Kashfa ya Bil. 40Tshs Magereza: Matumizi ya Mkataba wa Mfumo wa Usajili wa Wafungwa

Mambo ya perception vs. reality.....

Mimi nadhani rais atawasamehe kama wakikubali kurudisha hizo pesa kinyemela ref Kikwete). Hawa watu ukiwakamata uchumi wa nchi unaweza kuyumba (ref Punda). Mambo ya jeshi hayajadiliwi na miradi ya jeshi ni siri haitakiwi kujadiliwa na chombo chochote nchini (Pinda).

Naomba Mh Anna Makinda asizimishe hoja hizi zikiletwa ndani ya bunge ili kujadiliwa. Tunataka kujua usalama wa pesa za nchi yetu mikononi mwa hao tuliowapa? au kujinyakulia uongozi wa taifa let
 
Fuatilia kwa makini but dont make it personal.

Utaachaje kuifanya kuwa personal wakati unaona kabisa watoto wako wanakosa elimu bora, afya ni mgogoro na makazi yako hayakufanyi utamani kurudi nyumbani kufurahi na familia. Nakwakuwa amani haipo nyumbani umeamua kuhamishia makazi kwenye Bar? Wakati huo huo jirani yako yy ni kiyoyozi kuanzia barabarani mpaka chumbani..no utra violet rays zina igusa ngozi yake, amani yao nyumbani ni tele tabasamu la mkewe/mumeo ni pana na watoto wao ni kama maua katika bustani yao pale nyumbani kwao kwa afya nzuri na ngozi nyororo walizonazo? Kama waweza kutoifanya personal basi Mbingu ni yako maana umefanikiwa kuenenda katika roho na si katika mwili huu wa damu na nyama, na hisia zako zimekufa kabisa pia akili yako hasa ile inayoongozwa na reflex system like kufunga jicho mtu anapokuwekea kidole ime expire!

Hili ni janga la kitaifa kwani almost everybody is becoming a hero anapofanikiwa kukwapua public funds. Let me console myself with these words...Lord our God Jehova is alive, is never weary nor slumber; hakuna udhalimu ulioshinda kwakuwakandamiza wanyonge unfortunately History never lies! In one of my old post niliutangazia ufisadi ukomo wake nikatabiri anguko lao...inaonekana somo hili ni juu ya kiwango cha uelewa wao....The new Tanzania's mother is in a labour ward groaning from the labour pain naomba Mungu niwe hai pale atakapo deliver na kutuletea a bouncing baby BOY!:smile-big:
 
HAPO KUNA MINJA,MBOYA UNATEGEMEA NINI?KWA NINI DEAL NYINGI ZA WIZI WA FEDHA MCHAGA HAKOSEKANI?nauliza wana JF au ndio maana nyerere aliapa wasipewe urais wa nchi?
 
HAPO KUNA MINJA,MBOYA UNATEGEMEA NINI?KWA NINI DEAL NYINGI ZA WIZI WA FEDHA MCHAGA HAKOSEKANI?nauliza wana JF au ndio maana nyerere aliapa wasipewe urais wa nchi?

EE Mwenye enzi Mungu, muumba mbigu na nchi na vyote vilivyomo wafumbue macho watanzania ili wafanye maamuzi magumu juu ya mstakabali wa nchi yao, kwani hawajui lolote. Tunaomba na Kushukuru, na wote tuseme Amen.
 
Habari Leo Novemba 13, 2010

VIONGOZI wakuu wa Jeshi la Magereza nchini wanakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya Sh bilioni 40 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mfumo mpya wa kusajili wafungwa ujulikanao kama Offenders Management Information System (OMIS), kinyume na taratibu za sheria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyanzo vya uhakika kutoka ndani na nje ya Jeshi hilo,
kutokana na shinikizo la uongozi wa juu, Magereza ilijikuta ikiingia mkataba wa mradi huo kinyemela, kwani ulikataliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kutokana na kuwa na kasoro kubwa.

Taarifa hiyo inaeleza, kwamba mkataba huo ulianza kutekelezwa kibabe mara tu Serikali ilipotoa fedha za utekelezaji wa mradi huo katika mwaka wa fedha wa 2006/07, baada ya Serikali kuridhishwa na andiko la mradi huo, ambalo lilikuwa limeeleza vizuri juu ya taratibu zilizopaswa kutumika, katika utekelezaji wa mradi huo.


Andiko hilo lililoandaliwa na aliyepaswa kuwa Meneja Mradi, Abdallah Zawadi, liliombewa fedha kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo Novemba 27, 2006 Rais Jakaya Kikwete alitoa baraka za utekelezaji wa mradi huo.


Vielelezo ambavyo gazeti hili limevishuhudia katika ofisi za makao makuu ya Jeshi hilo vinaonesha kuwa, Machi 13, 2008, Wizara ya Mambo ya Ndani ilimwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro, barua yenye kumbukumbu namba CAB. 48/468/01/89 ikimfahamisha kuwa ombi la utekelezaji wa mradi huo lilikubaliwa ili utekelezaji wa mradi huo uanze mara moja.


Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Jeshi hilo kililiambia gazeti hili, kwamba baada ya barua hiyo kulikuwa na mazungumzo ya chini kwa chini kati ya Kamishna Nanyaro na
Bodi ya Zabuni, ambapo baadaye walitoa zabuni kinyemela kwa Kampuni iitwayo GIVA Tanzania Limited kuwa ndiye mtekelezaji mkuu wa mradi huo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kwa kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kutekeleza mradi huo, pia Bodi hiyo ililazimika kupitisha kampuni za TIBURON INC ya Marekani na CMC Ltd ya India, kuwa washindi wengine wa zabuni hiyo, ili washirikiane na kampuni hiyo (GIVA) na kuruhusu mkataba uandaliwe.


Moja ya nyaraka ambazo gazeti hili imezipitia zinaonesha kuwa kutokana na agizo hilo, kupitia barua yenye kumbukumbu namba P.2751/a/31, Makao Makuu ya Magereza ilimteua ACP Zawadi kuwa msimamizi wa mradi huo na kumtaka aandae mkataba na kumshauri Kamishna Mkuu wa Magereza, juu ya utekelezaji wa mradi huo naye akiwa Meneja Mkuu wa Mradi.


Chanzo kinaeleza kwamba ACP Zawadi baada ya kupitia nyaraka za Kampuni ya GIVA hakuridhishwa na uwezo wa kampuni hiyo katika utekelezaji wa mradi huo, hivyo mara kadhaa alimshauri Kamishna Nanyaro kuachana na kampuni hiyo, jambo ambalo lilipingwa.


Katika barua yake kwa Kamishna Mkuu wa Magereza yenye kumbukumbu namba PF 2010/Vol.1/2 ya Aprili 16, 2010 yenye kichwa cha habari: Ushauri na Usimamizi wa Mradi wa OMIS, ACP Zawadi alishauri kwamba mkataba huo ulipaswa kuandaliwa kwa kushirikisha watendaji wakuu wa mradi huo.


Watendaji hao ni Jeshi la Magereza, wataalamu kutoka Kampuni ya TIBURON INC ya Marekani, wataalamu wa CMC ya India na wawakilishi kutoka GIVA Tanzania Ltd ili kuweka wazi udhaifu ambao ungejitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.


Kwa mujibu wa barua hiyo, ACP Zawadi alionesha wazi kuwa GIVA licha ya kuwa ndiyo ilikuwa mzabuni mkuu, haikuwa na utaalamu juu ya kazi hiyo, lakini ilipewa zabuni ambayo iliitaka kushirikisha TIBURO INC ambayo imebobea katika teknolojia ya kuratibu shughuli

za wafungwa, kupitia mitandao ya kompyuta na Kampuni ya CMC ambayo imebobea katika mfumo wa kompyuta wa kuchukua alama za vidole.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya ACP kuonekana ni kikwazo katika mradi huo kutokana na ushauri ambao haukumfurahisha Nanyaro, aliondolewa katika uandaaji wa mkataba na usimamizi wa mradi huo, hivyo Kamishna aliwakabidhi kazi hiyo maofisa wake wawili - DCP Minja na CP Mboya, kuandaa mkataba huo kwa siri na kupuuza ushauri wa ACP Zawadi, licha ya kwamba maofisa hao hawana utaalamu wa kutosha katika fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.


CP Mboya alipoulizwa kuhusu jambo hilo alikiri kuhusika. Kwa upande mwingine DCP Minja hakupatikana kwa kuwa yuko masomoni nje ya nchi.


Chanzo hicho kinaeleza kwamba baada ya maofisa hao kuandaa mkataba huo kwa kushirikiana na Nanyaro mwenyewe, waliupeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mei 23, 2008.


Mkataba huo uliambatana na barua kumbukumbu namba HQC.80/PMIS/iv/26, iliyokuwa ikimshawishi AG kubariki mkataba huo.


Hata hivyo, nyaraka ambazo gazeti hili limezipata kutoka ofisi ya AG zinaonesha kuwa alikataa kusaini mkataba huo.


Kwa mfano, kupitia barua yake yenye kumbukumbu Na.JC/130/11/4 ya Juni ,2008 ambayo ilisainiwa na Pius Mboya, AG alikataa kusaini mkataba huo kwa kuwa ulikuwa na upungufu na kuagiza uandaliwe upya kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.


"Tumepitia makubaliano yenu na wazabuni, lakini tumebaini upungufu kadhaa, hivyo si vizuri kusaini mkataba huo kabla ya kuufanyia marekebisho," ilisema barua hiyo.


Barua hiyo inaeleza: "… barua yenu inaonesha kuwa zabuni ya mradi huo imetolewa kwa Kampuni ya GIVA Tanzania Ltd, wakati hati ya makubaliano inaonesha kuwa kuna kampuni nyingine mbili, hivyo muandae mkataba mpya utakaoshirikisha kampuni zote".


Baada ya uongozi wa Magereza kukaa kimya, Mei 20, mwaka jana, AG alimwandikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati huo, Patrick Rutabanzibwa,
barua yenye kumbukumbu Na.ACJC/a.130/11/1 ikimtaka kutosaini mkataba huo hadi utakapobarikiwa na ofisi yake, baada ya kurekebishwa Upungufu uliomo.

Licha ya hadhari hiyo, Rutabanzibwa alijikuta akitumbukia katika mtego, kwani alisaini mkataba huo bila baraka za AG.


Kwa mujibu wa nyaraka zilizoshuhudiwa na mwandishi wa habari hizi, mkataba huo ulisainiwa Mei 29, 2009.


Upande wa Serikali liwakilishwa na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu na Omary Igge akiwa mmiliki wa GIVA iliyopewa zabuni hiyo.


Makao makuu ya kampuni hiyo yako Social Security House, Samora Avenue ghorofa ya saba, Dar es Salaam. Rutabanzibwa alipoulizwa kuhusu kusaini mkataba huo, alikiri kuhusika, lakini akasema hawezi kuzungumzia hilo kwa undani kwa kuwa sasa hafanyi kazi wizara hiyo.


Igge kwa upande wake, alikiri kampuni yake kupewa kazi ya kupitia mkataba huo, lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani pia akidai alifuata taratibu zinazotakiwa.


Kwa upande wake, Kamishna Nanyaro alikiri kuwa na uhusiano na GIVA, lakini akasema suala la kuipa zabuni si jukumu lake, hivyo hapaswi kuhusishwa na kashfa hiyo.


"Ni kweli nina uhusiano wa karibu na mmiliki wa kampuni hiyo, lakini nachouliza ni kwamba kama mzabuni ni rafiki yako, unaweza kuacha kumpa kazi eti kwa sababu ya urafiki!
Tunachoangalia hapa ni uwezo tu," alisema Nanyaro.

Hata hivyo, alishindwa kutoa maelezo ni kwa sababu gani mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kukamilisha kazi hiyo kutokana na sababu za kitaalamu.


Licha ya kuonesha udhaifu, kampuni hiyo imekuwa ikilipwa fedha kwa awamu ambapo Aprili 19 mwaka huu, kupitia vocha namba 70/4 ya hundi namba 995592 ililipwa Sh 410,884,850; Juni 24, mwaka huu kupitia vocha namba 1081/6 ya hundi namba 693977 ililipwa Sh 346,994,154.50.


Juni 25 mwaka huu, kupitia vocha namba 156/6 ya hundi namba 996681 ililipwa Sh 389,115,130 na Juni 27 mwaka huu, kupitia vocha namba 1679/6 hundi namba 694001 ililipwa Sh 453, 005, 845.50 na kufanya jumla ya fedha iliyochotwa na kampuni hiyo ndani ya muda mfupi kufikia Sh bilioni 1.6.


Taarifa zaidi zinasema kampuni hiyo inaendelea kupokea malipo mfululizo na gazeti hili litachapisha malipo hayo kila linapojiridhisha kuwa na vithibitisho vya kutosha.



My Take:
Je hii itakuwa kashfa ya kwanza kubwa ya awamu ya pili ya JK? Kwa kutolewa na gazeti la Serikali ina maana gani?


Guys, this might be something serious, similar to EPA, KWANI JUNE 27 MWAKA JUU ILIKUWA NI JUMAPILI!
 
CAG nenda kule haraka!
MAGEREZA KUNA MADUDU MENGI ZAIDI YA HAYO WANAYOSIKIA!! KAMA YAWEZEKANA AENDE MAGEREZA YA MIKOA YOTE AONE UTUMBO ULIOPO HUKO...KAMISHNA MKUU ANA MIRADI KILA MKOA, KILA MRADI ULIOPO KWENYE MKOA NAYE ANA SHARE YAKE
 
Lakini itakuwaje kuwa hii kashfa ni kashfa ya geresha kwani mambo yote tayari yana maelezo ya kutosha na kukubalika na haifiki mbali?
 
Yaani haya mambo ya TZ, kuna wakati huwa naona for the health of your heart inabidi kutoyafatilia kwa saana!

yaani mdau ur right yaani mm hapa nasoma hii habari huku nikiwak ktk ambulance naelekea hospitaliiii,yaani tz kila mtu anafikiria kula kabla mwingin hajala.....izo hela si bora wangezielekeza kwenye menu ya wafunga angalu wapate matunda na mboga mboga
 
unajua kila mmoja sasahivi anaona bora a-ccm (achukue chake mapema) maana wakubwa wanajichotea. tatizo jingine ni kwamba diola yetu haina nguvu, na wananchhi ndo kabisaaaaa wamechoka. maana nguvu ya wananchi ni muhimu kusukuma mambo yaende mbele ikiwa waliopewa dhambana hawawajibiki.
 
meaning walisainishiana sebuleni kwa mtu au bar.......
Kama walisainishana sebuleni nani kawaruhusu? Wanatembea na kitabu cha hundi kikiimbiwa au kikipotea???
Kweli ufisadi hauishi Tanzania
 
mustakabali wa taifa hili wanaujua wenyewe mafisadi
sisi tupo tupo tu tunatoa macho na wameshika mpini sasa we unafikiri tutafanyaje hapo

Natamani sana kumiliki high range telescopic rifle!!!
 
Back
Top Bottom