Kashfa ya kutisha jeshi la Polisi

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso kupitia Clouds Fm leo asubuhi mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja kama Komba ameshakamatwa kuhusiana na kuwepo mtandao mkubwa ndani na nje ya jeshi hilo unajiusisha na kuwalaghai vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi.

Inasemekana vijana zaidi ya 200 walitapeliwa kiasi cha shillingi 800,000/= kila mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha kujiunga na Chuo cha Polisi Moshi baada ya kuhonga kitita hicho walitakiwa kulipa tena 25,000/= kama nauli ya kuwafikisha Moshi na kweli mabasi matatu yalikodishwa nakuwafikisha Moshi chuoni.

Baada yakufika chuoni taratibu zote za kuwasajili pamoja na kutakiwa kulipia gharama nyingine za kiasi cha shillingi 50,000/=,walinyolewa vipara na kuanza kupiga kwata kama makuruta wengine.

Kwa mshangao wa vijana hao siku ya pili waliitwa nakuambiwa kuwa wanatakiwa kuondoka hapo chuoni kwa vile sio makuruta halali na hawako kwenye kompyuta za chuo.

Kilichowashangaza zaidi ni pale walipokuwa wanatoka kweye lango la chuo kurudi makwao waliyaona mabasi yale yale yaliyowaleta yakiingia na vijana wengine ambao bila shaka nao wlikuwa wameingizwa mkenge!.

Msemaji wa Polisi ameamewataka wote wenye malalamiko au taarifa kuwa walitoa fedha ili kupatiwa ajira na matapeli hao au mawakala wao kutoa ushirikiano utakaowezesha polisi kukamilisha uchunguzi na kupata ushahidiwa kudhibitisha kesi ya Komba iliyopo mahakamani.

Taarifa zitumwe kwa ujumbe wa mfupi kwa ssimu ya IGP namba 0754785557 au kuwasiliana moja kwa moja makao makuu ya Polisi ghorofa namba 4 Ofisi ya Malalamiko.
 
Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la Polisi kupitia Clouds Fm leo asubuhi mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja kama Komba ameshakamatwa kuhusiana na kuwepo mtandao mkubwa ndani na nje ya jeshi hilo unajiusisha na kuwalaghai vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi.
Inasemekana vijana zaidi ya 200 walitapeliwa kiasi cha shillingi 800,000/= kila mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha kujiunga na Chuo cha Polisi Moshi baada ya kuhonga kitita hicho walitakiwa kulipa tena 25,000/= kama nauli ya kuwafikisha Moshi na kweli mabasi matatu yalikodishwa nakuwafikisha Moshi chuoni.
Baada yakufika chuoni taratibu zote za kuwasajili pamoja na kutakiwa kulipia gharama nyingine za kiasi cha shillingi 50,000/=,walinyolewa vipara na kuanza kupiga kwata kama makuruta wengine.
Kwa mshangao wa vijana hao siku ya pili waliitwa nakuambiwa kuwa wanatakiwa kuondoka hapo chuoni kwa vile sio makuruta halali na hawako kwenye kompyuta za chuo.
Kilichowashangaza zaidi ni pale walipokuwa wanatoka kweye lango la chuo kurudi makwao waliyaona mabasi yale yale yaliyowaleta yakiingia na vijana wengine ambao bila shaka nao wlikuwa wameingizwa mkenge!.

Hivi hizo taratibu za usajili zilifanyika pale pale chuoni Moshi au nje ya chuo?
 
Jk vunja hili jeshi ili walau tukuone upo serious,unataka wafanye nini ujue wameoza hawa?
 
sasa kama hata polisi wanaingizwa kwa rushwa au wanatoa rushwa ili wapate hizo nafasi, hivi ni nani atayebaki kweli kwenye hii ishu ya rushwa?? Nadhani ni mimi tu
sawa kabisa, nchi inatisha na ujumbe tunaouachia uzazi ujao ni balaa tupu.
 
Sasa kama hata Polisi wanaingizwa kwa rushwa au wanatoa Rushwa ili wapate hizo nafasi, hivi ni nani atayebaki kweli kwenye hii ishu ya rushwa?? Nadhani ni mimi tu

na mimi mkuu Elli ,kimsingi polisi ni uozo mtupu,unakumbuka ishu ya mke wa Chagonja?
 
Last edited by a moderator:
huyo komba wasijifanye hawamjui,wana ufamily friend na family ya chagonja.huyo babake komba (R.I.P) alikuwa ni rafiki mkubwa wa chagonja kipindi hicho wote wakiwa wana nyota moja huko mkoani mbeya.na hii connection inapitia moja kwa moja kwa mke wa chagonja na anachofanya komba ni kutafuta tu watu wanaohitaji ajira.
 
Tumefika hatua mbaya sana. Wtasajiliwaje pale chuo bila uongozi wa chuo kuwa na taarifa. Hii ni 'coordinated crime' ya hali ya juu sana. Mwema aadabishwe!
 
Polisi ni sehemu ya jamii yetu, jamii yetu yenyewe inaabudu rushwa kwa hiyo mi sishangai maana jamii yetu yote ndo ilivyo. Mbona hamshangai wajumbe wa NEC ya CCM kupatikana kwa rushwa wakati hiki chombo maamuzi yake ni makubwa kwa nchi yetu?
 
Mpwa ukianza kuhesabu ishu zao utakuja kuchanganyikiwa maana kuna mtu mmoja tena mwenye cheio kikubwa cha Polisi, siku moja vijana wake walikamata Godauni (sp) kumbe ni mchongo wa huyo Kigogo basi lie godown, jamaa wakanunua kufuli wakafunga ili mzigo usitoke, huwezi amini kila kitu kilihamishwa usiku ule ule next morning wanakuja kukuta hamna kitu kabisa na kufuli limefungwa, kumbe ni ishu ya Kamanda fulani...mmmh ni mengi sana
na mimi mkuu Elli ,kimsingi polisi ni uozo mtupu,unakumbuka ishu ya mke wa Chagonja?
 
Dawa ya upumbafu kama huo ni wetu sisi wananchi hasa walio zezeta katika kupambana na maisha yao, naomba adhabu kubwa ianzie kwa hao vijana ambao ni vilaza wanao amini uwezi fanikiwa bila hongo, na hao ndio watakuwa wa kwanza kuomba rushwa baada ya kumaliza mafunzo, nadhani elimu na uraia inatakiwa kwa vijana wote, huko wapi uzalendo wa nchi yao,je huko police kuna biashara gani hadi utoe laki nane, rushwa itakwisha siku watoa rushwa wataacha kutoa, waombaji wapo siku zote,
Amka vijana
Amka tanzania
 
Niliapa kutowapa ushirikiano polisi kwa jambo lolote lile na pia sitaki msaada wao
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom