Kashfa Polisi Tanzania: Baada ya Bangi sasa Silaha

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
9 Juni 2013

Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi 3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.

Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu saa 11:00 alfajiri.

Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri taratibu zingine za polisi.

Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo wahusika wa basi na nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na stendi, baadhi ya askari waliovaa kiraia walionekana maeneo hayo mapema.

Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka ndani ya polisi, Koplo huyo alikutwa na shehena hiyo karibu na kituo cha mabasi ya Kampuni ya Mohammed Trans, akijiandaa kuelekea Dar es Salaam ambako inasemekana wana wateja wao.
 
hizi kashfa zingine hawa jamaa wanajitakia, lakini utakuta kesi inapigwa pigwa kimtindo imesha kimya kimya...
 
Yule Askari aliyekamatwa anasafirisha bangi ameachiwa na wenzake akiwa chini ya ulinzi. Eti kawatoroka.
 
9 Juni 2013

Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi 3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.

Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu saa 11:00 alfajiri.

Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri taratibu zingine za polisi.

Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo wahusika wa basi na nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na stendi, baadhi ya askari waliovaa kiraia walionekana maeneo hayo mapema.

Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka ndani ya polisi, Koplo huyo alikutwa na shehena hiyo karibu na kituo cha mabasi ya Kampuni ya Mohammed Trans, akijiandaa kuelekea Dar es Salaam ambako inasemekana wana wateja wao.
Tumefika pabaya kwa kweli.

Inaonekana wana wateja wao wa kuaminika, ambao bila shaka ni majambazi.

Askari wa Usalama wa raia, kutumika kuwawezesha majambazi, kweli tuna hali mbaya.
 
Dah. Afadhali maana kuna ndugu zetu walikuwa wanaenda kuporwa mali na kuuwawa kwa hizo silaha.
Sasa hivi kila mtu anatafuta njia ya mkato ya kupata fedha.
 
Je? Utasema wanafanya peke yao hao !
Lazima ni mtandao mkubwa sana RPC,OCD
yaani limeoza geshi la polisi,wanawateja wao.

Wakiitwa kwenye tukio la uharifu masaa 5
ndiyo wanakuja kumbe wateja wao wanafanya
kazi. Nadhani siku hizi ukitaka kuiba unakwenda
polisi halafu unalipia huduma kabisa.
 
Haya matukio tunayatafsiri vibaya, ingekuwa raia ndio tumewakamata hawa askari hapo sawa ingebidi tusiwe na imani na idara hii hata kidogo. Lakini tuelewe askari mmoja mmoja ni binadamu kama mwanadamu mwingine anayeongozwa kwa tamaa ya utajiri wa haraka haraka. Kwahiyo kama mmoja wao amejiingiza kwenye hizi tamaa na wao wenyewe yaani idara husika imeng'amua hilo na kumchukulia hatua inabidi tuwapongezeeeeee.

Nijuavyo mimi kila idara hapa kwetu tanzania inawatu ambao sio waadilifu lakini sijawahi sikia idara imetangaza kuwakamata watumishi wake kwa kukosa uadilifu kwa njia yoyote ile.

Labda ushauri wangu kwa idara ya polisi ni kwamba waache kutangaza kila kitu chao bila kupima athari ya hicho kitu kwa jamii. Najua kwamba jinsi kamanda wa polisi anavyoonekana kwenye vyombo vya habari ndio nafasi yake ya kupewa shavu inaongezeka kwa tafsiri ya kwamba anafanya kazi zaidi lakini kwa hili mnaharibu picha ya taasisi hii kwa ujumla.
 
Polisi wetu wamegeuka wezi na majambazi kuwazidi wezi na majambazi wenyewe.
 
Je? Utasema wanafanya peke yao hao !
Lazima ni mtandao mkubwa sana RPC,OCD
yaani limeoza geshi la polisi,wanawateja wao.

Wakiitwa kwenye tukio la uharifu masaa 5
ndiyo wanakuja kumbe wateja wao wanafanya
kazi. Nadhani siku hizi ukitaka kuiba unakwenda
polisi halafu unalipia huduma kabisa.

Hapo usikurupuke bwana keneth....Suala la polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa sio nia wala sio makusudi.....Askar wapo kwenye shughul mbali mbali likitokea tukio mpaka uwakusanye itachukua mda kidogo...hata kama uwezo wako ni Mdogo wa kufikiri ili nalo Umeshndwa kulitambua.
 
Haya matukio tunayatafsiri vibaya, ingekuwa raia ndio tumewakamata hawa askari hapo sawa ingebidi tusiwe na imani na idara hii hata kidogo. Lakini tuelewe askari mmoja mmoja ni binadamu kama mwanadamu mwingine anayeongozwa kwa tamaa ya utajiri wa haraka haraka. Kwahiyo kama mmoja wao amejiingiza kwenye hizi tamaa na wao wenyewe yaani idara husika imeng'amua hilo na kumchukulia hatua inabidi tuwapongezeeeeee.

Nijuavyo mimi kila idara hapa kwetu tanzania inawatu ambao sio waadilifu lakini sijawahi sikia idara imetangaza kuwakamata watumishi wake kwa kukosa uadilifu kwa njia yoyote ile.

Labda ushauri wangu kwa idara ya polisi ni kwamba waache kutangaza kila kitu chao bila kupima athari ya hicho kitu kwa jamii. Najua kwamba jinsi kamanda wa polisi anavyoonekana kwenye vyombo vya habari ndio nafasi yake ya kupewa shavu inaongezeka kwa tafsiri ya kwamba anafanya kazi zaidi lakini kwa hili mnaharibu picha ya taasisi hii kwa ujumla.

upo sahihi sana mkuu! wengine lawama tu, hawataki kufikirisha akili zao. Police nao watu na wanazo tamaa za kimaisha kama ilivyo wale tunaowaita mafisadi chamuhimu walokamatwa wafukuzwe kazi na waburuzwe mahakamani kwakua kazi ya ulinzi hawaiwezi tena!
 
Back
Top Bottom