Kashfa nzito Polisi

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,413
8,684
Kashfa nzito polisi

Tanzania Daima
na Hellen Ngoromera

JESHI la Polisi kwa mara nyingine limeingia katika kashfa mpya baada ya askari wake kadhaa wa kituo kimoja cha polisi wilayani Kilombero kutuhumiwa kuendesha operesheni maalumu ya mateso makali yaliyosababisha kifo cha mtuhumiwa mmoja.
Ripoti ya siri ya uchunguzi dhidi ya polisi walioendesha mateso hayo miezi mitatu iliyopita katika eneo maalumu walilolipachika jina la ‘Kalvari’ wakilifananisha na mahali aliposulubiwa hadi kufa, mtu anayeaminika kuwa mkombozi wa Wakristo duniani, Yesu Kristo, imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete Ijumaa iliyopita.

Mbali ya Kikwete, nakala za ripoti hiyo ya uchunguzi iliyoandaliwa na mchunguzi binafsi, zimewasilishwa pia kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Tume ya Haki za Binadamu siku hiyo hiyo ya Ijumaa.

Uchunguzi kuhusu mauaji hayo ulifanywa na mtaalamu huyo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchunguzi, utaalamu alioupata kupitia Jeshi la Polisi alilolitumikia kwa miaka 12 akifanya kazi katika Kitengo cha Uchunguzi wa Uhalifu wa Nyaraka (Fraud Department).

Mtaalamu huyo, John Robert Mswanyama, wa Kampuni ya JRM Monitoring Agency (T) LTD alifanya kazi hiyo iliyomwezesha kuwahoji watu 12 ambao maelezo yao yameambatanishwa katika ripoti yake ya maandishi yenye kurasa 83 kwa maelekezo ya familia ya marehemu, Seif Ramadhan Mambosasa, ya Mang’ula, mkoani Morogoro, anayeaminika kuuawa na polisi hao.

Katika ripoti yake hiyo ambayo imeambatanishwa picha nne za marehemu Ramadhan, wanafamilia wake wanamuomba Rais Kikwete aunde tume huru kuchunguza mauaji ya ndugu yao huyo ambaye wanadai alifariki kutokana na kipigo alichopewa na askari polisi hao.

Aidha, ripoti hiyo, inaeelezea mwenendo wa tukio zima, tangu kijana huyo na wenzake walipokamatwa kwa tuhuma za wizi wa simu ya kiganjani na redio, na jinsi alivyofikishwa kituo cha polisi na mambo yote yanayodaiwa kutokea hadi kifo chake, yakiwemo mateso waliyoyapata watuhumiwa hao pamoja na marehemu.

“Mheshimiwa Rais, ukweli hasa wa tuhuma hizi utajulikana pale tu hatua za haraka za kuunda tume huru ya uchunguzi wa jambo hili kwa undani zaidi, kwani tume itakuwa na nguvu ya kuwahoji wahusika, yaani polisi waliohusika, pia wale raia watatu na wengineo, kwani hakuna shaka juu ya kifo cha marehemu Seif kuwa kilisababishwa na mateso aliyoyapata,” inaeleza barua kwa rais iliyoambatanishwa na kuwa sehemu ya ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ya kwanza ya aina yake hapa nchini ambayo Tanzania Daima imeiona nakala yake, inaeleza kuwa, Seif alifariki dunia baada ya kukamatwa na watu wengine sita, wakituhumiwa kuiba mali za mkazi wa huko Kilombero, Abdallah Mohamed Dube.

Akizungumza na gazeti hili, Mswanyama, alisema katika utafiti wake alioufanya kwa mwezi mmoja kuhusiana na suala hilo, amebaini kuwa watuhumiwa hao (akiwemo marehemu), walipewa mateso na askari polisi wa Kituo cha Ruhembe, wakiongozwa na Mkuu wa Kituo hicho (OCS).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mswanyama, Seif alifariki Julai 18 mwaka huu katika Hospitali ya K.I. inayomilikiwa na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na akazikwa siku mbili baadaye baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, Ifakara.

Pamoja na Seif, wengine wanaodaiwa kuhusika na tuhuma hizo ambao pia wamehojiwa na Mswanyama ni Jafari Kilinda, Abdallah Likana, Mohamed Akile, Khasimu Mgonigani na Francis Mselemu.

Sambamba na wengine waliohojiwa na mtafiti huyo kama mashahidi ni Paulina Shao (mke wa marehemu Seif), Hamisi Mbiji, Salehe Semboko ambaye ni Mwenyekiti wa serikali ya Kitongoji cha Mkula ‘B’, Sharifa Mambosasa (au Kulwa ambaye ni pacha wa marehemu Seif), Hamis Mpoka na Juma Mambosasa (kaka wa marehemu).

Kwa mujibu wa maelezo ya watuhumiwa hao, walipofikishwa kituoni waliteremshwa katika gari na baada ya OCS kupewa taarifa zao, aliwaamuru askari kupeleka vifaa vya kufanyia mateso ambavyo ni shoka, mpini wa chuma, nondo vitambaa vyekundu na baadaye watuhumiwa waliingizwa katika chumba kimoja na kuanza kuteswa.

Katika chumba hicho inadaiwa kuwa OCS huyo ndiye alikuwa msimamizi wa kazi hiyo.

“Watuhumiwa walifungwa vitambaa usoni na pingu kinamna kwa kupitisha mikono yao chini ya miguu na baadaye kuwanyanyua na kuwaning’iniza kwenye meza ambayo askari walipaita ‘Calvary’ waliwatesa kwa dakika kati ya 45 hadi 60 wakishirikiana na raia,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadaye ilipofika saa 6:30 mchana, OCS aliamuru wateremshwe na kupelekwa mahabusu lakini kutokana na mateso, walishindwa kusimama vizuri na askari waliwapeleka mahabusu kwa kuwaburuza.

Wakizungumzia mateso ya marehemu Seif, watuhumiwa hao walidai kwa kuwa awali aliteswa sana hadi kushindwa kutembea, kwa mara nyingine alichukuliwa na polisi na kutakiwa afungwe pingu kisha kupandishwa ‘Calvary’ lakini alikataa kufanya hivyo na kuwaambia askari hatafungwa tena pingu na kuwa labda wamuue.

“Ndipo askari (anamtaja jina) alipochukua kipande cha ubao na kumpiga kwenye shingo kwa nyuma (kisogoni) na ndipo Seif akaanguka chini na akaonyesha kama mtu aliyepoteza fahamu… askari walichukua pingu na kumfunga kisha kumpandisha ‘Calvary’ na kumpiga kwa hasira kwa zamu huku OCS akisema kama hawatasema kata vichwa vyao,” inaeleza ripoti hiyo.

Ripoti ya mtaalamu huyo ambayo imekuja siku chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari kuhusu tukio hilo kutokana na taarifa zilitolewa na mmoja wa ndugu wa marehemu, Frederick Lyasato, inawataja raia watatu ambao walishirikiana na polisi katika mateso hayo.

Lyasato aliieleza Tanzania Daima kuwa, siku ya tukio jamaa yake, Erasto Mahita (20), pamoja na Francis Mselem (18), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mgudeni, wote wakazi wa Mkula, walikuwa dukani ambako Mahita anafanyia kazi.

Kwa mujibu wa Lyasato, muda mfupi baadaye, polisi wa Kituo cha K2 wakiwa na gari lao walifika eneo hilo na kuwakamata watu hao.

Lyasato aliieleza Tanzania Daima kuwa, wakati tukio hilo linatokea, wananchi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkula aliyetajwa kwa jina moja la Semboko, walifika katika eneo hilo na kuhoji sababu za watu hao kukamatwa lakini polisi hao waliwatishia kwa bunduki zao.

Aliongeza kuwa wakati polisi na watuhumiwa hao wakiwa njiani kuelekea kituoni, walifika eneo lenye kichaka ambapo mtu anayedaiwa kuibiwa vitu hivyo, Mohamed Dube, ambaye pia alikuwa ndani ya gari aliwataka polisi kuwaua na kuwatupa vichakani watuhumiwa hao, ikiwa watakataa kuhusika na tuhuma hizo.

“Kwa kuwa washitakiwa walikuwa wakihojiwa ndani ya gari kuhusiana na tuhuma hizo na wao kukataa kuhusika nazo, yule mlalamikaji aliwataka polisi kuwaua ili wakawatafute watuhumiwa wengine, na kama sh 200,000 alizowapa hazikutosha, waseme ili akachukue nyingine katika ATM,” alisema Lyasato.

Akizungumza na Tanzania Daima, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Thobias Andengenye, alikiri kulifahamu tukio hilo lakini akasema kuwa taarifa alizopata ni kuwa, marehemu Mambosasa alipata kipigo kutoka kwa wananchi baada ya mtuhumiwa huyo kudaiwa kuiba.

“Hakuna ubishi kuwa marehemu hakupigwa, polisi hawakuwa watu wa kwanza kuwapata watuhumiwa hao, kwa taarifa nilizonazo ni kuwa polisi walipofika katika eneo la tukio walikuta mtuhumiwa amepigwa, walichofanya wao ni kumuokoa tu,” alisema RPC huyo.

Kwa mujibu wa Andengenye, baada ya kufanya wizi huo marehemu Seif alijihami kwa kukimbia na kuwa eneo alilokimbilia ni ambalo watu wanapita kama njia na kuwa watu wengi wanafanya kazi karibu na eneo hilo.

Hata hivyo, maelezo haya ya RPC yanakinzana na yale yaliyomo katika ripoti iliyotumwa kwa rais, ambayo inaonyesha kuwa polisi walitoa taarifa za uongo kuhusu kifo hicho na mazingira kilivyotokea.

Tuhuma hizi zinakuja katika kipindi kisichozidi miaka miwili tangu polisi kadhaa jijini Dar es Salaam, akiwamo aliyekuwa Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) mkoani humo, Abdallah Zombe, watuhumiwe kwa kuua raia wanne katika mazingira ya utata. Kesi yao ingali mahakamani.
 
mmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhh
 
Taarifa ya 2007 kipindi hicho Chadema walikuwa wanamuita Lowassa ni FISADI. Sasa hivi 2017 Chadema wanamuita Lowassa ni MKOMBOZI.

Aisee eeeeee
 
Lowassa yupo hamjampeleka Mahakama ya Mafisadi.Masamaki yuko guru ati hana tuhuma kazi ipo
 
Hizi "interrogation" za kishamba bado zinaendelea?
Oysterbay na Sitakishari walikuwa maarufu kwa utesaji.
Shuke kwa CID ni muhimu, Sirro awalete FBI na Scitland Yard kutia mafunzo.
 
Kwanini mtu asiwakariri hao wafanya huo unyama ili akitoka awafanyie na wao ili waone uchungu wake
 
Hili gazeti ni kifungashio tu cha maandazi.

Yaani wanamwita Yesu mtu anayedhaniwa kuwa mkombozi wa wakristo duniani???

Hii ni kashfa kubwa sana kwa wakristo kwa ujumla.

Waombe radhi ama la. Gazeti hili lisinunuliwe tena.
 
Back
Top Bottom