Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Acha tuhoji sasa. Hii ni kansa ya kimya kimya na wahanga ni wengi japo hawasemi.
Madai yaliyopo ni kwamba mtuhumiwa ukikamatwa, halafu simu yako ikachukuliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi, basi andika maumivu! Tena zinafanyiwa refurbishing kabisa!
Ni mara chache sana watuhumiwa hurudishiwa simu zao. Unaweza kuachiwa kwa dhamana lakini upelelezi ukachukua mwaka mzima na zaidi. Mpaka unakata tamaa.
Nataja simu kwa sababu ndio "zinapendwa" zaidi. Lakini kuna iPads na Laptops pia.
Nahoji hili kwa sababu maneno yanasemwa sana chini chini na naona yanalitia doa Jeshi letu tukufu linalofanya kazi ngumu ya kulinda raia na mali zao usiku na mchana.
Ni kweli wazee mna kamradi maalum ka kuziuza simu hizo kwenye "black market" na wadosi?
Hili lichunguzwe!