Kashfa ya Bil. 40Tshs Magereza: Matumizi ya Mkataba wa Mfumo wa Usajili wa Wafungwa

My Take:
Je hii itakuwa kashfa ya kwanza kubwa ya awamu ya pili ya JK? Kwa kutolewa na gazeti la Serikali ina maana gani?

Mkuu... Tumedandia IT na watoto wanatukimbiza kweli miaka hii, sijui serikali yetu imejiandaaje na cyber era
 
But why Rutabanzibwa tena? Hivi hii sheria ya manunuzi ya Umma ni siri au ngumu sana kiasi hicho kwamba ni vigumu mno kuizingatia? Lakini itakuwaje kama hizi ni kelele za wapinzani tena kwa kutumia gazeti la serikali?

Umenichekesha.

Wapinzani wanaweza piga kelele kwa kutumia Daily News kwani Kiingereza wanajua??

Ahh! No Kumbe ni la Kiswahili???

Hawa lazima ni wapinzani tu.
 
My Take:
Je hii itakuwa kashfa ya kwanza kubwa ya awamu ya pili ya JK? Kwa kutolewa na gazeti la Serikali ina maana gani?

Wanajaribu kutekeleza majukumu yao chini ya mazingira magumu wanayowekewa na CCM............

Ukweli ni kuwa CCM is a dying horse...........you do not flog a dying horse but you dig a trench for its eventual burial..............CCM inaingia madarakani kwa dhuluma ya kugeuza matokeo ya kura za uchaguzi na hiyo ni dhuluma wafikiri itakuwa mstari wa mbele kupambana na silaha iliyoiweka madarakani?

If you say yes think again...................................
 
But why Rutabanzibwa tena? Hivi hii sheria ya manunuzi ya Umma ni siri au ngumu sana kiasi hicho kwamba ni vigumu mno kuizingatia? Lakini itakuwaje kama hizi ni kelele za wapinzani tena kwa kutumia gazeti la serikali?

Ukishangaa ya Mussa utaona ya Firauni . . . . Ziko nyingi tu hizo ila waandishi wana access na facts kidogo tu . . . . the list can go on . . .

Immigration . . . .
Wizara ya Afya . . .
Ngorongoro . . .
TANAPA . . . . .
TAMISEMI . . .
.
.
.
System yetu ya uongozi inataka total overhaulling. Tatizo si sheria bali ni uongozi na uadilifu.

Sakata la Prisons halikuanzia kwa Nanyaro, lilianzia kwa Banzi kabla hajaondoka. Ni project kubwa ambayo hata UNDP walifund upande wa infrastructure na ikakamilika. I am talking in 2006 . . . sasa hivi 4 years later tuko pale pale.
 
Kwa kuwa gazeti la Habari Leo limetumika wakati wa uchaguzi naamini inaendelea kutumika.
Naona kama si haba kuweka habari hizi hadharani especially kipindi hiki.
Nakubaliana na Yetuwote
Ni kumzuia JK asimrudishe Masha, Kwani alikuwa na mpango huo.
.. or any other ulterior motive lakini si kufichua mafisadi kwani Habari Leo is part and parcel of this government na washirika wake....
 
Very sad. Hii ni dalili kwamba awamu hii nayo itatawaliwa na ufujaji wa pesa za walipa kodi.

Kuhusu habari hii kutolewa na HabariLeo, mimi naamini ni katika jitihada za kujitakasa. Gazeti hili na kakake Daily News yamevurunda mno wakati wa uchaguzi kwa kujigeuza kuwa vyombo vya kampeni za CCM. Sasa baada ya kampeni kwisha wanajaribu kurudi kwenye maisha ya kawaida na kujipatia uhalali mbele ya jamii. Hata hivyo safari yao ni ndefu kweli!
 
Ukishangaa ya Mussa utaona ya Firauni . . . . Ziko nyingi tu hizo ila waandishi wana access na facts kidogo tu . . . . the list can go on . . .

Immigration . . . .
Wizara ya Afya . . .
Ngorongoro . . .
TANAPA . . . . .
TAMISEMI . . .
.
.
.
System yetu ya uongozi inataka total overhaulling. Tatizo si sheria bali ni uongozi na uadilifu.

Sakata la Prisons halikuanzia kwa Nanyaro, lilianzia kwa Banzi kabla hajaondoka. Ni project kubwa ambayo hata UNDP walifund upande wa infrastructure na ikakamilika. I am talking in 2006 . . . sasa hivi 4 years later tuko pale pale.

TEMESA aka wazee wa Trafic light na vivuko nchini. Kunanuka balaa huko nako basi ngoja tuanze kufuatilia kwa nguvu zote.

 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, gazeti la Serikali linachapisha kashfa inayouhusu "uongozi wa juu" wa Serikali!

Hongereni sana HabariLeo! Lakini tusijesikia kwamba Mhariri Mtendaji anasimamishwa kazi kutokana na kadhia hii!

-> Mwana wa Haki

P.S. Najua walilazimishwa kuandika ile habari ya "uporaji mke" aliodaiwa kuufanya Slaa. Sasa uchaguzi umeisha, wanafanya kazi yao ya UANDISHI WA HABARI, si UCHAKACHUAJI WA HABARI!
 
Hawa jamaa ni kama panya wakiwa kwenye ghala la mahindi,
Ukiziba sehemu moja wanatoboa kwingine.
 
Ukiangalia AG alipoint dosari na akasema ziwekwe sawa, lakini waheshimiwa wakasaini bila kujali ina maana kuna wakubwa zaidi ya AG wanaoukingia kifua uchafu huo.Pia Rutabanzibwa nafikiri yuko kufanikisha maovu kumbuka IPTL,Richmond kote ana mikono.
 
Heri ya wachina ambao ukifanya kosa kama unapelekwa uwanja wa Taifa tena mpya kama huu wetu, unaita media and then mhusika will get hanged publicly.
 
That is alot of money!Hii inastahili kuingizwa Bungeni ikajadiliwe na kina Tundu Lissu na Kina Mwakyembe!!Aisee Nanyaro hana hata aibu,ama hajasoma maadili ya uongozi???
 
Mimi hii naiita ni sinema. Kila kitu kilipangwa na na kuchezwa kwa ajili ya audience ambao ni watanzania. Walijua fika itajagundulika so wanaamua wao kuiongoza waonekane as if ndio wameibua ufisadi.

Kama movie inavyokua they know where this will end ilhali wameshachota fedha zetu. Kama movie za kihindi zilivyo 'stelingi' hauwawi, atashinda tu. Director wa hii movie aliepanga mchezo huu ni system nzima, maana watu wawili au watatu hawawezi cheza movie.

Nashurutika kuamini hata CAG huwa anaparticipate tangu mwanzo wa kuandika hii sinema, what is unfolding now is part of the ongoing script. Kina Ruta hao ni waigizaji tu wanaoonekana kwenye screen. Movie hii haina tofauti yoyote na ile ya Richmond, EPA, IPTL, na Meremeta, nk. Mwisho wake bahati nzuri twaweza kuhisi itakuwaje.

Nia za hizi movie ni kupumbaza tuone wanaibua vitu na kuvifanyia kazi lakini hakuna kitu. Nina hakika kuna scripts nyingi tu zinaendelea kuandikwa na kueditiwa, fraud and more fraud, wakati wao wa screening utafika tu na the same yatatokea.
 
Inawezekana serikali imeona kashfa inakaribia mikono ya upinzani ikaona ni vema ijiwahi ili ionekae na yenyewe haipendi ufisadi maana kama mtakumbuka kwenye kampeni wapo wana ssm walisema kashfa ya richmond na EPA hazijaletwa na wapinzani
 
Albert Anschtein alisema hivi,
two things are infinite, the world and human stupidity
hii sasa nimeamini, pamoja na kuwa watu wamekazania kupambana na mikataba ya kijinga na kifisadi bado kuna wazalendo wa nchi hii wanaingia kichwakichwa? Tunahitaji dictator bongo ndo ataweza kutawala hii nchi au tuwakodi wachina waje kuiongoza bongo japo miezi michache ili wakichinja mafisadi watatu, wengine ndo watajifunza au wahame nchi!
 
Nipo kwenye mchakato wa kuikimbia Tanzania...! (Mkimbizi wa wizi). Manake kila kukicha naibiwa tu...! Haswa na Serikali yangu....!

Nimechoka kuibiwa...!
 
Back
Top Bottom