BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,889
Hakuna haja ya tume nyingine tena itumie mabilioni for doing nothing! Tunachotaka ni kuona wahusika wote wanatiwa ndani haraka sana na kufikishwa mahakamani kujibu hatia dhidi ya ufisadi na wahusika wote wafilisiwe mali zao. Tumechoka na tume zisizokuwa na manufaa yoyote!
Posted Date::1/22/2008
Tume ya kufuatilia ufisadi BoT yaanza kazi
Na Tausi Mbowe
Mwananchi
TIMU iliyoteuliwa kufuatilia taarifa ya ukaguzi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu upotevu wa fedha za akaunti ya Malipo ya Kigeni (EPA) imeanza kazi yake rasmi kwa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Tume hiyo iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufutia kampuni ya Ernest & Young kubaini kuwa kulikuwa na upotevu wa zaidi ya Sh133 bilioni katika mazingira ya kutatanisha ndani ya benki hiyo na hatimaye Rais Kikwete kutengua wadhifa wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daud Ballali.
Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni Mwenyekiti wa Timu hiyo, Johnson Mwanyika ilisema tayari timu hiyo imeshaanza kazi yake na wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa wa wananchi.
Timu hiyo imesema kuwa itakuwa makini kwa nia ya kuhakisha kuwa ukweli unajulikana na kuweka wazi hadharani ili kulinda heshima ya Taifa kwa kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini. Kwa mujibu wa Mwanyika nia ya timu ni kufanya kazi yake kwa uhakika na kuwaomba wananchi kuwa na subira na kutoa kila ushirikiano utakaoiwezesha timu hiyo kukamilisha majukumu yake.