Kashfa Bandarini: Wafanyakazi watatu wa TRA wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Mahebe

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
319
63
attachment.php
 
Attachments

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.jpg
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.jpg
    165.9 KB · Views: 22,173
SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili. Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.

Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,alisema Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.

Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.

Katika kikao kilichofanyika bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

Waziri Mkuu alisema upotevu huo unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

MICHUZI BLOG
 
Waangalie na malipo ya umeme yanayofanyika kwa mitandao, inawezekana nako pia takwimu haziendani.
 
Hakika kila zama na nabii wake
tanzania ya kuwajibika imeanza kuchukua hatamu yake taratibu
mungu ibariki tranzania yetu ambayo misingi yake ilipotea siku nyingi.
 
Mtukufu Rais alisema "Mtumishi wa UMMA ukifanya makosa usitegemee kuhamishwa kituo cha kazi, utafukuzwa (nitalala nao), naona sasa kauli yake inatimia.Ikigundulika hao jamaa wamepiga pesa za umma fukuzia mbali huko.
 
paragraph tatu za mwisho hazikupaswa kuwepo....hayo yalishasema jana na kuanza kutekelezwa...
 
Waangalie na malipo ya umeme yanayofanyika kwa mitandao, inawezekana nako pia takwimu haziendani.
Huko mimi ndiyo nimechoka ukiwa mbagala Dar ukanunua umeme kwa mtandao wa sh.10,000 utapata Units 77.7 na ukiwa Morogoro- Misufini kwa ela hiyo unapata units 28.4 wakati makato ni yale yale, Tarif ni ile ile (moja) na Mtandao uliotumia kununulia ni ule ule...!
============================
Hivi huyo Robert Nyoni ana uhuhusiano wa kiundugu na Blandina ('Irion' Lady)...!?
 
Nami nilijiuliza hilo swali na nikakumbuka huyu aliwahi pata skendo wizara ya Afya baada ya mgogoro wa madaktari nadhani na akapelekwa/kurudishwa TRA pale kama boss fulani (sikumbuki nafasi ipi). Inawezekana kabisa wana uhusiano wa kindugu.

Nchi ya Shaaban Robert angalau imeanza kupata mwanga yaweza ikawa sehemu ya dunia na kujitoa katika ulimwengu wake wa kusadikika
 
Jana nilishangaa kusikia hao wafanyakazi wa TRA wanahamishwa kituo, yaani mnatoa uchafu bandarini mnaupeleka mikoani? kwani huko ndiko kuliandikiwa uchafu?
 
Mtukufu Rais alisema "Mtumishi wa UMMA ukifanya makosa usitegemee kuhamishwa kituo cha kazi, utafukuzwa (nitalala nao), naona sasa kauli yake inatimia.Ikigundulika hao jamaa wamepiga pesa za umma fukuzia mbali huko.

Sio fukuzia mbali..filisi na weka segerea..wanakula raha wakati wananchi wanaishi kwa shida!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom