Kashfa ya Bil. 40Tshs Magereza: Matumizi ya Mkataba wa Mfumo wa Usajili wa Wafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya Bil. 40Tshs Magereza: Matumizi ya Mkataba wa Mfumo wa Usajili wa Wafungwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 14, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Habari Leo Novemba 13, 2010

  VIONGOZI wakuu wa Jeshi la Magereza nchini wanakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya Sh bilioni 40 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mfumo mpya wa kusajili wafungwa ujulikanao kama Offenders Management Information System (OMIS), kinyume na taratibu za sheria.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyanzo vya uhakika kutoka ndani na nje ya Jeshi hilo,
  kutokana na shinikizo la uongozi wa juu, Magereza ilijikuta ikiingia mkataba wa mradi huo kinyemela, kwani ulikataliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kutokana na kuwa na kasoro kubwa.

  Taarifa hiyo inaeleza, kwamba mkataba huo ulianza kutekelezwa kibabe mara tu Serikali ilipotoa fedha za utekelezaji wa mradi huo katika mwaka wa fedha wa 2006/07, baada ya Serikali kuridhishwa na andiko la mradi huo, ambalo lilikuwa limeeleza vizuri juu ya taratibu zilizopaswa kutumika, katika utekelezaji wa mradi huo.


  Andiko hilo lililoandaliwa na aliyepaswa kuwa Meneja Mradi, Abdallah Zawadi, liliombewa fedha kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo Novemba 27, 2006 Rais Jakaya Kikwete alitoa baraka za utekelezaji wa mradi huo.


  Vielelezo ambavyo gazeti hili limevishuhudia katika ofisi za makao makuu ya Jeshi hilo vinaonesha kuwa, Machi 13, 2008, Wizara ya Mambo ya Ndani ilimwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro, barua yenye kumbukumbu namba CAB. 48/468/01/89 ikimfahamisha kuwa ombi la utekelezaji wa mradi huo lilikubaliwa ili utekelezaji wa mradi huo uanze mara moja.


  Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Jeshi hilo kililiambia gazeti hili, kwamba baada ya barua hiyo kulikuwa na mazungumzo ya chini kwa chini kati ya Kamishna Nanyaro na
  Bodi ya Zabuni, ambapo baadaye walitoa zabuni kinyemela kwa Kampuni iitwayo GIVA Tanzania Limited kuwa ndiye mtekelezaji mkuu wa mradi huo.

  Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kwa kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kutekeleza mradi huo, pia Bodi hiyo ililazimika kupitisha kampuni za TIBURON INC ya Marekani na CMC Ltd ya India, kuwa washindi wengine wa zabuni hiyo, ili washirikiane na kampuni hiyo (GIVA) na kuruhusu mkataba uandaliwe.


  Moja ya nyaraka ambazo gazeti hili imezipitia zinaonesha kuwa kutokana na agizo hilo, kupitia barua yenye kumbukumbu namba P.2751/a/31, Makao Makuu ya Magereza ilimteua ACP Zawadi kuwa msimamizi wa mradi huo na kumtaka aandae mkataba na kumshauri Kamishna Mkuu wa Magereza, juu ya utekelezaji wa mradi huo naye akiwa Meneja Mkuu wa Mradi.


  Chanzo kinaeleza kwamba ACP Zawadi baada ya kupitia nyaraka za Kampuni ya GIVA hakuridhishwa na uwezo wa kampuni hiyo katika utekelezaji wa mradi huo, hivyo mara kadhaa alimshauri Kamishna Nanyaro kuachana na kampuni hiyo, jambo ambalo lilipingwa.


  Katika barua yake kwa Kamishna Mkuu wa Magereza yenye kumbukumbu namba PF 2010/Vol.1/2 ya Aprili 16, 2010 yenye kichwa cha habari: Ushauri na Usimamizi wa Mradi wa OMIS, ACP Zawadi alishauri kwamba mkataba huo ulipaswa kuandaliwa kwa kushirikisha watendaji wakuu wa mradi huo.


  Watendaji hao ni Jeshi la Magereza, wataalamu kutoka Kampuni ya TIBURON INC ya Marekani, wataalamu wa CMC ya India na wawakilishi kutoka GIVA Tanzania Ltd ili kuweka wazi udhaifu ambao ungejitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.


  Kwa mujibu wa barua hiyo, ACP Zawadi alionesha wazi kuwa GIVA licha ya kuwa ndiyo ilikuwa mzabuni mkuu, haikuwa na utaalamu juu ya kazi hiyo, lakini ilipewa zabuni ambayo iliitaka kushirikisha TIBURO INC ambayo imebobea katika teknolojia ya kuratibu shughuli

  za wafungwa, kupitia mitandao ya kompyuta na Kampuni ya CMC ambayo imebobea katika mfumo wa kompyuta wa kuchukua alama za vidole.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya ACP kuonekana ni kikwazo katika mradi huo kutokana na ushauri ambao haukumfurahisha Nanyaro, aliondolewa katika uandaaji wa mkataba na usimamizi wa mradi huo, hivyo Kamishna aliwakabidhi kazi hiyo maofisa wake wawili - DCP Minja na CP Mboya, kuandaa mkataba huo kwa siri na kupuuza ushauri wa ACP Zawadi, licha ya kwamba maofisa hao hawana utaalamu wa kutosha katika fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.


  CP Mboya alipoulizwa kuhusu jambo hilo alikiri kuhusika. Kwa upande mwingine DCP Minja hakupatikana kwa kuwa yuko masomoni nje ya nchi.


  Chanzo hicho kinaeleza kwamba baada ya maofisa hao kuandaa mkataba huo kwa kushirikiana na Nanyaro mwenyewe, waliupeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mei 23, 2008.


  Mkataba huo uliambatana na barua kumbukumbu namba HQC.80/PMIS/iv/26, iliyokuwa ikimshawishi AG kubariki mkataba huo.


  Hata hivyo, nyaraka ambazo gazeti hili limezipata kutoka ofisi ya AG zinaonesha kuwa alikataa kusaini mkataba huo.


  Kwa mfano, kupitia barua yake yenye kumbukumbu Na.JC/130/11/4 ya Juni ,2008 ambayo ilisainiwa na Pius Mboya, AG alikataa kusaini mkataba huo kwa kuwa ulikuwa na upungufu na kuagiza uandaliwe upya kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.


  "Tumepitia makubaliano yenu na wazabuni, lakini tumebaini upungufu kadhaa, hivyo si vizuri kusaini mkataba huo kabla ya kuufanyia marekebisho," ilisema barua hiyo.


  Barua hiyo inaeleza: "… barua yenu inaonesha kuwa zabuni ya mradi huo imetolewa kwa Kampuni ya GIVA Tanzania Ltd, wakati hati ya makubaliano inaonesha kuwa kuna kampuni nyingine mbili, hivyo muandae mkataba mpya utakaoshirikisha kampuni zote".


  Baada ya uongozi wa Magereza kukaa kimya, Mei 20, mwaka jana, AG alimwandikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati huo, Patrick Rutabanzibwa,
  barua yenye kumbukumbu Na.ACJC/a.130/11/1 ikimtaka kutosaini mkataba huo hadi utakapobarikiwa na ofisi yake, baada ya kurekebishwa Upungufu uliomo.

  Licha ya hadhari hiyo, Rutabanzibwa alijikuta akitumbukia katika mtego, kwani alisaini mkataba huo bila baraka za AG.


  Kwa mujibu wa nyaraka zilizoshuhudiwa na mwandishi wa habari hizi, mkataba huo ulisainiwa Mei 29, 2009.


  Upande wa Serikali liwakilishwa na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu na Omary Igge akiwa mmiliki wa GIVA iliyopewa zabuni hiyo.


  Makao makuu ya kampuni hiyo yako Social Security House, Samora Avenue ghorofa ya saba, Dar es Salaam. Rutabanzibwa alipoulizwa kuhusu kusaini mkataba huo, alikiri kuhusika, lakini akasema hawezi kuzungumzia hilo kwa undani kwa kuwa sasa hafanyi kazi wizara hiyo.


  Igge kwa upande wake, alikiri kampuni yake kupewa kazi ya kupitia mkataba huo, lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani pia akidai alifuata taratibu zinazotakiwa.


  Kwa upande wake, Kamishna Nanyaro alikiri kuwa na uhusiano na GIVA, lakini akasema suala la kuipa zabuni si jukumu lake, hivyo hapaswi kuhusishwa na kashfa hiyo.


  "Ni kweli nina uhusiano wa karibu na mmiliki wa kampuni hiyo, lakini nachouliza ni kwamba kama mzabuni ni rafiki yako, unaweza kuacha kumpa kazi eti kwa sababu ya urafiki!
  Tunachoangalia hapa ni uwezo tu," alisema Nanyaro.

  Hata hivyo, alishindwa kutoa maelezo ni kwa sababu gani mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kukamilisha kazi hiyo kutokana na sababu za kitaalamu.


  Licha ya kuonesha udhaifu, kampuni hiyo imekuwa ikilipwa fedha kwa awamu ambapo Aprili 19 mwaka huu, kupitia vocha namba 70/4 ya hundi namba 995592 ililipwa Sh 410,884,850; Juni 24, mwaka huu kupitia vocha namba 1081/6 ya hundi namba 693977 ililipwa Sh 346,994,154.50.


  Juni 25 mwaka huu, kupitia vocha namba 156/6 ya hundi namba 996681 ililipwa Sh 389,115,130 na Juni 27 mwaka huu, kupitia vocha namba 1679/6 hundi namba 694001 ililipwa Sh 453, 005, 845.50 na kufanya jumla ya fedha iliyochotwa na kampuni hiyo ndani ya muda mfupi kufikia Sh bilioni 1.6.


  Taarifa zaidi zinasema kampuni hiyo inaendelea kupokea malipo mfululizo na gazeti hili litachapisha malipo hayo kila linapojiridhisha kuwa na vithibitisho vya kutosha.  My Take:
  Je hii itakuwa kashfa ya kwanza kubwa ya awamu ya pili ya JK? Kwa kutolewa na gazeti la Serikali ina maana gani?
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ina maana kuna watu wamechoka na madudu
   
 3. Madago

  Madago Senior Member

  #3
  Nov 14, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nikiendelea kutafakari, hua naamini kabisa fedha za kampeni za CCM huwa zinapitia sana kwenye miradi ya wizarani hasa ya jeshi...
   
 4. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo ni wazi sheria ya Manunuzi imevunjwa, cha ajabu katibu alihamishiwa wizara nyingine ili akaibe na huko.
   
 5. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli...and this is just the beginning...miaka hii mitano tutaona uchafu mwingi tu!
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Acheni waanze kunyukana wao kwa wao ... vita vya panzi furaha ya kunguru. Maana sasa hata yule mama anayejifanya hajui maana ya neno fisadi watamuweka kwenye wakati mgumu asijue aegemee kundi lipi.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  There we go again!!!!!! Halafu tunasema elimu bure haiwezekani!
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hizo zitaliwa na nyingine zitatengwa tena ili ziliwe.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani haya mambo ya TZ, kuna wakati huwa naona for the health of your heart inabidi kutoyafatilia kwa saana!
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Source: Habari leo hili si ndiyo lile gazeti la propaganda za CCM za kumchafua Dr Slaa?, Naona wameanza propaganda za kuonesha kuwa Tanzania inakuza utawala bora.
   
 11. R

  Rugemeleza Verified User

  #11
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kashfa za magereza ni kubwa sana na kama lingemulikwa zaidi madudu mengi na ya kutisha yangefahamika. Hii ni kashfa ya ulaji tu ambayo wote waliohusika wanatakiwa si tu kushtakiwa bali pia kufilisiwa vyote walivyonavyo kwani wamefanya yote kinyume cha sheria. Kama kuna maagizo ya Mwanasheria Mkuu kwamba mkataba haukutakiwa kusainiwa na vilevile kama huyo Mkuu wa Magereza ana uhusiano wa karibu na hiyo kampuni ni wazi kuwa kuna mgongano wa maslahi hivyo kisheria alitakiwa asishiriki katika mchakato mzima. Kuhusu Rutabanzibwa huyo naye ni wazi kuwa amesaini mkataba kinyume cha maagizo ya Mwanasheria Mkuu na huyu alitajwa na Dr. Slaa na Lissu kuwa yumo katika orodha ya aibu. Jibu ni moja ni lazima ashtakiwe na kufilisiwa.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Fuatilia kwa makini but dont make it personal.
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu huu ni usanii tu. I can assure you kuwa hakuna lolote litakalofanyika, siku zitaendelea na watanzania wataendelewa kuibiwa na kuchekelea. Kama kashfa ilianza kutokea mwaka 2006 inakaendelea 07, 08 maana yake ni kwa imetoka hiyo.

  Serikali ina wakaguzi wa mahesabu, na ina wahasibu na watu wanaofanya kazi za kulinda mali za umma. Lazima wanafahamu kama walikuwa kimya basi wanajua ni kwanini walikuwa kimya.

  It will be the same as EPA, and life will go on.
   
 14. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huu ni mwanzo tu, bado zingine zitaibuliwa....watch. Utashangaa kusikia kuwa hizi zilienda kwa CCM kwa ajili ya kampeni yao.

  Huyo Rutabanzibwa ni mtu wa madudu tupu. Dr. Slaa alishawahi kumtaja kuwa naye ni mmoja wa mafisadi lakini utafanyaje wakati fisadi mwingine ndo karudi ikulu kwa ufisadi. Dawa ni kuchapana tu, ndiyo nimesema kuchapana ndipo watu watakuwa na adabu.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  But why Rutabanzibwa tena? Hivi hii sheria ya manunuzi ya Umma ni siri au ngumu sana kiasi hicho kwamba ni vigumu mno kuizingatia? Lakini itakuwaje kama hizi ni kelele za wapinzani tena kwa kutumia gazeti la serikali?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Nov 14, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mambo ya perception vs. reality.....
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kila wizara na idara ya serikali ina mradi au miradi inayohusiana na Information system. Chache zina deliver lakini nyingi mhhh. IT inatumiwa kuchota fedha

  CAG kama ana kitengo kizuri cha Information System Audit atagundua system nyingi kwenye idara za serikali si tu zimekiuka sheria za manunuzi bali pia hazina Quality ya Information system.
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji, Why Rutabanzibwa?? Jibu ni rahisi kabisa. Kwa kuwa he was one of them on IPTL and he is one of then kwenye hii scandal ya Magereza. Na ikifika wakati utasikia anagombea ubunge au anateuliwa mkuu wa mkoa or something like. So si kitu kipya and nothing is gonna happen to him, be sure of that.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naskia kuchoka ghafla
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana mkuu... cha maana ni CAG kuwezeshwa kwenye kila technical area, yaani mimi huwa nasoma ripoti zake kwenye mambo ya afya na maendeleo ya jamii na kujisikia furaha na huzuni kwa mpigo... kwani anajitahidi sana, lakini anamiss a few loopholes wanazotumia pros

  Tusubiri ya tanesco
   
Loading...