Mwanakijiji
Zitto, hili suala la binafsi kama utalizungumzia utalizungumzia on your own personal terms siyo kwa kufurahisha JF au watu wachache wanaotaka kuridhisha udadisi wao tu. NI kweli jambo hili lilivuta hisia za watu wengi na mambo ya kitaifa n.k. Kama tulivyosema awali kama CCM na wahusika upande huo hawataki kuzungumzia kwanini tukulazimishe wewe ulizungumzie ilimradi tu tujue "nini kilitokea".
Mwanakijiji
Zitto akiamua kuzungumzia sasa hivi sina tatizo ni uamuzi wake, akitaka kuzungumzia mwezi ujao sawa sina tatizo, akigoma kulizungumzia kabisa sina tatizo...ni uamuzi wake! kati ya vitu vilivyoko mawazoni mwangu suala la Amina na Zitto liko mbali kweli!
Mwanakijiji unadai mimi nimevunja principle ya utetezi wa mambo binafsi, si kweli, ninachotetea hapa ni upotoshaji na ushabiki unaouleta kupitia mgongo wa marehemu, wahusika wanasema hakuna mkono wa mtu kwenye msiba ule wewe na genge lako mnang'ang'ania Nchimbi anahusika. Hicho ndicho ninachokipinga inavyoonyesha una ajenda yako ya siri. Kule kwenye marurupu umekuwa ukidai forcefully kuwa hakuna majibu atakayotoa Zitto yatatosheleza bila ya kuongeza maswali mengine, well sasa huku familia ishatupa majibu na inavyoelekea hakutakuwa na majibu yatakayo kutosheleza!
Mwanakijiji
Nilishasema tangu mwanzo hakuna jibu litakaloridhisha na hakuna swali litakaloachwa kuulizwa! Mmemuuliza Zitto kawajibu. Haitoshi. Mmeyaleta ya mama yake haitoshi. Hamuwezi kukubali jibu lolote isipokuwa "ndiyo mimi na Amina tulikuwa na uhusiano wa kimapenzi na ulikuwa mzuri kweli". Akijibu hivyo haina maana itakuwa mwisho maswali yatakuja "kwanini uvunje ndoa ya watu, wewe kama kiongozi.. tukuamini vipi na wake zetu? vipi mabinti zetu na dada zetu, unawezaje kukaa Bungeni ilhali hivi na vile".
Well, yaonyesha pia hakutakuwa na majibu ya kukutosholeza Mwanakijiji
Umedai umeandika makala ya kumtetea Nchimbi itatoka J3. Hiki ni kiroja kingine wakati huo huo unadai kuna mkono wa Nchimbi kwenye ugonjwa wa Kayombo.
Ukazidi kumsakamaKLH News! Kayombo apelekwa India kwa Matibabu!
Bila ya shaka wote mmesikia kuwa Mbunge wa CCM na Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji alikuwa amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Habari ambazo zimenifikia ni kuwa Mheshimiwa huyo amesafirishwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi. Bw. Kayombo kwa wale wanaokumbuka alipata nafasi ya kuzungumza nami kuhusu kukataa kwa serikali kuleta mikataba Bungeni. Katika uchaguzi ujao wa NEC Bw. Kayombo anagombea kuingia NEC kupitia mkoa wa Ruvuma. Nafasi hiyo ya NEC inagombewa pia na Naibu Waziri wa Michezo na Utamaduni Bw. Emmanuel Nchimbi.
Mwanakijiji
Mbunge mmoja kijana wa CCM aliyekuwa uwanja wa ndege kumsindikiza Marehemu alisikika akizungumzia taarifa za kupelekwa Kayombo India akisema "heri yangu mimi sigombei UNEC wowote".Mwanakijiji
Mtanzania, ningekuwa sijatenda haki kama nisingejaribu kuonesha huo uhusiano hasa wakati CCM inaelekea kwenye uchaguzi.
Unadai utakuwa hujatenda "haki" yaani kumzushia mtu ni kutenda haki!
Ninachotaka kusisitiza hapa sio kufunga mjadala wa Amina bali ni kuheshimu maamuzi wa wana familia. Inaelekea wewe Mwanakijiji ndio una uchungu sana na Amina kuliko baba yake sio? Kwanini hutaki kuheshimu maamuzi ya wanandugu?
Mwanakijiji unataka kuburuza watu wote tuamini kuwa kifo cha Amina kuna mkono wa mtu, sorry hilo wengine hatukubaliani nalo.
mie nilimshangaa huyu mwanakijiji kujidai anamjua sana AMINA halafu information ndogo kama dhehebu la AMINA alikuwa hajui.
Nyani, familia ya yule kijana aliyepigwa risasi na Dito ilisema ni mapenzi ya Mungu... kwanini Dito na kesi ya kujibu?
Katika misingi tuliyokulia ya utaifa hapa Tanzania, huwa hatutafuti details za madhehebu, makabila au koo za watu. Kwa hiyo kumjua mtu siyo lazima ujue dhehebu lake, unaweza ukajua kuwa ni mkristo au ni mwislamu lakini usijue zaidi ya hapo. Vile vile unaweza kujua kuwa anatoka mkoa wa Mbeya lakini usijue details zaidi ya hapo.
I give up... haya "mapenzi ya Mungu" yatatuletea matatizo kweli. Ni bora watu wote wanakufa kuanzia sasa TAnzania wazazi waliofiwa waseme ni "mapenzi ya Mungu" polisi wasichunguze, watu wasiulize, tuzike na yaishe!
Duh...ebwana eeh!!! unasema kweli walisema kijana wao kutwangwa risasi at point blank range ni mapenzi ya mungu? Ni nani aliyetoa kauli hiyo...? Kwa kweli hiyo sikumbuki...
Lakini hata kama walisema hivyo...sidhani kama walimaanisha Ditto asichukuliwe hatua...kwa sababu tendo alilofanya Ditto kwa kweli halina ubishi wowote.
Ukisema hivyo utakuwa umekasirika mkuu...
__________________Mwanakijiji
Naomba nirudie kusema kuwa sisemi kuwa Amina amekufa kutokana na njama za watu fulani, nasema kuna minong'ono na tetesi nyingi mtaani ambazo hadi majina ya watu yanatajwa. Hili si haki kwa mtu yule atajwaye na pia kutokuyapa uzito unaostahili hasa pale kiongozi wa kitaifa anapokufa katika usiri na utata, ni kuchochea minong'ono hiyo.