Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 15,916
- 15,641
Siku ya jumatano, watanzania hasa wakazi wa dar es salaam kwa shauku kubwa walijazana kwa shauku kubwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Kambarage (maksudi)kumlaki kipenzi chao Richard ambaye umaarufu wake umeongezeka hasa baada ya kujinyakulia kitita cha dola laki moja kutoka big braza.
Nikiwa naangalia mapokezi yake, nilistushwa kuona wanajamii waliowakilisha furaha zetu wakilalama utaratibu mbovu uliotumika kumtorosha Richard ili asionwe na watu. Niliangalia sura za simanzi za wabongo wale ambao walikwenda na maua na mashada yake kumpongeza kuitangaza Tanzania huko sauzi...
Inawezekana waandaaji wa mapokezi wanaugua akili au labda Richard mwenyewe kuamua kutojitokeza mbele ya halaiki. Lakini kwa nini multchoice-Tanzania waliwahamasisha wabongo kujazana uwanjani?? Inasemekana kwamba, kulikuwa kumeandaliwa hafla ya kumpongeza ktk ukumbi fulani, na kila atakayetaka kumwona shurti alipe kiingilio, sasa kinachogomba ktk ubongo wangu ni kwanini basi uwaambie watu wajitokeze kwa wingi uwanjani? Mbona hata kina Kofi Olomide wanalakiwa na watu wengi hata wengine kupiga nae picha ingawa inajulikana amekuja kwa show yenye kiingilio kikali?
Nadhani wababaishaji hawako katika siasa peke yake, hata katika sanaa kuna wababaishaji kinoma. Matajiri wa bongo wapo wachache hivyo kura zao zisingetosha kumpatia ushindi richard, watu walimtwangia kura na sanasana vijana ambao walikuwa wanahamasika kumpa tafu mwenzao. Hivyo kuwanyima fursa ya kumwona angalau hata kuwapungia mkono ni kuwapoka ushindi wao.
Natumaini macho ya JF yalikuwepo pia uwanjani, hivyo watatujuza kilichotokea na wenye kuwafahamu waandaaji wa mapokezi watawahiji ili tuletewe majibu hapa. KWA NINI WABONGO WADHALILISHWE????