Kashfa ya EPA: Mwanyika azidi kujichanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya EPA: Mwanyika azidi kujichanganya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Mar 9, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  TIMU YA RAIS YA UCHUNGUZI WA FEDHA ZA EPA

  TAARIFA KWA UMMA


  Kama mnavyofahamu tarehe 08 Januari, 2008 Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete aliunda Timu inayojumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili, pamoja na mambo mengine, kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria kwa makampuni na watuhumiwa wa upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Mheshimiwa Rais alituagiza kuwa tuwe tumekamilisha kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita.

  Taarifa hii ya tatu inatolewa kufafanua na kutoa taarifa ya namna kazi inavyoendelea kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais takriban miezi miwili iliyopita.

  Timu inapenda kuufahamisha umma kuwa pamoja na majukumu mengi iliyopewa, kwa sasa Timu imejikita katika kufanya uchunguzi wa kitaalam na wa kina. Kwa msingi huo, pamoja na fedha zinazorudishwa, ni vyema Umma na Wanahabari wakafahamu kuwa kazi ya uchunguzi haijafika mwisho na kwa sasa Timu inaona ni vyema kutotoa taarifa ambazo zitaathiri kazi ya uchunguzi inayoendelea. Tunapenda kuusihi Umma na Wanahabari kuwa na subira wakati kazi hii inaendelea.

  Hata hivyo, Timu inapenda kuuhakikishia Umma na Vyombo vya Habari kuwa kazi hii ya uchunguzi inaendelea vizuri na Timu inapata ushirikiano mzuri kutoka kwa makampuni na wamiliki wanaohusika na upotevu wa fedha za EPA.

  Vilevile tunapenda kuukumbusha Umma na Wanahabari kuwa Timu imepewa miezi sita ya kufanya kazi na hatimaye kuwasilisha Taarifa kwa Mheshimiwa Rais. Huu ni mwezi wa pili tangu Timu ianze kazi yake. Kwa msingi huo, Timu inawasihi Umma na Wanahabari kuwa na subira kwani Wahenga walisema SUBIRA YAVUTA HERI. Tunawahakakishia kuwa kazi inaendelea vizuri na heri yaja kwani tulichonacho hadi sasa katika uchunguzi si haba.

  Vilevile Timu inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maswali na malalamiko ya kutokamatwa kwa waliohusika. Tunapenda kuueleza umma kwamba uchunguzi wetu hadi hivi sasa unaonyesha kwamba wahusika wakuu ni makampuni. Kisheria, makampuni hayo ni mtu yaani ‘Legal Person'. Hata hivyo, makampuni hayo ni tofauti na mtu wa kawaida. Kampuni katika maana hii, inajitegemea yenyewe.

  Kwa msingi huo, ikiwa kampuni imefanya kosa, kuna utaratibu wa kufuata kisheria. Kazi inayofanyika hivi sasa, ni uchunguzi wa kina kuhusu maafisa wa makampuni hayo ili kufahamu ni kitu gani kilichosababisha hali hiyo kutokea. Uchunguzi huu unaendelea na ndiyo utakaotuwezesha kujua hatua za kisheria zitakazochukuliwa.

  Timu inapenda kuutarifu Umma na Wanahabari kuwa itaendelea kutoa taarifa ambazo inaamini hazitaathiri uchunguzi unaoendelea mara kwa mara.

  Imetolewa na Johnson P.M Mwanyika,
  Mwenyekiti wa Timu
  9 Machi, 2008


  Hii ni taarifa aliyoitoa leo lakizi sidhani kama inajibu maswali ya msingi ambayo watanzania tunataka majibu yake hivi sasa.
  Kwani guyo legal person hawezi kutajwa ili watu wamfahamu?
  Huo uchunguzi wa kina unaofanywa ni upi wakati Ernst & Young walishamwaga kila kitu?
  Tunayeyushwa?
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Naamini AG hakuandika hii taarifa bali imeandikwa na yeye akapewa kuja kusoma tu bila ya kuitafakari .Tanzanai bwana ina maajabu .
   
 3. M

  Msavila JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  ENRON ilikuwa kampuni na walioshitakiwa ni uongozi wa kampuni . Mbona unaanza kututia mchanga machoni mapema hivi? Je sheria ndivyo zilivyo hapa kwetu???
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Naona umefika wakati tuwazirie nchi tu ili yaishe wafanya wanavyofanya; inawezekanaje mtu kwa taarifa ya ukurasa mmoja atoe kauli mbili zinazopingana?
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa ngozi imekamatwa na mtu aliyekutwa na ngozi huyu hapa..na ngozi imerudishwa!

  Eti aliyekutwa na ngozi hakuna sababu kisheria kumweka ndani!

  Mimi narudia tena -Tz ole wako ukamatwe ukiwa umeiba kuku..yaani utafungwa tu ndugu yangu!

  Ila ukiiba pesa nyingi.. poa na utapeta tu..sana sana watu wataanza kusema mnamwonea gere/wivu!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu sasa analeta usanii, taarifa mnatoa ninyi wenyewe (serikali) kuwa pesa zinarudishwa halafu mnakuja kusema sio sahihi kutoa taarifa!. Huyu awekwe chumba kimoja na Mkulo wapate kusemezana maana yaonyesha wanatumikia serikali tofauti.
   
 7. k

  kipanga mweupe Member

  #7
  Mar 9, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajumuia na Watanzania wenzangu....naona sasa hili suala la pesa za EPA linaanza kuzungushwa sababu tu ni ule usemi wa mwenzetu unaanza kufanya kazi.

  Haingii akilini jinsi tume inavyotoa taarifa kwa usiri usiri wakati kampuni ya Ernst & Young ilimwaga hadharani majina ya makampuni yote...........kuna kitu gani hapo??

  Unapotuambia kuwa kampuni is an independent entity, tunalielewa hilo lakini kampuni inapokosea muwajibishwaji ni nani? Kama si uongozi wa hiyo kampuni?

  Wacheni kulindana, hapo tunaanza kuona changa la macho hiloooooooo kwa Wadanganyika[/B.

  Lakini iko siku!!!! kumbuka Malawi, Zambia, Kenya (juzi juzi) na of current Malaysia mabadiliko ya kisiasa ambayo hayakutarajiwa yanajitokeza kila kukicha na bila kutegemea.....A WIND OF CHANGE WILL COME!!!!

  Mungu Ibariki Tanzania na Ubariki Kizazi cha Wanyonge wa Tanzania
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145  Mimi nilitegemea Rais wetu baada ya kujizolea sifa za kumleta Bush Tanzania na baadaye kusemekana kwamba kaufanikisha usuluhishi wa Kenya kumetulia , nilietegemea atahamia Zanzibar na hata Uchafu wa EPA na BOT ? Nimeanza kupatwa na wasi wasi kwamba kuna jambo hapa .Hivi Pinda na kamati yake haijamaliza kazi kujua hawa akina AG na Hosea wanasimamia wapi ?Au ndiyo ngoma ilisha toka no more damage ?
   
 9. A

  August JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Majina haya wezi kutolewa sasa hivi ili waweze kupewa Tenda Nyingine Serekalini , ambazo zitawewezesha kurudisha pesa ya EPA, na kwa kesi ngumu kutafuta Vijana wa Mtaani ili kuwa uzia kesi, bigshot , wasalimike ili waje wawatoe Vijana
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280


  salaleh!! Masatu umeokoka lini?
   
 11. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kipanga Mweupe karibu katika jamvi la JF.
   
 12. peace2007

  peace2007 JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 214
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Vilevile Timu inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maswali na malalamiko ya kutokamatwa kwa waliohusika. Tunapenda kuueleza umma kwamba uchunguzi wetu hadi hivi sasa unaonyesha kwamba wahusika wakuu ni makampuni. Kisheria, makampuni hayo ni mtu yaani ‘Legal Person’. Hata hivyo, makampuni hayo ni tofauti na mtu wa kawaida. Kampuni katika maana hii, inajitegemea yenyewe.


  Kwa hiyo hao waliorudisha hizo 50 billions ni makampuni "legal persons" na sio wakurugenzi wa hayo makampuni???? Manake nini??? Hao wakurugenzi hawakamatiki wakati ndio wamewaletea hizo pesa???? Hivi ingekuwa kampuni yangu imegushi malipo ya serikali wangesema mimi kama mkurugenzi sikamatiki kwani kuna utaratibu maalumu? THUBUTU....MWANYIKA HII NI DANGANYA TOTO
   
 13. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Yule bilionea wa Urusi wa kampuni ya mafuta Mikhail Khodorkovsky yuko gerezani kwa kosa la kukwepa kodi. Inaeleweka kwamba kampuni yake ya mafuta ndio ilikwepa kodi lakini yeye ndio alikuwa mmiliki na (Mkurugenzi(?)).

  Sasa kampuni ikifanya kosa anayewajibika ni uongozi, kampuni ikiibia serikali anyewajibika ni mkurugenzi au uongozi. Wataalamu wa sheria watusaidie hapa kuhusu sheria za makampuni za Tanzania, na sheria za jinai kwa upande wa makampuni.
   
 14. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu nikidhani aliyeandika hapo ni kipanga mweupe, au macho yangu ndo hayaoni?
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pamoja na yoote hayo bado tu kuna kenge wanataka uamini eti JK kiboko, anatisha and yuko very serious kucombat ufisadi. Kinachoonekana hapo hiyo tume imeundwa makusudi na JK ikifanya kazi ya kuneutralize hii ishu na baada ya hiyo miezi sita watakuja na ripoti sawa kabisa na ile ya Takukuru kuhusu Richmond!!!!!!!!!! pambaaaaaaf!
   
 16. G

  Gus Member

  #16
  Mar 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili suala la EPA limewapa nafasi watoto wa kiume kuongeza umbea, kama mnataka data za uhakika hebu zifanyieni kazi. kwa taarifa yenu, baadhi ya wazungu walioko hapa bongo wana taarifa kibao lakini wanatuangalia kama vitoyi. mnafikiri IMF iliyotoa maagizo kwamba oditing ifanyike hawana data hii? wanayo! wanatuchora tu. na watoto wa kiume mmekaa kunong'ona hapa. andikeni barua banki ya dunia na hao imf watoe taarifa waliyonayo.
  jk hawezi kuwaanika, kwani hamjui hilo? mnafikiri wale wote waliofadhili kampeni yake walitoa wapi hizo hela?
   
 17. Tulamanya

  Tulamanya Senior Member

  #17
  Mar 10, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kijana kwanza karibu JF!

  Pili, sikuelewi unataka kusema nini hasa hapa! Wewe IMF wanakuhusu nini? Sisi tunataka serikali yetu iwajibike kwetu ndo maana tunaipa pressure kufanya mambo bila kupindisha sheria na taratibu tulizo jiwekea!!
  We bwana mdogo, si kwamba watu hapa hawajui nani anahusika na EPA Scam, watu hawa wanajulikana vizuri kabisa, tunachotaka ni serikali yetu kudhibitisha haya tuliyo nayo na kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani, kuwafilisi mali walizo nazo etc na sio hizi blabla za Mwanyika ambaye yeye mwenyewe hatuna imani naye cause inatakiwa ajihuzulu kufuatana na Richmonduli Scam! hapa anatapatapa tu kama mfa maji! Kwani nani aliwaambia watoe progress report kama si kujikanyaga tu?

  IMF au World bank uwaandikie barua wakwambiaje tena?
   
 18. L

  Lione Senior Member

  #18
  Mar 10, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nivigumu kweli kuamini mambo haya yanavyokwenda na kutokea,unajua jamaa wanatufanya wote wajinga kabisaaa!hivi kweli kama mtuhumiwa ni kampuni,legal person,kama asemavyo mwanyika,kampuni ilienda bank kuu,ikanegotiate huo wizi,ikafanikisha?ama ni mtu mwenye kampuni?mbona siwaelewi hawa jamaa?mwanyika inamaana wewe sio mtanzania?mwanyika huna uchungu na hii inchi?mwanyika ulisoma kule upareni,kwa kodi za hawahawa watanzania unaowasiliti leo,utazikwa wapi weye?mwanyika na wenzio,mnajisikiaje mnapopita huko nahuko mkiona watoto wakifa kisa hakuna panadol kule hospitali?mwanyika hao unaowatetea hawatakuzika,nisie wana watanzania,mwanyika hebu geuka nyuma uone ulipotoka,kule kwa mama yako upareni,angalia ule umasikini unaonyanyasa watu pale,unadhani wanapenda kua vile?wanajitahidi kila kukicha,ilajitahada zao zinakwamishwa na hao unaowatetea,mwanyika umewasaliti,mwanyika hakika hawakuelewi,mwanyika,kwanini lakini?mwanyika ni tumbo tu ndo linakubadilisha kiasi hicho?mwanyika unajua kwamba ukila sana kuna kuvimbewa?na moja wapo ya dawa za kuvimbewa ni kutapishwa,unataka wakutapishe?mwanyika?kweli niwewe?mwanyika wewe?
   
 19. Think Global RC

  Think Global RC Member

  #19
  Mar 10, 2008
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu zangu lazima tuwe wakweli kwa nafsi zetu. mwanyika na hosea hawawezi kujisafisha hata kidogo.leo kuna watu wanataabika kuliko maelezo,nimetembelea vijijini watu wanafungwa,wanteshwa kwa kuwa hawana hela za kuchangia maendeleo. huu sio utawala bora kabisa, leo wale waliotufikisha hapa tulipo wao ni miungu watu hawapaswi kutajwa hadharani. kuna sababu gani za msingi za kuendelea kumuacha hosea atambe wakati yeye ndie aliyepotosha ukweli wa richmonduli kwa kutumia fedha za masikini walipa kodi wa tanzania.mwenye wazo la nn kifanyike, let us work together 2 make things go in proper direction.
   
 20. Wakunyuti

  Wakunyuti JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilishasema na nitaendelea kusema.. sisi watanzania tunaonekana malofa na hata watanzania wenzetu wenyewe wacha wazungu tu...sasa huyu jamaa na ripoti yake anaamua kuitoa huku akijua ni ya uzishi mtupu na haijitoshelezi lakini anajua mwisho wa siku watanzania watakubali tu na mambo yatapita na shughuli zitaendelea kama kawaida..hivi ndivyo jinsi watanzania tulivyolelewa na kufundishwa na ndio jinsi tulivyo ikubali hali kama hii ya kuwa wapole katika kila ishu, zote pamoja na unyeti wake..makelele tuna piga lakini baada ya muda tuna nyamaza na tunasahauu.........''LET US STOP THIS''..hawa jamaa tunawapa urahisi sana wakuiongoza hii nchi..as if wanaongoza miti tu..jamani tuwe wazalendo sasa..ripoti za kejeli kama hizi tuwe tunazipinga kwa nguvu zote na kwa njia zote bila kuchoka.. this is KITUKO..


  Nimtazamo tu wananchi msijenge chuki''
   
Loading...