Kasaloo Kyanga is no more

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,799
30,725
Heshima kwenu wakuu.

Yule mwanamuziki mahiri mwenye sauti ya dhahabu Kasalo Kyanga amefariki dunia leo.

Kasalo Kyanga atakumbukwa sana kwa tunzi zake nzuri tangu akiwa Matimila,Toma Toma,Tancut Almasi na Maquiz du zaire.
Baadhi ya tungo zake [1] Nina kwenda safari na Karubandika.

Source;Radio one kipindi hizi nazo.
 
Mara ya mwisho nilimwona mahojiano yake live alikuwa amechoka sana ngozi ya mwili ilichakazwa na vipele vyeusi pia sura yake ilikuwa imebadilika sana labda umri !.

RIP Kasalo Kyanga msalimie pacha wako Kyanga Songa.
 
<font size="3"><span style="font-family: lucida console"><b>Mara ya mwisho nilimwona mahojiano yake live alikuwa amechoka sana ngozi ya mwili ilichakazwa na vipele vyeusi pia sura yake ilikuwa imebadilika sana labda umri !.<br />
<br />
RIP Kasalo Kyanga msalimie pacha wako Kyanga Songa.</b></span></font>

Mkuu huo uchambuzi wako vipi tena?
Anyway........labda ni umri!
 
tatizo hili bado linatusumbua wabongo, fikiria Hayati Phili Lutaya alipata ujasiri miaka ya themanini (1980s) lakini sisi leo mwaka 2011 tunaumauma maneno ...say it out please!
Mkuu huo uchambuzi wako vipi tena?
Anyway........labda ni umri!
Mara ya mwisho nilimwona mahojiano yake live alikuwa amechoka sana ngozi ya mwili ilichakazwa na vipele vyeusi pia sura yake ilikuwa imebadilika sana labda umri !.

RIP Kasalo Kyanga msalimie pacha wako Kyanga Songa.
 
RIP Kasaloo. He was a talented composer/vocalist. Nakumbuka zile nyimbo zake tamu akiwa Tancut Almasi (Safari sio kifoooo mama watoto..... Subiri nitarudiii mamaa... Nikirudi mama nitakuletea zawadi.... zawadi nono.... mama watooto.)
 
Heshima kwako Lukindo.

Mkuu nakubaliana na hoja yako.Siku hizi magonjwa ni mengi sana unaweza kumdhania mtu tayari kaukwaa UKIMWI kumbe ana kisukari ndiyo maana nilijaribu kuweka angalizo labda ni umri.

tatizo hili bado linatusumbua wabongo, fikiria Hayati Phili Lutaya alipata ujasiri miaka ya themanini (1980s) lakini sisi leo mwaka 2011 tunaumauma maneno ...say it out please!
 
Far right...... John Kitime on the left....TANCUT ALMASI

with+kasaloo+kyanga.JPG
 
Kutoka kushoto Buhero Bakari(trumpetor),Abdul Salvador(Faza Kidevu),Kasaloo Kyanga, Asha Salvador(mke wa Abdul), na Kyanga Songa Miembeni Bar Ilala..........1986 Tancut Orchestra

kyanga.jpg
 
R.I.P Mnyalukolo kasolo kyanga,namkumbuka nywele zake nyingi alivyokuwa anazitunza vizuri
 
nakumbuka railway gerezani club akiwa na sambulumaa chini ya Nguya Viling enzi vyombo vya music deal kinoma. RIP KASALOO
 
R.I.P Kasaloo Kyanga Mzee wa masafa marefu

Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Ninakwendaa safari, safari yenyewe ya masafa marefu,

Lakini usisikie yaoo mama watoto oo,&#8230;&#8230;&#8230;&#8230;&#8230;..,

Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu&#8230;&#8230;&#8230;&#8230;&#8230;.,

Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,
Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,

Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,
Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,

Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili

Iyeye, oo mama iyee,

Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Zawadii nono, mama watooto.

(a keba, keba, keba, keba, keba, keba, keba, kebaaa,)
(fimbo, fimbo, fimbo, fimbo, lugoda,lugoda, lugoda, lugoda - Mangalaa..
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom