Kashfa ya Makamba kuteua katibu(w) Kyela siku yeye anavuliwa gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya Makamba kuteua katibu(w) Kyela siku yeye anavuliwa gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 5, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amemshukia Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba, kwamba alitumia madaraka yake vibaya kutokana na kufanya uteuzi wa Katibu mpya wa chama hicho Wilaya ya Kyela, Joseph Mlozi, siku ambayo yeye na wenzake walikuwa wanajivua gamba.

  “Ameletwa huyu Mlozi kuwa Katibu wa CCM sijui kama atakaa sana sielewi maana kuja kwake hakujanifurahisha, aliteuliwa siku ambayo Makamba na wenzake wanavuliwa gamba…yaani wewe siku ambayo unachishwa kazi unakimbilia kusaini karatasi huyu ateuliwe kwenda Kyela,” alisema na kuhoji: “Unakimbilia wapi?”
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hivi gamba inabidi UJIVUE/UVULIWE au YOTE kama ukikataa basi uvuliwe kinguvu?

  Anyway, kuhusiana na hiyo thread, Makamba kwenye speech yake alisema "anaenda kutayarisha makao"....... Huenda alisahau kwamba alianza tayarisha makao kwenye chama kabla hata ya kujivua gamba............
   
Loading...