Kasaka Arudi CCM!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,681
40,623
Unawezaje kuung'ata mkono unaokulisha? Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Lupa (Chunya) Bw. Njelu Kasaka ameamua kurudi kundini!! Bw. Njelu alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha wabunge 55 waliodai bungeni kurudishwa serikali ya Tanganyika!! Alijaribu kuwa mwiba kwa CCM lakini "wakuu" wakaamua kumtupa nje..!!
 
Tanzania kuna political terrorism si rahisi kama mtu kama huna roho ngumu kufanya upinzani wa kweli .Lakini baada ya kurudi watu watajiuliza anataka nini ? Kweli alikuwa na madai ya uhakika ? Amekosa ambacho kimemfanya arudi ? Aanategemea nini baada ya kurudi ?Je atafaniukiwa kukipata baada ya kurudi ? Iko kazi kubwa wacha nisikilizie wengine mnasemaje .
 
Mzee Mwanakijiji,

Tulikuambia, CCM hawana mipango ya maendeleo ya wananchi, lakini inapokuja kushikilia power hilo hawana mchezo nalo, hata kama wanachukiana kiasi gani, kwenye hilo la power wanaelewana,

tena wote kuanzia Mkapa, Kikwete, Sumaye, Malecela, Kingunge, Kinana, Mahita, wote wanajichanganya, ila kukiwa shwari ndio utasikia vijembe wanapigana wenyewe kwa wenyewe,

ole wako uwasaliti, hapo hapo wanasahau matatizo yao na kukugeuzia kibao, huyo Kasaka ilibakia kidogo ale vumbi maana mpaka umeme kwenye nyumba yake walikata!
 
Mzee ES, umefanya nywele zangu zisimame... ndo maana mimi siamini hata chembe kuwa siku chama kingine kikishika madaraka CCM wataridhia kiulani.. Ila wasidhanie kuwa watatawala milele!!! Chama hiki kinatisha!!!
 
Wazee Wanabodi, haya ni maneno ya Mbunge wa zamani wa CUF, aliyerejea CCM, na kupokelewa na Rais Kikwete,

Mbunge wa zamani wa CUF, ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa uenezi wa sera za CUF, taifa, Bwana Hiza Tabwe, akizungumzia kiurudi kwake CCM,

Quotes:

"Kuna machache sana yalichangiwa na upinzani katika kuleta mabadiliko ya maendeleo ya nchi yetu, lakini mafanikio hayo yote yanatokana na mchango wa busara za viongozi wa CCM na serikali yake."

"CUF wamejitahidi sana kuikosoa serikali ya CCM ingawa kwa mambo machache yaliyokuwa na ukweli, na mengi yasiyokuwa na ukweli ili tu kutaka kuungwa mkono na wananchi, pamoja na CUF kuelewa fika kuwa ulikuwa ni upotoshaji wa ukweli ili tu waungwe mkono na kukubalika kisiasa"

"Mambo mengi yanayosemwa na upinzani, huwa ni njama tu za upinzani kutaka kujiongezea umaarufu na wananchi, kwa mfano madai kuwa CCM haijawahi kuleta mafanikio ya maendeleo, tangu taifa letu lipate uhuru. Kauli kama hiyo ni miongoni mwa dhambi kubwa niliyowahi kuifanyia CCM na watanzania wote kwa ujumla huku nikiwa ninajua kuwa ni uongo wa hali ya juu, nikiwa CUF."

"Wapinzani husema mambo mengi ya uongo ili tu kuwapa matumaini wafuasi wao, na moja ya kauli hizo ni kuwa mimi nimenunuliwa na CCM!"

"....Kwa hiyo sioni nguvu mbele ya hoja za upinzani kiasi cha kuwafanya wananchi waamini hayo, kwa sababu CCM inakubalika miongoni mwa wananchi asilimia 98%, ya watanzania wote, sasa chama kinachokubalika kiasi hicho na umma kinawezaje kuninunua mimi mtu mmoja? kwa manufaa gani niliyonayo yanayopita ya wananchi aslimia 98%, na wananchama wake ambao ni kwa kwa mamillioni ya wananchi?"

Ok Guys What is up with this?
 
Uchu wa madaraka alio nao Tambwe sijawahi kuona mtu mwingine anao labda ni Nchimbi wa CCM na CCM kwa ujumla lakini Tambwe ni mtu ambaye ukimwahidi madaraka he can do anything .

Tambwe anajua kupanga hoja sana na ni mtu wa majungu na sasa kaingia CCM basi kafika mahapa pake maana kule bila ya majungu bwana huna nafasi .Tambwe kautaka Ubunge kuanzia mwaka 1995 akiwa NCCR hadi CUF akaukosa leo anasema haya baada ya kuukosa .Lakini pia nakubaliana na hoja yale juu ya matamshi baadhi ya CUF na s upinzani .Kuna wapinzani kama yeye , Mrema nk wana mambo yao na si kuwatumikia wananchi .

Swala la kusema uongo ili kupata kura hufanywa na watu wote kwenye siasa na hasa wanapokuwa kuwa siyo sincere . Kumbuka mwaka 1995 Pale Temeke JK anahutubia mkutano wa CCM ili Mrema apigwe chini .JK alitamka maneno haya ,Wananchi wa Temeke ichagueni CCM maana baada ya hapo tatizo la maji litaisha kwa kuwa Banki ya Dunia imetoa pesa kwa ajili ya kumaliza tatizo hili Temeke.Wakati huo nadhani JK alikuwa Nishati ama Fedha .JK alijua anasema uongo na hadi sasa maji Temeke ni hadithi yeye akiwa Rais . Mwaka 1996 nilikutana na JK Hilton Hotel London nikamuuliza juu ya maneni yake yale kule Temeke na yeye alijibu hivi , Shemeji wewe ulitaka watoto wangu wasiende chooni ?Akimaanisha kwamba alikuwa anamwaga soga kupata kura lakini Bank ya Dunia ikitoa pesa zinagawawia katika miradi ambayo iko katika progress .Hawa ndiyo wanasiasa wetu na leo JK ni Rais wetu .

Tambwe hawezi kusema mbele yangu mimi .Nilimuokoa alipoigwa chini na NCCR kw akosa la ku forge vyeti .Wakati huo akina Lamwai wanavuma Upinzani na yeye aliondolewa kugombea alikuja nyumbani kwangu saa tisa usiku na kuomba msaada . Nguvu yangu ikiwa kubwa sana ndani ya Chama hicho Kiwilaya .

Kwa majungu na tamaa zake na tabia ya kusema uongo alikosana na Mrema akaingia CUF .Kule nilijuua hatadumu na anajuwa kuwatumia walala hoi ili apate akitakacho . Leo Tambwe anasema maneno haya ? Tambwe ninamfaham,u hadi chumbani kwake huyu ni mnafiki na si mwana siasa wa kweli . Chukueni maneno yangu na mtamsikia Temeke na CCM yenu ila sema CCM watamdhibiti maana wanamjua vyema.Naamini anautaka Ubunge lakini kachelewa maana yeye na Abbas Mtemvu wote walikuwa wanafanya biashara haramu sana kuipa serikali mzigo mkubwa kwa kutoa tenda za kijinga na hasa Mtemvu na garage yake ya Temeke . Akibisha ninaweza kumkumbusha na hata kuomba doc fulani zipitiwe kuona ukweli juu ya uharamia wao .

Ni uhuru wa Tambwe kuingia hata chooni ila asilete nyondo tuna habari zoooooooooooote .
 
Mzee Shughuli Bwana,

Mimi huwa nawazimia wakata issue kama nyinyi, Hivi babu Ubwete yupo wapi? Kyoma?!?.

Mzee ES, kwa jinsi ninavyojua, wanasiasa wengi ni waongo tena wa kutupa, wewe unajua hilo nalabda una Phd (isiyo rasmi:)) kwenye fani hiyo, maana umo ndani.

Kuna ka hadithi flani kuhusu wanasiasa waliokuwa wanasafiri na basi, wakapata ajali karibu na shamba la mkulima mmoja. Masaa machache baadaye, polisi walipofika kuulizia kama kuna majeruhi, mkulima akawaambia, hahhhaaa bwana mi nimewazika wote! akaulizwa hakuna majeruhi? akajibu kuna wengine walidai wameumia etc lakini wanasiasa ni waongo mi najua walikuwa wamekufa!!!!

Tambwe ni mmoja wa hao wanasiasa!

FD
 
Mzee Shughuli Bwana,

Mimi huwa nawazimia wakata issue kama nyinyi, Hivi babu Ubwete yupo wapi? Kyoma?!?.

Mzee ES, kwa jinsi ninavyojua, wanasiasa wengi ni waongo tena wa kutupa, wewe unajua hilo nalabda una Phd (isiyo rasmi:)) kwenye fani hiyo, maana umo ndani.

Kuna ka hadithi flani kuhusu wanasiasa waliokuwa wanasafiri na basi, wakapata ajali karibu na shamba la mkulima mmoja. Masaa machache baadaye, polisi walipofika kuulizia kama kuna majeruhi, mkulima akawaambia, hahhhaaa bwana mi nimewazika wote! akaulizwa hakuna majeruhi? akajibu kuna wengine walidai wameumia etc lakini wanasiasa ni waongo mi najua walikuwa wamekufa!!!!

Tambwe ni mmoja wa hao wanasiasa!

FD
 
Mzee Shughuli,

Bravo! Yes tunataka watu kama wewe kwenye forum, no question kuwa una uhakika na unachokisema, na I love the fact unaposema kuwa wewe mwenyewe personally umewahi kumsadia huyo Mzee Tambwe,

Hesima juu bro, na ubarikiwe Yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees!
 
Mwanakijiji tutafika tu ma-issue aliyoshusha mzeeshughuli bwana naona ndiko huko tunakoelekea. Nina wasiwasi na filgga anaweza akashinikizwa aifunge.
 
Mzee shughuli,

Nimeirudia posting so far kama mara kumi, I still can not get enough of it tafadhali mzee tuwekee mengine inaonekana una mengi,

tena I promise kuwa ukiyaongeza nitayaweka kwenye hilo hilo gazeti aliloandika huu upuuzi wake! Weka vitu mwanangu!
 
Bwana Tambwe kilicho muondoa NCCR wala haikuwa tofauti za siasa na Mzee wa Kiraracha bali ni tabia yake ya uongo kwenye Chama , makundi na uzinzi .Tambwe aliwamaliza wanawake wa NCCR. Tambwei alitupatia sana wasi wasi hasa kwa umri ule kutaka Siasa madaraka ya kisiasa lakini akawa na watoto hana mke .Nyumbani kwake yeye anaishi na watoto wake .

Tambwe ni mrogo wa maradaka na mpenda biashara chafu zote .Mimi leo akisema hakuna lolote upinzani namshangaa maana alikuwa huko miaka yote na hakuyaona haya .Nina imani na yeye kuamua kuaondoka Upinzani kwamba ni haki yake ya kikatiba na si zaidi ya hapo .Uozo hawezi kuuona leo huyu jamaa ni mnafiki mpenda madaraka .

Tambwe ukitaka habari zake fika kitu kinaitwa Kwa Zuru Natal Tandika pale muulize mtu mmoja anaitwa Shaban Ndambwe ama Jamal Warner pale Mtoni Mtongani watakueleza alivyo mbaya hata wa kupanga kuiba kura na kuhonga watu ili wafanye kampeni chafu.

CUF wana mchezo sawa na CCM wote wana Siasa za kuangamiza na ndiyo maana alikimbilia huko .Amehama vyama vingapi na sasa anaishia CCM? Huko mimi nasema mwacheni mtamsikia kawasha moto huko maana hakawii mtu wa majungu yule .Muulizeni kwa nini aliondolewa kugombea Ubunge NCCR mwaka 1995 akasaidiwa na nguvu ya Vijana Temeke. Ali forge vyeti na Elimu yake ni kidato cha 4 tu .Ana sifa zingine za ajabu mimi nakaa kimya na kama akijibu hii hoja basi nitammaliza atashangaa na CCM watamuona si mtu .Sijui huko atapewa kitu gani ila najua hawezi kuifanay CCM kuwa Ngome ya CCM mbele ya CUF maana yeye ni mafya na CUF n mafya zaidi yake ila ana mbinu za kuleta uharamia za CUF ambazo atawapa wana CCM kufanya uchaguzi hilo ni sawa ila atakuwa na wakati mgumu sana .
 
Yule mbunge machachari ambaye ilibakia kidogo tuwe na Tanganyika Njeru Kasaka yuko wapi sasa hivi?????
 
Yule mbunge machachari ambaye ilibakia kidogo tuwe na Tanganyika Njeru Kasaka yuko wapi sasa hivi?????

Mara ya mwisho nilimsikia wakati anahama vyama kati ya CCM, CUF na CHADEMA wakati wa kugombea Ubunge 2005
 
anaitwa Njelu Kasaka alikuwa mbunge wa Lupa huko Mbeya. alishindwa kura za maoni ndani ya CCM akahamia CUF lakini muda ulikuwa umeisha akawekewa pingamizi na akarudi tena CCM. hajulikani alipo
 
Back
Top Bottom