Kashfa nyingine Magereza

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,070
253
UONGOZI wa juu wa Jeshi la Magereza nchini unakabiliwa na kashfa ya matumizi
mabaya ya fedha kupitia miradi yake ambapo sasa imebainika kuwa zaidi ya Sh bilioni
mbili zimetumika katika utekelezaji wa mradi wa ‘Bayogesi’ kinyume na utaratibu.

Bayogesi ni chanzo cha nishati ipatikanayo kwa kuozesha aina zote za tungamotaka
(biomass), hasa kinyesi katika mchanganyiko ambao unatakiwa uwe na kiasi kidogo sana
cha hewa ya oksijeni (anaerobic digestion).

Bayogesi inajumuisha asilimia 60 ya methane na asilimia 40 ya hewa ya ukaa
(carbondioxide).

Mara nyingi hutumiwa majumbani kwa kupikia na kutoa mwanga wa taa.

Chanzo chetu kimeliambia gazeti hili kuwa mradi huo ambao ulianza kutekelezwa takribani
miaka miwili iliyopita katika Gereza la Ukonga ulipaswa kugharimu Sh milioni 700, lakini
mpaka sasa umegharimu zaidi ya Sh bilioni 2, licha ya kwamba bado upo katika hatua za awali za utekelezaji wake.

Chanzo hicho kilisema kuwa mradi huo ulipaswa kutekelezwa katika kipindi kisichozidi
miezi minane hadi mwaka mmoja, lakini kumekuwepo na ucheleweshwaji unaodhaniwa unalenga kuongeza gharama.

Ucheleweshwaji huo umeongeza gharama zaidi ya mara tatu ya fedha zilizokuwa zimetengwa, kwa mujibu wa chanzo hicho na kwamba hadi sasa miaka miwili ilishakwisha.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa mkandarasi ambaye ni kampuni ya Ainea
Kimaro Co Ltd, alipewa kazi hiyo bila kufuata taratibu za zabuni na amekuwa ikifanya
kazi hiyo bila kuwa na kampuni ya ushauri, jambo ambalo limesababisha kazi hiyo kukwama
huku kukiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa mpaka sasa.

Gazeti hili limewasiliana na uongozi wa kampuni hiyo ambayo pia iliwahi kutekeleza mradi
kama huo katika Magereza ya Rwanda kati ya mwaka 1999 hadi 2006, na kuthibitishiwa
kwamba ndio inayotekeleza mradi huo.

Hata hivyo uongozi wa kampuni hiyo haukuelezea zaidi juu ya kashfa hiyo kwa madai
kwamba Magereza ndio wenye maelezo yote kuhusu mradi huo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kampuni hiyo inayodaiwa kuwa na ubia na mmoja wa
viongozi wa juu ndani ya jeshi hilo, ilishalipwa fedha zote (Sh milioni 700) zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo hadi utakapokamilika,lakini imekuwa ikiendelea kulipwa fedha za ziada na jeshi hilo.

Malipo hayo yamekuwa yakitolewa kwa madai kwamba makadirio ya mradi huo yalikuwa
madogo hivyo zinahitajika fedha za ziada na kwamba malipo hayo yamekuwa yakifanyika
kwa maelekezo ya 'kigogo’ huyo.

Mkaguzi wa nje (External Auditor), aliyetambulika kwa jina moja la Suba, alipoulizwa
kama alishawahi kukagua utekelezaji wa mradi huo alisema kwamba haufahamu kwani
hakuwahi kuukagua.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Mzee we mjelajela nini? Mpaka uwe na interest na habari za hawa jamaa ni lazima utakuwa na ufahamu nao angalau kidogo. Elewa saizi kila idara ya serikali ni uchakachuaji? Ni PM kwa habari zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom