Kashata Ya Bububu

AmaniGK

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,149
365
Karatasi nakamata,kueleza yalosibu
Nna kipande cha kashata,nlichonunua Bububu
Kashata yenye utata,utamuwe wasulubu
Nimeziona kashata,ya bububu ni pekee

Kitaka kula najing'ata,kwa utamu so kifani
Nikimung'unya nadata,Sijui sababu gani
Tamu zaidi ya bata,Alopakwa Asumini
Nimemung'unya kashata,ya bububu ni pekee

Sikuinunua kwa shaka,nlipoiona bububu
Ulimi ulinitoka,nilitamani kutubu
Nilijiona kishoka,rudi bara nliona tabu
Nimezing'ata kashata,ya bububu ni pekee

Utamuwe wa milele,nnapoilamba ni tabu
Chachu kama uwele,hata sijui sababu
Ina sukari kichele,ni dawa tena tabibu
Nimeshaonja kashata,ya bububu ni pekee

Kashata yangu naficha,simpi mtu yeyote
Naila usiku kucha,wala sendi kokote
Utamu lojificha,tamanisha siku zote
Nimeziona kashata,ya bububu ya pekee

Amani
Malenga wa jamii
 
Karatasi nakamata,kueleza yalosibu
Nna kipande cha kashata,nlichonunua Bububu
Kashata yenye utata,utamuwe wasulubu
Nimeziona kashata,ya bububu ni pekee

Kitaka kula najing'ata,kwa utamu so kifani
Nikimung'unya nadata,Sijui sababu gani
Tamu zaidi ya bata,Alopakwa Asumini
Nimemung'unya kashata,ya bububu ni pekee

Sikuinunua kwa shaka,nlipoiona bububu
Ulimi ulinitoka,nilitamani kutubu
Nilijiona kishoka,rudi bara nliona tabu
Nimezing'ata kashata,ya bububu ni pekee

Utamuwe wa milele,nnapoilamba ni tabu
Chachu kama uwele,hata sijui sababu
Ina sukari kichele,ni dawa tena tabibu
Nimeshaonja kashata,ya bububu ni pekee

Kashata yangu naficha,simpi mtu yeyote
Naila usiku kucha,wala sendi kokote
Utamu lojificha,tamanisha siku zote
Nimeziona kashata,ya bububu ya pekee

Amani
Malenga wa jamii
Hiyo lazma ni kashata y bangi
 
Back
Top Bottom