johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,840
- 141,763
Wafanyabiashara wa nyama za mafungu huko Vingunguti wamelalamikia kitendo cha Bodi ya nyama kukamata nyama zao na kuzipeleka kituo cha polisi Buguruni ambako badala ya kuiteketeza waligawana na kubakiza makongoro.
Akiongea katika eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam mh. Kumbilamoto alisema Bodi ya Nyama ilipaswa kuvuta subira kwani eneo la kuuzia nyama ujenzi wake bado haujakamilika.
Naye Kamanda wa polisi kituo cha Buguruni amekana askari wake kugawana nyama akisema haiingii akilini eti askari wagawane nyama iliyotakiwa kuteketezwa ambayo huenda ina kimeta.
Chanzo: ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
=====
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yalaani kitendo walichofanyiwa wafanyabiashara wa nyama Vingunguti.
Halmashaur ya Jiji la Dar es Salaam imelaani kitendo kilichofanywa na Bodi ya Nyama kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni kuvamia wafanyabiashara ya machinjio ya Vingunguti na kuchukua nyama zao kwa madai ya kutokidhi vigezo vya kisheria kwa Afya ya mlaji.
Akizungumza na wafanyabiashara wa machinjio hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana kwani hakuna kiongozi yoyote waliemshirikisha katika oparesheni hiyo.
Amesema kuwa, bodi ya nyama walivamia machinjio hayo na kusema uwongo katika vyombo vya habari kwa wafanyabiashara hao wamekaidi kwenda eneo maalum ambalo wametengewa na Halmashaur ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili kuuza biashara zao jambo ambalo si kweli kwani eneo lililotengwa bado halijakamilika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara wa Nyama na mazao yake, Joel Meshark amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana hata kidogo kwani waliondoka na nyama hizo kwa madai ya nyama hizo ni vibudu.
“Walikuja kuchukua nyama na kuondoka nazo kwenda nazo Polisi Buguruni na kudai wamekwenda kuziteketeza lakini hakuna ukweli wowote kwani walichoma makongoro na hakuna nyama yoyote iliyoonekana”amesema Meshark.
Naye Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Ruta amesema kuwa, Mbunge wa Jimbo hilo, amewataka wafanyabiashara hao kupitia mwanasheria wao wafike ofisi ya Mbunge kwa ajili ya taratibu ya kwenda kufungua kesi ili haki yao ipatikane.
Aidha amesema, amesekitishwa sana na kitendo hicho kwani lengo lao lilikua ni kuwachonganisha wananchi na Serikali yao, hivyo ofisi ya Mbunge haitalifumbia macho jambo hilo.
Jackson Matutu Miongoni mwa wafanyabiashara hao amesema kuwa, alipokonywa nyama yake na viongozi wa bodi kwa madai nyama yake haikua katika mazingira mazuri hivyo wakamtaka alipe faini shilling laki moja, lakini baada ya kulipa alifukuzwa nje kama jambazi na hakuna chochote alichokipata.
“Nyama yangu ilikua kwenye chombo nilifika pale kwa ajili ya kuipeleka sehemu inayohusika lakini Jeshi la Polisi Buguruni kwa kushirikiana na Bodi ya nyama waliichukua nyama yangu na kuondoka nayo, walidanya wameichoma Moto ila nimeshuhudia wakigawanyana pale Polisi”amesema Matutu.

Kamanda Mambosasa: Polisi hawakugawana nyama za wafanyabiashara bali ziliteketezwa na nyingine ilifukiwa ardhini, zilikuwa kilo 130 siyo 800!
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam mh Mambosasa amesema tume iliyoundwa kuchunguza sakata la nyama ya wafanyabiashara imegundua nyama yote iliteketezwa. Mambosasa amesema tume ilionyeshwa shimo kubwa ambamo minofu na mautumbo ilifukiwa na sehemu nyingine ambayo miguu na makongoro...
www.jamiiforums.com