MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 884
Habari za uhakika kutoka Urambo zinasema kuwa baada ya Sitta kutoswa uspika, aliekuwa diwani wa urambo mjini(CCM) ndg Ali Mwiniko amefanya sherehe kubwa jana kufurahia anguko la bwana Sitta. Sababu ni kwamba, anamshutumu Sitta kuwa ndie aliechangia CCM kupoteza kata tano ktk uchaguzi wa mwaka huu ambapo zimekwenda upinzani ikiwamo pia kata ya Urambo mjini ambapo diwani huyo aliangushwa vibaya na Mgombea wa Chadema aitwaye Amatusi Ilumba. Diwani huyo ana bifu kubwa sana na Sitta. Habari ndio hiyo kutoka Urambo.