Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.

Mugongo Mugongo

JF-Expert Member
Nov 8, 2006
223
8
5s-amina.jpg



Jana gazeti la Majira limeripoti kwamba Bwana Mohammed Mpakanjia, mkazi wa Dar es Salaam, amemuandikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh. Samuel Sitta, kumuarifu kwamba amemtaliki mkewe, Mhe. Amina Mpakanjia, kwasababu ya kufanya mapenzi nje ya ndoa (ugoni) na Mhe. Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Katika barua hiyo, ambayo imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Mpakanjia amemuomba Spika Sitta amuonye Mhe. Kabwe kwa kitendo chake hicho.

Gazeti la leo la Tanzania Daima linaripoti kwamba Mhe. Amina Chifupa atafanya mkutano na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo kufafanua hili jambo ingawa amethibitisha kwamba ni kweli mumewe amemtaliki toka tarehe 3 Mei mwaka huu. Hata hivyo, Mhe. Chifupa na Mhe. Kabwe wote wanadai hizi ni njama za wana-CCM. Mhe. Kabwe anadai yeye ana uhusiano mzuri wa "kikazi" na Amina Chifupa na kwamba anamheshimu kama "mtu makini". These are his quotes.

Sasa, Sitta atachukua hatua gani? Je, atalipeleka kwenye Kamati ya Maadili kama ambavyo alipekela malalamiko ya Bwana Mengi? Makamba atachukua hatua gani? Je, the Zitto myth ndio inaanza kuporomoka? Je, kama ukila uroda mke wa mtu na ukakamatwa una haki ya kusingizia ni njama za maadui wako wa kisiasa? Je, maadui zako wa kisiasa wakiona udhaifu wako ni kupenda uroda (hasa kwa wake za watu), je wanaruhusiwa kuu-expose? Some of these are hypothetical questions.
 
Mmmmhhhh!!!! hii khabari nzito!

Mh.Zitto ni mdau wa JF, aje hapa afafanue labda story yake itakuwa tofauti kidogo.
 
wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu wa ccm,tayari kampeni za "kimtandao" zimeanza baada ya bibie amina chifupa kudaiwa kutaka kugombea uenyekiti wa vijana taifa...lile zimwi la kampeni chafu chafua lililoanza kwa muungwana kinaendelea ,baada ya dr nchimbi kudaiwa kumpakazia amina hafai kwa "kuwapa" CHADEMA...Hii imepelekea amina kulimwa talaka...hili sakata si udaku ila ndio siasa..tutege sikio ..zaidi angalia tanzania daima la leo 7/5/07 hapa:-

www.freemedia.co.tz
Naona leo kidogo tatizo kupata electronic copy ya tanzania daima la leo online...lakini zaidi amina amedhibitisha kukutana na waandishi wa habari maelezo ,kuelezea namna ,naibu waziri na mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu,alivyompa nyeti mumewe na kupelekea amina kulimwa talaka na mumewe....


Amina Chifupa kulipua bomu leo
na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), amesema leo analipua bomu mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuvunjika ndoa yake na Mohamed Mpakanjia, tukio analosema limesababishwa na kiongozi mmoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Naibu Waziri.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Amina, alisema anamuomba Mwenyezi Mungu amuamshe salama, ili aweze kuzungumzia suala hilo ambalo anafahamu kuwa linaweza kumuweka katika wakati mgumu kabisa.

“Nafahamu ninapambana na watu hatari, lakini kesho (leo) namuomba Mwenyezi Mungu aniamshe salama, ili niweze kuliweka bayana suala hili mbele ya waandishi wa habari MAELEZO. Nimekusudia kusema ukweli wote kuhusu suala langu,” alisema Amina.

“Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu… hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa ‘ndiyo mzee’,” alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.

Amina ambaye ameihakikishia Tanzania Daima kuwa alipewa talaka na mumewe, Mei 3 mwaka huu, anasema tukio hilo lilikuja baada ya kiongozi huyo wa CCM ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho kumuita mumewe ofisini kwake.

“Nilipewa talaka siku ile ile baada ya Mpakanjia kutoka ofisini kwa kiongozi huyo. Kwa kweli (anamtaja) ndiye aliyevunja ndoa yangu kwa kumuambia mume wangu mambo ya uongo,” alisema.

Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kwamba, Amina anaamini kwamba kikubwa kilichosababisha akutwe na masahibu hayo, ni kile kinachoelezwa kuwa uamuzi wake wa kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), hatua ambayo inaonekana kuwashtua na kuwakera baadhi ya viongozi wa sasa wa umoja huo.

Hivi sasa Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana anayetarajiwa kumaliza kipindi chake mwakani.

Hata hivyo, Amina alipotakiwa kueleza iwapo alikuwa akikusudia kugombea nafasi hiyo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kumtaka mwandishi kusubiri hadi wakati utakapofika kwani kuna muda mrefu bado, kabla ya yeye kufikia uamuzi huo.

Mbali ya hilo, Amina alielezwa kushangazwa kwake kuona masuala yake ya ndoa, yakipelekwa bungeni, wakati mahusiano yake ya nyumbani hayana uhusiano wowote na ubunge wake au uanasiasa wake.

Habari ambazo zilithibitishwa zinaonyesha kuwa, Amina amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbunge kijana wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambaye alipopigiwa simu na gazeti hili jana, aliyapuuza madai hayo ambayo alisema; “hayana ukweli.”


Zitto mmoja wa wabunge machachari wa upinzani, alisema anafahamu kwamba suala hilo limeandaliwa na kundi la watu wenye sababu za kisiasa, ambao wamekuwa wakimtafuta yeye na Chifupa kwa muda mrefu.

“Ukaribu wangu na Amina ni wa kikazi tu… na ukaribu huo ulianza siku Spika wa Bunge alipotuteua tuhesabu kura za wabunge zilizomuidhinisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Siku hiyo tulipokuwa tukihesabu kura, afisa mmoja wa bunge alitufuata katika chumba cha kuhesabu kura na akatutaka kutozitaja kura mbili zilizokuwa zimeharibika, jambo ambalo mimi na Amina tulilikataa. Tangu hapo nilianza kumheshimu Chifupa baada ya kubaini kuwa alikuwa mtu makini na mwenye msimamo. Tangu wakati huo tumekuwa na uhusiano wa karibu kikazi,” alisema Zitto, alipohojiwa kwa njia ya simu.

Alisema, siku zote amekuwa na uhusiano mzuri na wabunge wote vijana kwa wazee, lakini anashangazwa na uvumi juu ya uhusiano wake na Amina kuonekana vinginevyo.

Gazeti moja la kila siku, (si Tanzania Daima), jana lilimkariri Mpakanjia, akithibitisha kumtaliki mkewe baada ya kubaini ndoa yake ikiingiliwa na mbunge wa CHADEMA ambaye hata hivyo hakumtaja.

Habari zaidi ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kwamba, ushahidi mkubwa unaoonekana kuwaunganisha kimapenzi wabunge hao vijana, ni tukio la siku moja jioni, ambalo Amina alionekana akiwa amevaa koti la Zitto, wakiwa wameketi pamoja katika Hoteli ya Dodoma.


 
Kabla ya kujikita katika ushabiki ni vyema kwanza tukajiuliza maswali kadhaa;

1. Mzee Mpakanjia ana ushahidi gani kuthibitisha madai yake?

2. Je masuala ya kulana "uroda" ambayo kwa kiasi kikubwa hufanywa kwa usiri Spika ana mamlaka ya aina gani nayo?

3. Kwa nini Mzee Mpakanjia asilipeleka suala hili kwa wazazi wa Bi Amina, kwani alipopeleka posa alipeleka kwa Spika?

Kama ushahidi ni "tetesi" mbona tumezisikia "tetesi" nyingi tu kuhusiana na Bi Amina sina haja ya kutaja majina kwani huwa mara nyingi sipendi kufanyia kazi udaku lakini nina majina ya wabunge wasiopungua 10 ambao naambiwa Bi Amina ameshawahudimia.

In that case where do we draw a line between private matters na public one?
 
mugongo hongera kwa kubandika hii...utagundua kuwa namimi nimeirusha nadhani iunganishwe tu..huko nyuma tumemuongelea sana amina ..kiasi watu walifikia kumfananisha amina na mbowe...now true colours of amina ndizo hizi...kama tumeamua kumapa uongozi mkiangalia personel life yake mtamfukuza na hata huyo nchimbi karopoka kwa sababu kijana wa kigoma naye kapata ,ukizingatia ni mpinzani..mbona wengine waliopita hajawataja!!!!
au kwa ajili amesikia anautaka uenyekiti wa UV...au kwa sababu walipita wengine ni ccm...aache ubaguzi wa mapenzi..mbona huyo nchimbi alirushiwaga kashfa ya kumtaka yule mwandishi wa habari wa "uhuru"

zitto baab kubwa,!!!! kama mtu kaleta mpira mwenyewe na kipa kashatoka kwa nini usipige goli?? mradi uwe na viatu imara...!!!~
 
Hii Habari nzito
Kwa nyepesi nyepesi za haraka kuna watu wanadai bibie hakuwa na hiana tangu akiwa shule.
Maswali ya kujiuliza Mpakanjia alijua lini na why now?
 
Philemon

Sikubaliana na wewe katika hili. Kilichopo ni madai ambayo hayajathibitika. kutumia madai hayo na kufafanisha na thread ya Ac V Mbowe si sahihi kwa maana hata huko tuliona madai mengi tu kuhusiana na Mbowe na ni yenye kutia kinyaa hasa. Suala hapa je kuna ukweli?

Umekwenda mbali kumpongeza Mh Zitto kwa yaliyotokea kama ni kweli kafanya hivyo amepotoka na sidhani kama utakuwa unamsaidia kwa kumsifia kwa mmomonyoko huu wa maadili ya uongozi
 
Kama kweli mh. Zitto kale uroda wa huyu bibie, it is a big shame to himself and to my party. Nampa pole na kumtakia uponyaji wa haraka ili asimame tuendelee kukijenga chama chetu. Sio kwamba kula uroda ni kitu kibaya; kibaya hapa ni kula uroda wa mke wa mtu. Mbaya zaidi mke mwenyewe ni Amina Chifupa ambaye maadili yake ni questionable for ages.

Ukishakuwa mwanasiasa unayeng'ara lazima uwe makini sana. Ujue kuna watu watafurahia mafanikio yako na kuna wengine hawatafurahia tu bali pia watakuchukia na kufanya kila hila ili kukumaliza kisiasa. Hii ni hasa katika nchi kama za kwetu ambazo bado zimekaa kikomunisti komunisti. Sasa Zitto hata kama kweli hajamla uroda huyu binti alipaswa kujua kuwa kuwa naye karibu kiurafiki ingempeleka pabaya. Ni rahisi wote wawili kukanusha, lakini the damage has been done and it should have been possible to prevent it.

Sasa kinachotakiwa hapa kama kweli kosa hili limetokea ni Zitto kukiri na kuomba msamaha kwa Bwana Mpakanjia, kwa mke wake na kwa CHADEMA. Then asimame tuendelee na mapambano. Hakuna njia nyingine ya uponyaji hapa zaidi ya yeye kukiri na kuomba msamaha hadharani!

Zitto amekuwa mtu wa madili kwa muda mrefu sana. Nitasikitika kama kweli atakuwa amefikia hatua ya kuporomoka kimaadili kwa muda mfupi namna hii tangu awe mbunge.

Nasubiri kusikia kwake.
 
Yeah Nyeupe Iitwe Nyeupe Na Nyeusi Iitwe Nyeusi, Kwanza Tusubiri Uthibitisho Halafu Tujue Wapi Pa Kusimama, Lakini Kama Limetokea Wote Wawili Wameaibisha Bunge, Na Waejiaibisha Wenyewe.

Hii Sasa Itawafanya Wenye Wake Wabunge Wawe Na Khofu, Pia Wale Ambao Wake Zao Watataka Wagombee Watakuwa Na Hali Ngumu Kulikubali Hilo.

Tusubiiri Ushahidi, Bwana Zittto Tunakuomba Uje Utueleze Ni Kipi Kilichojiri
 
Kama Hii Breaking Newss Unaapaswa Uiache Kwanza Maana Inatest Tofauti Sasa Ukiichanganya Unaiondoa Test
 
Mtumwitu,
Nakubaliana na maadili yako. Lakini mbona ile picha yako si ya mwitu? (ha!ha!ha)
 
jamboonormal_amina5.jpg


TAZAMA TAJIRI MTOTO ANAVYOMPIGA JICHO "mama shughuli" ILI HALI MUMEWE ANACHEKELEA TUUU

jamboonormal_amina6.jpg

sasa hiyo TV watagawana vipi?
 
Hivi watu wakipendana kuna shida gani? Huyu mumewe yeye hatembei nje? Hapa wameshikana na wametalakiana haya ya kumwandikia spika ni katika kufanya nini hasa wakati wameisha peana talaka.

Absolutely stupid?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom