Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

NMBCzar

Member
Nov 20, 2016
8
80
- Mimi ni mkazi wa Tabata na mwajiriwa wa Benki ya NMB. Kwa maslahi mapana ya taifa na ya Benki hii, nadiriki kuyaweka maisha yangu na ajira yangu hatarini kwani nikijulikana either ntatoweka au ntafukuzwa kazi. Niko tayari kwa yote mawili, Ila siwezi kunyamaza kwenya kashfa la ajabu, aibu na la kijinga linalotia kinyaa kama hili linalotendeka ndani ya hii benki. Kwa lugha nyingine huu ni uozo, ambao nadhani serikali au Takukuru walichunguze. Hii benki haitaki kitu chochote kizuri kisichokuwa na maslahi binafsi kwa wakubwa. Nimeamua kuwa mpiga mbiu au kafara ikibidi.

- Kuna kampuni ya wajerumani walioleta teknolojia (suluhisho la uhakika) ambayo imeonekana kuwa ni ya hali ya juu kwenye maswala ya nishati. Wakazi wa Tabata tumeliona hili pale Kimanga kwa miaka miwili sasa. Ila hii teknolojia imepigwa vita kali sana ndani ya benki, na hatimaye hao wajerumani wakafukuzwa. Nimeambiwa walifukwa vibaya sana, wakiambiwa hawana vigezo kwa sababu walikubaliwa kufunga mitambo yao na afisa wa ngazi ya chini, huku hawa hawa viongozi wakiendelea kuchukua vitu vya hovyo kariakoo kuja kufunga kwenye hii saiti. Zaidi waliambiwa hawawezi kufanya lolote, wakitaka waende mahakamani

- Siku ya ijumaa 18/11/2016 niliondoka kazini mapema kidogo, mida ya saa 7 baada ya dada wa kazi kunitaarifu kwamba , mwanangu wa pili alirudishwa kutoka shule mapema baada ya kuonyesha dalili za kuwa na malaria. Pale Tabata Kimanga nina kabiashara kadogo, kwa hiyo nikaamua kupapitia kuangalia maendelo kabla ya kwenda nyumbani. Biashara yangu haipo mbali na jengo la ATM la NMB. Baada ya kuwasili, niliona umati mkubwa mbele ya jengo hilo, kidogo nilishtuka na kutaka kujua kulikoni. Wengi wa waliokusanyika pale, walionyesha kukerwa sana kwa sababu wajerumani walikuwa wanang’oa mitambo yao za kufua umeme walizofunga kwenye hizi ATM tatu za hapa Kimanga.

- Kwa wakazi wa Segerea, Kigogo, Buguruni, Ubungo, Tabata na viunga vyake vyote, wanalijua hili ATM kwa sababu ni sehemu pekee hapa DAR pakukimbilia umeme unapokatika kwa kipindi kirefu na huduma za ATM zikawa hazipatikani. Nina maana kwamba umeme unapatikana hapa masaa 24 na hakuna foleni. Waendesha bodaboda, wafanyabiashara wadodgo wadogo, na walinzi katika eneo hili walilitegemea sana hii mitambo ya wajerumani iliyokuwa inafua umeme na kutoa mwanga mkubwa pale umeme unapokatika hasa usiku. Kwa kifupi, hii sehemu haikuwa tu ni ya uhakika, ila pia ilikuwa ni kivutio kikubwa sana hapa Kimanga, ilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila aliyepita alisimama na kupashangaa. Jana nioni mida ya saa mbili nilipita pale, ni giza !

- Kutaka kujua zaidi kinachoendelea, nilimpigia simu mshikaji wangu wa kitengo cha IT. Mshikaji aliogopa kuongea nami kwenye simu, na kuniomba tukutane jioni ili tupate Kinywaji, ingawa naye alionyesha dhahiri kukerwa na huu uamuzi. Basi jioni yake tukakutana maeneo ya Bima, Cha kwanza kabisa, mshikaji alichoniambia, aisee, hii issue ni nzito, hawa wajerumani ni tishio, teknolojia yao imegusa maslahi ya wakubwa, jamaa wamechachamaa kule ndani. Walikuwa wanakula sana kwenye hizi ATM. Inveter na betri zimekuwa zinafungwa na makampuni yao. Hawataki kabisa kusikia juu ya hawa wajerumani. Kwa miaka miwili sasa, ATM ya kimanga ndio sehemu pekee ndani ya Benki ambako umeme ulikuwa haukatiki na wala simu za mitambo kusumbua zilikwisha kabisa. Idara inayoshugulikia maswala ya umeme na ATM maintenance zilifurahi sana na kudhania viongozi wangelipokea hii teknolojia kwa furaha zaidi na kuisambaza nchi nzima, lakini ikawa kinyume chake. Cha kushangaza zaidi, ni kwamba, hao wajerumani walifunga hiyo mitambo iliyotumika kwa miaka miwili bila kulipwa hata senti tano, na walipoanza kudai malipo ndio mambo yakaharibika

- Habari zilizovuja za ndani kwa ndani ambayo ndiyo sababu yangu kubwa ya kuvuja hii habari, ni kwamba, Mkurugenzi wa kitengo cha Ugavi, alitamba mbele ya wajerumani akiwaambia kwamba, aliyewapa ruhusa kufunga hii mitambo, ni mtu mdogo sana ndani ya benki. Kwa maana hiyo hawana vigezo kufanya biashara na NMB na hawatalipwa, kwa hiyo wao wakaondoe madude yao, na wawe tayari kusikia habari za huyo ofisa aliyewapa hidhini kufukuzwa ndani ya benki siku chache zijazo. Wakitaka wampe kazi. Habari zaidi zinadai kwamba, siku hiyo hiyo wajerumani walipong’oa mitambo yao pale kimanga, kampuni ndogo isiyoeleweka kutoka Kariakoo ilipewa hiyo kazi. Na kichekesho cha mwaka, pale wajerumani walipoanza tu kung’oa mitambo yao, ATM mbili ziligoma kufanya kazi na foleni ikaanza kwenye ATM moja iliyosalia. Huu ni uozo na uwenda wazimu, tangu lini vifaa vya kichina kutoka kariakoo vikawa na ubora zaidi ya vifaa vya Kijerumani?

- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati. Vinginevyo serikali iingilie kati. Takukuru wawachunguze hawa viongozi wanaoweka maslahi binafsi kwenye taasisi za umma na kuzuia vitu vya maana vinavyoweza kutatua kero za wananchi huku wakiangalia matumbo yao binafsi. Huyu ofisa kwangu mimi ni shujaa kwa sababu alileta suluhisho. Kwanini ageuzwe kuwa kafara?



Ndugu wana Jamiiforums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazopata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wanajukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili mojawapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.

NMB pia inapenda kuwahakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Endapo kutatokea umepata huduma isiyoridhisha au ufanyajikazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa Posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
Ndugu wana Jamiiforums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya utendaji mliouona kuwa si wa kuridhisha hasa kwa maendeleo ya benki yenu pendwa, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko hayo na kama ikibainika kuna watu kwa makusudi wamefanya hayo, tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi yao na wafanyakazi wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wanajukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili mojawapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.

NMB pia inapenda kuwahakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Endapo kutatokea umepata huduma isiyoridhisha au ufanyajikazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa Posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
Chama tawala shida(tuhuma za wabunge kuhongwa,n.k),watendaji serikalini shida,n.k sijui tukimbilie wapi!!!
 
Hapo ni kwenye tenda ya umeme wa ATM tu! Bado kwenye software, mafuta, chai, spea za magari nk. Watanzania wamelaaniwa kabisa! Ndio maana sishangai mabenki kufirisika, maana kila sehemu. Wapinzani wa serikali hii ambao wengi ni sehemu ya wapigaji njoo huku, "eti afisa wa chini"
 
75 Reactions
Reply
Back
Top Bottom