Kashfa ya "degree ya chupi": Mkuu wa wilaya ya Korogwe kizimbani

Yaaah ana yo haki kama watuhumiwa wengine!
Na hapo ana chukuliwa kama mteja wao!

Eti kwenye hii kesi huyo mkuu wa wilaya alikuwa na haki ya kutetewa na ofisi ya mwanasheria mkuu?
 
huyu jamaa maneno ya shombo ndo yake
aliwahi kumwambia mtu 'asiwe anafikiria kwa kutumia tumbo' lol
 
afadhali, mambo ya 'kuzaririsha' wanawake yapungue.

Huwa naona hata nikiwa kwenye daladala, mdada anapita na kimkoko chake, akifanya tu kosa utasikia konda anamwambia 'gari yenyewe ya kyupi'
 
Hapa nataka kujua Mwanasheriandio amepata elimu ya kichupichupi au huyu aliyeteuliwa ndiyo aliteuliwa ki.............chu...............
 
Wapi alisoma haijalishi ila kwa DC kutoa maneno kama hayo ni kudhihaki kiti chake. Aliyepiga walimu wazembe mkoani Kagera alifukuzwa kazi. Nashangaa kwanini Gumbo bado yuko ofisini.

Huyo aliyewapiga bakora walimu ameshinda u NEC huko Nachingwea. CCM ni wasanii na akili zao zinafanana. Kauli ya Pinda ya LIWALO NA LIWE ilidhibitisha kuwa nchi hii haina mtawala.
Ndo maana kuna Marais zaidi ya mia hapa Tanzania, mf rais wa wasafi, rais wa manzese, rais wa masharobaro. The list continues,,,,,,,,,,,,,
 
Hapo kachukuliwa kama mkuu wa wilaya!
Siunajua serikali yetuz.

Japo inapofika mahakamani ana hukumiwa kama mtu binafsi na alitakiwa awe na lawyer wake!

Hapo ndipo utajua watu hatu fanani. Maana unapo kuwa mtumishi wa umma ukisimama kizimbani cheo kina wekwa pembani na tuna shughulika na sheria!

Kwa kifupi ana kingiwa kifua!
[QUOTEkif=EMT;4843278]Kivipi? Kesi inamhusu yeye binafsi au kama mkuu wa wilaya?[/QUOTE]
 
KIkwete rais wa ajabu! Yaani hajamwajibisha huyu muhuni wake? Hata kama wanajuana walivyovuana chupi na kupeana shahada, Gumbo hakupaswa kuyasema aliyosema hadharani. Je katika mchezo huu rais anafaidika vipi? Je huu si ushahidi kuwa aliridhika na mwakilishi wake kumtukana bi wa watu? Ningekuwa huyu bi mkubwa ningemshitaki Gumbo na aliyemteua under vicarious accountability and liability.

Hii ni kesi ambayo huyu binti angeishinda kirahisi. Alivyomdhalilisha mbele za watu hana thamani. inabidi adai thamani yake mbele ya jamii irudishwe!
 
Hapo tutakuwa tuna muonea mahana aliye mchagua hakumtuma akatumie hiyo lugha labda ithibitike pasi na shaka mwajili wake ame mtuma afanye hivyo.

Kwa swala hili ni vigumu kumuhusisha muajili kwa kosa la mwajiliwa.

Mwajiliwa ata beba mzigo wake mwenyewe!

KIkwete rais wa ajabu! Yaani hajamwajibisha huyu muhuni wake? Hata kama wanajuana walivyovuana chupi na kupeana shahada, Gumbo hakupaswa kuyasema aliyosema hadharani. Je katika mchezo huu rais anafaidika vipi? Je huu si ushahidi kuwa aliridhika na mwakilishi wake kumtukana bi wa watu? Ningekuwa huyu bi mkubwa ningemshitaki Gumbo na aliyemteua under vicarious accountability and liability.
 
Jamani huyo Mkuu wa Wilaya amekosa nidhamu kwa kiwango cha juu. Bahati NZuri huyo Mwanasheria namfahamu saana, amesoma na kupata Shahada yake katika Chuo kikuu cha Tumaini huko Iringa!!!
 
Kosa la aliyemtuma ni kutomwajibisha anapoonyesha wazi kushindwa kufikia viwango ambavyo ni kuwahudumia wale waliomchagua aliyemwajiri kwa adabu na staha. Hii kwa kimombo huitwa vicarious accountability. Hili halina mjadala. Mwanao akiiba kama hutamchukulia hatua nawe unalaumiwa. Simple.
 
Adhabu atakayopata ni kuhamishiwa wilaya nyingine.
 
mkuu wa wilaya ya korogwe, mrisho gambo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya korogwe jana kwa shtaka la kumkashifu mwanasheria wa halmashauri ya mji korogwe kuwa ana stashahada ya chupi. Katika kesi hiyo, hakimu alikataa mwanasheria mkuu wa serikali kumwakilisha mkuu huyo wa wilaya katika kesi ya madai ya shilingi milioni 96 dhidi yake.

Katika kesi hiyo na. 7/ 2012 mlalamikaji ni mwanasheria wa halmashauri ya mji korogwe, najum tekka anayedai kukashifiwa na gambo wakati wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwamba stashahada ya sheria aliyopata mtumishi huyo ni ya chupi.

Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo wa wilaya alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kisha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo hamis salum, mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe mwanasheria mkuu wa serikali ambaye aliwakilishwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, rebecca msalangi kwa kuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha gambo kwenye shauri hilo.

mimi sina imani na hakimu. Ni utashi wangu tu kutokana na hali ya tanzania ilivyo. Nashauri jopo la mahakimu kama inawezekana. Sisemi hatatoa haki. La. Nachosema tanzania aliyotuletea mshua ??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????? Mmmmmmmmh! Sijui!
 
Jamani huyo Mkuu wa Wilaya amekosa nidhamu kwa kiwango cha juu. Bahati NZuri huyo Mwanasheria namfahamu saana, amesoma na kupata Shahada yake katika Chuo kikuu cha Tumaini huko Iringa!!!

Tumaini Uni? Mh, aisee Tumaini, Tumaini, nami nina mashaka! (wazee wa First class na upper seconds!?"
 
Kosa la aliyemtuma ni kutomwajibisha anapoonyesha wazi kushindwa kufikia viwango ambavyo ni kuwahudumia wale waliomchagua aliyemwajiri kwa adabu na staha. Hii kwa kimombo huitwa vicarious accountability. Hili halina mjadala. Mwanao akiiba kama hutamchukulia hatua nawe unalaumiwa. Simple.

Labda maoni yako yamesikilizwa.
 
Back
Top Bottom