Kashfa nzito kodi ya dhahabu migodini; Serikali yavutana na Shirika la Fedha la Kimataifa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mwandishi Wetu


gold.jpg




Serikali yavutana na Shirika la Fedha la Kimataifa


KUMEJITOKEZA mvutano kati ya Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuhusu sekta ya madini nchini na hasa dhahabu, huku utafiti wa awali uliofanywa na Kampuni ya CRA-International, ukibainisha kuwa baadhi ya migodi ya dhahabu nchini, imekuwa ikijihusisha na ukwepaji kodi, Raia Mwema, imeelezwa.

Hali hiyo inajitokeza wakati ambao Serikali ikitarajia kukusanya takriban Sh bilioni 99.5 kutokana na utozaji mrabaha kwenye kampuni za uchimbaji katika miezi 12 kuanzia Juni, mwaka huu hadi Juni, mwaka 2012.

Hata hivyo, makusanyo hayo yanayotarajiwa ni kidogo mno, yakitajwa kufikia asilimia 4.5 tu ya mauzo ya dhahabu nje ya nchi, yanayofanywa na migodi ya dhahabu nchini.


Mvutano huo wa IMF na Serikali ambao umezua hali ya kutokukubaliana kwa pande hizo, umechangiwa na mapendekezo ya IMF kutaka mrabaha usiongezwe kinyume cha nia ya Serikali, ambayo imekuwa katika shinikizo la kupandisha mrabaha.


Kikao kilichoibua hali ya kutofautiana, ingawa mapendekezo mengine ya IMF yalikubaliwa na Serikali, kilifanyika Septemba 15, mwaka huu, Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, IMF waliwasilisha mapendekezo yao yaliyotokana na ufuatiliaji waliofanya kuhusu sekta ya madini nchini.

Msimamo wa Wakala wa Kodi Norway

Kikao hicho kilishirikisha pia taasisi nyingine ambazo zilitoa mtazamo wao, ikiwamo Wakala wa Kodi wa Norway (NTA), ambapo mwakilishi wake alielezea mgongano wa mtazamo kati ya migodi nchini na serikali.

Wakala hiyo ilieleza kuwa migodi ya madini nchini imekuwa ikieleza kulipa kodi
ya kutosha serikalini lakini wakati huo huo, Serikali imekuwa ikilalamika kutopata kodi ya kutosha kutoka kwenye sekta ya madini.


"Ingawa kiwango cha mapato kutoka kwenye migodi kimekuwa kikiongezeka, lakini changamoto bado ipo kwamba je, taarifa za gharama za uendeshaji zinazowasilishwa na mgodi ni za ukweli kiasi gani?


"Ukweli ni kwamba, hapa vyombo vya Serikali ni muhimu kujijengea uwezo kujiridhisha na taarifa za migodi hasa ya dhahabu," anaeleza mwakilishi wa Wakala wa Kodi Norway (Norwegian Tax Agency-NTA).


Msimamo wa Serikali ya Tanzania

Katika maelezo ya mwakilishi wa Serikali ya Tanzania, ilielezwa kuwa misamaha ya kodi, ambayo wadau wengine walipendekeza ifutwe au kuangaliwa upya, misamaha hiyo ni ya lazima hasa kwa miradi ya ufadhili.

"Katika suala la kuvutia mitaji, kuweka vivutio kwenye mfumo wa kodi si la lazima na wala si kigezo pekee cha kuvutia wawekezaji nchini. Vipo vivutio vingine ambavyo tunaweza kufanya, kama kuboresha miundombinu na mazingira ya uendeshaji biashara.


"Kwa hiyo, msamaha wa kodi hauwezi kuendelea kuchukuliwa kama kigezo pekee cha kuvutia mitaji ya kigeni nchini.


"Kampuni nyingi kubwa za kimataifa zimejijengea tabia ya kutangaza kupata hasara katika shughuli zake katika nchi za Afrika lakini wanatangaza kupata faida kwenye nchi zao ambako ndiko makao makuu ya kampuni hizo. Kwa nini? Nadhani kuna hujuma hapa!" alieleza mwakilishi wa serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.


Wakala wa Ukaguzi Madini nchini

Hapa ndipo mgongano ulipojitokeza, hasa baada ya IMF kupendekeza kutoongezwa utozaji mrabaha, na Serikali ilikataa.

Serikali kupitia Tanzania Mining Audit agency (TMAA) ilikataa mapendekezo hayo, ikisisitiza kuwa bei ya dhahabu imekuwa ikiongezeka duniani.


"Kuhusu hili suala la viwango vya utozaji mrabaha, Serikali inatambua viwango vinavyotozwa kwa sasa ni kidogo ikilinganishwa na nchi nyingine mfano Botswana na Ghana.


"Na kwa hiyo, Serikali inaendelea kufikiria kuongeza mrabaha na hali ya ushindani katika uwekezaji wa migodi ikaendelea kuwa bora.


Siri migodi ya North Mara na Geita

Katika hatua nyingine, uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwapo kwa Kampuni ya Kimataifa CRA-International, iliyofanya utafiti kuhusu migodi ya dhahabu ya North Mara na Geita.

Utafiti huo ambao ripoti yake inaweza kuwasilishwa serikalini na hususan Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), umefichua hujuma nzito zinazofanywa katika migodi hiyo ya dhahabu, ikihusisha mazingira ya utoaji taarifa za shaka kuhusu gharama za uendeshaji na hata mauzo ya dhahabu.


Taarifa za migodi hiyo ndiyo zinazotumiwa na Serikali kukokotoa hesabu zinazohusisha uendeshaji wa migodi hiyo ili kubaini kama inajiendesha kwa faida au hasara.


Raia Mwema
limepata ripoti ya awali ya utafiti huo ambao umehusisha migodi miwili mikubwa ya dhahabu nchini, North Mara Gold Mine, ulioko Nyamongo, mkoani Mara na Geita Gold Mining Ltd, ulioko Geita, mkoani Mwanza.


Kati ya mambo yaliyofichuliwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na migodi hiyo kujipatia mitaji kwa njia ya mikopo ambayo mazingira yake pia ni tata.


Ni kwenye hiyo mikopo ambamo, faida inayotokana na uuzaji dhahabu haikatwi kodi na badala yake, hufidia katika ulipaji mkopo hasa pale, kampuni inapoamua kujitangaza haikupata faida kubwa. Hali hiyo huifanya Serikali kutoambulia chochote kwa maana ya kodi.


Hali kama hii iliwahi kuzungumzwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.


Katika hotuba yake ya Bajeti Mbadala, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alisema: "Sehemu kubwa ya fedha zinazotokana na faida wanazopata (migodi mikubwa) kwenye mauzo ya dhahabu huishia kulipia madeni na riba na hivyo kukosesha Serikali mapato.


"Hii kwa wataalamu wa kodi, inaitwa ‘tax planning measures'. Muundo huu wa mitaji ya uwekezaji itapelekea makampuni haya kutangaza hasara kila mwaka," alisema Zitto, maelezo ambayo kwa kiasi kikubwa yamebainika katika utafiti huo uliofanywa na CRA-International.


Mwenendo wa sekta ya madini nchini si wa kuridhisha ingawa Rais Jakaya Kikwete, aliunda Kamati ya Kutafiti na Kupendekeza namna bora ya kufaidika na sekta hiyo, bila kudhulumu wawekezaji na Watanzania. Kamati hiyo iliongozwa na Jaji Mark Bomani na imekwishawasilisha ripoti yake kwa Rais.








 
Itakuwa Vizuri kweli kama IMF itawataja wachimbaji wote hapa nchini wa dhahabu wasiolipa Ushuru; madege yanakuja kupakia dhahabu na kuondoka kama vile hakuna sheria ya nchi
 
Itakuwa Vizuri kweli kama IMF itawataja wachimbaji wote hapa nchini wa dhahabu wasiolipa Ushuru; madege yanakuja kupakia dhahabu na kuondoka kama vile hakuna sheria ya nchi

Sijui hiyo 3% ya royalties ni ya kitu gani....Mpaka hii leo bado hii ni siri kubwa sana.
 
Hii nchi ingekuwa na viongozi wenye ujasiri wangetangaza kiasi cha kodi anayataka kuchimba madini abaki asiyetaka apande ndege aende kuchimba kwingine - very simple. Sijui kwa nini wanakaa chini kuvutana kuhusu kodi? Madini hayaozi, kwa jinsi hali ilivyo haya madini hayatusaidii kabisa kwa hiyo tunaweza tu kukaa bila kuchimba hadi hapo tutakapoamua kuyachimba wenyewe.
 
Hapa ndipo ninaposema UwT umelala, siku hizi kazi yake ni kufanya u-spy wa kuhakikisha viongozi wanakuwepo madarakani. Nikikumbuka enzi ya UwT ya awamu ya kwanza, haya yasingeweza kutokea.

Tunajua watu wanaoingia UwT pia ni wataalamu wazuri, kwanini hawapenyezi watu wao katika senior levels kwa ajili ya kubaini haya? Kazi yetu ni kluuza sura tu, na maneno mazuri mazuri kila kukicha. Utasikia wanasema and I quote "....serikali inaanda mikakati endelevu...." "....serikali ika katika mchakato...." Mikakati na michakato isiyokuwa na time frame. My foot!!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nilishaachaga kulalamika mimi, nangojea siku tutakapoamua kwamba imetosha
 
Tuliokuwa tukionekana mahayawani kutaka hawa wachimba madini walipe kodi nafikiri tunaanza kufahamika sasa. Dhahabu wachukue, mafuta ya kuchimba madini tuwasamehe kodi, kodi hawalipi halafu watulipe royalties ya 3% kuna msemo maarufu wa ndugu zetu wa kichagga wanasema Yesuuu!!! Waislamu wanatamka Allah Akbar!!! maana mtu unaweza kupandwa na hamaki ukavunjilia mbali computer huu sijui hata niuitaje?
 
Hiyo issue ya kodi IMF wamekuwa wakiisema tangu enzi na enzi; nakumbuka wakati nikifanya MSc. 10 years ago huko nchi fulani, hao IMF mwakilishi wake alikuja kutufundisha then one of the student akauliza mbona ninyi mnaweka masharti magumu alafu unakuja kutuchanganya hapa darasani kuwa nchi zetu na sera za nchi zetu zina matatizo makubwa ni aje?

Jibu likawa...tukiwaambia serikali zenu ziangalie makusanyo ya kodi na kubana watu wao walipe kodi wao wanaenda kuongeza kodi kwa wauza maandazi na wauza mahindi ya kuchoma badala ya kuongeza kodi kwa giants kama makampuni ya madini; wenye meli kubwa za kuuza samaki; wauza magogo and so on... Sera ztu vile vile hazizingatii hali halisia ya uzalishaji zina maneno mazuri yasiyotekelezeka; akamalizia kusema corruption is the main source of all these issues!

Hii bado limekua ni tatizo letu kubwa na nimekuja kuelewa kwakadri nilivyofanya kazi nchini kuwa si kwamba viongozi hawalijui hilo nooo bali kwajinsi hiyo ndivyo ambavyo wao kama individuals wanafaidika kwa kiasi kikubwa kwani loopholes za kujipatia mapato makubwa zinakuwa nyingi narahisi bila sheria kuwabana...
 
Back
Top Bottom