habari huna wenzio wanakueleza juu ya Mamvi kumwaga manyanga ngoma nzito unakurupuka na kutaka ushahidi .Jamani mambo mengine si kukimbilia ushahidi wacha utaona ukweli mbele.Hapa ni JF hakuna kulala kitu .
 
Back
Top Bottom