Kashfa mpya: Kamati ya Bunge yahongwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa mpya: Kamati ya Bunge yahongwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kipa, Apr 1, 2009.

 1. k

  kipa Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  QUOTE

  Katibu wa Bunge akiri kufahamu tuhuma hizo

  na Mwandishi Wetu
  IKIWA takribani wiki moja sasa tangu gazeti hili liliporipoti jinsi wabunge wanavyochuma mamilioni ya fedha kupitia malipo yao halali ya mishahara, posho na fedha nyinginezo zinazotokana na malipo yao rasmi wanayostahili, baadhi ya wabunge wametuhumiwa kuhongwa zaidi ya sh milioni 200 na kampuni moja binafsi ili kuipa upendeleo.

  Habari za uhakika zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano zinadai kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (majina tunayahifadhi kwa sasa), walihongwa na kampuni ambayo pia tunahifadhi jina lake kwa sasa, ili wasiikwamishe kupata mradi iliyokuwa ikiunyemelea.

  Taarifa hizo zinaeleza kuwa, kamati hiyo ya Bunge yenye wabunge kadhaa machachari wakiwamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ilipewa fedha hizo ili kuwaziba mdomo wajumbe wa kamati hiyo, wasihoji uwezo wa utendaji wa kampuni unaodaiwa kuwa ni wa kiwango cha chini kulingana na ukubwa wa mradi iliyoomba kuutekeleza.

  Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake gazetini, alithibitisha yeye na wanakamati wenzake kupewa fedha hizo.

  Alisema suala hili lilifanyika kwa tahadhari kubwa kwani hakuna ushahidi unaoweza kuwatia hatiani kuhusu kuchukua fedha hizo.

  Uchunguzi wa kina wa timu ya waandishi wa gazeti hili umebaini kuwa, tayari viongozi wa juu serikalini wamekwishapata taarifa za kamati hiyo kuhongwa, na wameamuagiza Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah kuchunguza tuhuma hizo na kutoa taarifa.

  Kwa mujibu wa uchunguzi huo, serikali ilishtushwa na taarifa za wabunge hao kuhongwa, kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi yao walikuwa wakichukuliwa kama viongozi wa kupigiwa mfano.

  Kwa mujibu wa habari hizo, serikali imetoa pia kazi ya kuchunguza tuhuma hizo kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambavyo vitatoa taarifa kwa viongozi wa juu serikalini.

  Akizungumza na gazeti hili jana kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu kuwapo kwa tuhuma hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Kashillilah alikiri kuwa na taarifa hizo, lakini alieleza kuwa hajapata maelezo ya maandishi kutoka serikalini ya kumtaka kuchunguza suala hilo.

  “Ni kweli nimesikia kuhusu jambo hilo, taarifa hizo ninazo, kuna kitu kama hicho, lakini sijapata barua rasmi kutoka serikalini inayonitaka kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.

  “Hata hivyo, mimi sina nguvu za kufanya uchunguzi kama huo hata kama nikitakiwa kufanya hivyo, lakini jambo linalonishangaza, na kwa kweli siamini, ni kama barua hiyo ambayo ni ya siri sana imenyofolewa kutoka katika ofisi za Bunge.

  “Lakini baadhi ya wabunge wanajua ni kwa nini wanafanya hivi! Mimi sina ruhusa ya kutoa maelezo kuhusu mambo ya Bunge, msemaji ni Spika, akielekeza jambo kwangu naweza kulitolea ufafanuzi. Na ni vizuri uelewe kuwa hawa wabunge ni viongozi wakubwa, sasa kuzungumzia tuhuma zao magazetini ni jambo kubwa mno.

  “Tuvute muda, ngoja niwasiliane na wakubwa, nikiwa katika hali ya kulizungumzia hili, nitatoa maelezo. Lakini kwa sasa ninachoweza kusema ni kwamba sijui ni kamati gani, na ilipewa sh ngapi,” alisema Dk. Kashillilah.

  Naye Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tuhuma hizo, alijibu kwa ufupi kwamba hana taarifa zozote kwa sababu hakuwapo ofisini kwa siku kadhaa, na kwamba aliingia nchini jana akitokea nchini Afrika Kusini.

  Hata hivyo, Spika Sitta aliahidi kuwa atawasiliana na wasaidizi wa ofisini kwake ili kujua kama kuna barua yoyote kutoka serikalini inayotaka wabunge wanaotuhumiwa kwa kosa hilo kuchunguzwa.

  Kwa muda wa takribani mwezi mmoja sasa, kumekuwa na malumbano baina ya wabunge, huku baadhi yao wakishutumiana kwa kuhongwa na kukiuka maadili ya ubunge.

  Malumbano hayo sasa yanaonekana kuanza kuchukua sura ya kuumbuana baada ya baadhi ya wabunge kuanza kutoa siri za wenzao ambazo hapo awali zilikuwa zimefichika
  .........................................................................................................

  Mhhh utamu huuu, sijui kamati gani hii, hembu nianze kuchakurachakura kwenye hili faili


  Regards
  kipa
   
 2. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu umbea,kama na habari taja majina taja jina la kampuni,otherwise acheni kuchuma pesa kwa kuandika habari ambazo hazina uhakika. Kama una uhakika utaandika majina bila kificho.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kunamradi gani mkubwa naona utakuwa ule wa national ID ambao ulionyesha kuna kundi au mtu amekosa hiyo takirima.
   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  kamati ya mafweza ilivyotetea dowans????????
  mpaka mmoja wao akaitwa dowans tehetehe!!!!!!!!!!!!
   
 5. E

  Edo JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sio sikukuu ya wajinga hii?????
   
Loading...