Kashfa kubwa kwa viongozi wa CCM kuhusu upigaji 10% ya mikopo ktk halmashauri

Jul 3, 2020
29
63
Kumekuwepo upigaji mkubwa wa pesa za mikopo ya 10% kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

Pesa hizo zinazelenga kutolewa kwa makundi maalumu kama ya vijana,wanawake na walemavu.

Kashfa hiyo inawahusu viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini kabisa kama wajumbe, wenyeviti na makatibu wa matawi,mashina,
madiwani na wabunge.

Viongozi hao wamekuwa wakila pesa hizo kwa kuunda vikundi feki vya makundi hayo maalumu na kujinufaisha na pesa hizo kinyume cha sheria huku wakipata baraka kutoka viongozi wa halmashauri.

Huku hayo yakifanyika PCCB yaani taasisi ya kupambana na rushwa ikifumbia macho uozo huo wa wizi
wa pesa za mikopo bila ya hatua yoyote ya kisheria.

Wahanga wakubwa ni walengwa wa mikopo hii kwani makada na viongozi wa CCM wamejimilikisha mikopo hii na kuigeuza ya chama.

Rejea kashfa ya upigaji ktk wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Kwa kashfa hii viongozi wote wa CCM waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria hasa madiwani na wabunge ili tabia hii ikome kabisa.
 
Back
Top Bottom