Karume1+karume2+karume3=ufalme?

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Jamani,ebu tafakarini hii,nimeinyofoa hapa;http://www.bongotz.com/bongoyetu02_23_08.htm

BALOZI KARUME SULUHISHO LA TATU ZANZIBAR

Na, Antar Sangali - Bagamoyo

Mwishoni mwa mwezi wa Januari mwaka 2008 Mtoto wa pili wa Rais wa Kwanza wa Visiwa vya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amaan Karume Balozi Ali Karume aliianika hadharani azma yake ya kuwania urais wa Zanzibar mwaka 2010.

MwanaCCM huyo ametamka kinagaubaga kwamba hafanyi kampeni hivi sasa bali anakusudia kuwania urasi mwaka 2010 kupitia chama chake na kwamba hana maskhara katika kukusudia kwake huko.


Balozi Karume mwanadiplomasia na mchumi aliyefuzu kitaaluma kutaja kwake nia ya kuutaka urais wa visiwa hivyo ndicho kiu kilichonishawishi niamue kuandika makala hii.

Lipo kundi la watu wenye mtazamo hasi wanaomuona na kumuhukumu bila ya hatia Balozi huyo katika mbio hizo za urais na kusema ni sawa nchi ya Zanzibar kuwa chini ya ufalme katika kubadilishana madaraka ya urais kwa kigezo cha ati kwanini “anatoka Amani na kuingia Ali”.

Kilichonisukuma kuandika makala hii ni mambo matatu,kwanza ni ukomavu wa Balozi Karume kidiplomasia na kisiasa, pili uthubutu wake katika kukabili uhalisi wa hali ya hewa ya kisiasa ya sasa visiwani humo na tatu uwezo binafsi alionao katika utambuzi wa turufu za siasa za Tanzania, Zanzibar, Afrika Mashariki, Afrika na Dunia kwa ujumla.

Tamko la Balozi Karume la kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ikiwa atashinda urais visiwani humo si kwamba linalenga kuzika hasama na utengano uliopo bali pia ni mpya na adimu sana katika vinywa vya wanasiasa wa Tanzania hususani toka kambi ya Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ni “piku” katika jozi ya karata za siasa na kwamba si rahisi kutamkwa na kiongozi asiye na uthubutu,uwezo na upembuzi wa mambo lakini pia haitamkwi kiwepesiwepesi na mwanasiasa butu asiyetambua miiko na mizungu ya diplomasia au ishara za mabadiliko katika siasa.

Kauli ya Balozi Karume ni mithili ya jawabu katika matatizo ya kudumu ya Zanzibar bila ya kutazama anayetamka ni mtoto kutoka nyumba ya Abeid Karume, Thabit Kombo, Mtoro Rehan Kingo, Salmin Amor, Aboud Jumbe au Abdallah Kassim Hanga. Ni kauli iliyobeba ujumbe hai katika siasa za Zanzibar.

kimsingi visiwa hivyo vinahitaji kiongozi mwenye fikra mpya, mikakati endelevu na utashi wa wazi katika kufuta matabaka kwa lengo la kuleta umoja kamili na maelewano ya kudumu miongoni mwa wazanzibar.

Swali la kwanini Balozi Ali awe mgombea wa urais wa Zanzibar mwaka 2010 akitaka kuingia badala ya Kakaye jawabu lake ni fupi, si Ali kama Ali, bali uwezo wa Ali na utashi mpya anaoukusudia ndiyo kigezo na pengine ni mtaji au ni tiketi yake kabla ya mchakato mzima wa kumpata mgombea kuanza ndani ya CCM.

Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliposema kuwa Rais wa Nchi yetu hataangaliwa kwamba anatoka kabila gani au dini ipi,inathibitisha pia kwamba ni mtazamo dhaifu kuitazama nyumba anayotoka Rais anayehitajiwa ima iwe ni yenye mnasaba wa uongozi au nyumba ya mtu asiye na umaarufu.

Uwezo wa Mzee Abeid Karume kiuongozi haukufanana kamwe na Dk. Kwame Nkurumah wa Ghana, na uwezo wa Jomo Kenyata wa Kenya pengine ulipishana sana na ule aliokuwa nao Julius Nyerere wa Tanganyika. Hapa nazungumzia zaidi uwezo katika uongozi bila ya kutazama kabila, amilia au dini ya kiongozi tunayetaka atuongoze.

Itapendeza sana ikiwa watajitokeza wagombea wengine zaidi katika kuwania urais wa Zanzibar mwaka 2010 kupitia CCM lakini wenye uthubutu na utashi wa wazi kama wa Balozi Ali katika kuitazama nchi hiyo na mikakati mipya aliyonayo.

Tuliwahi kumsikia Dk Salmin Amour Juma mwaka 1995 akisisitiza na kukataa kata kata kuunda serikali ya pamoja kwa kile alichodai hawezi kuchaganya mchele na kokoto kati ya CCM na CUF licha ya ushindi mwembamba alioupata.

Mwaka 1957 na 1963 tuliona jinsi Abeid Karume alivyoomba kuunganisha viti kati ya ASP na ZPPP lakini kiongozi wa ZPPP Mohamed Shamte alivyompiga chenga ya mwili 1963 na kukubali kuungana na ZNP cha Ali Muhsin Al Barwan na hatimaye yakazuka Mapinduzi ya damu Januari 12.1964.

Rais Jakaya Kikwete ni Rais pekee wa mfano Barani Afrika katika kukubali kama kuna matatizo na mitafaruku katika nchi yake na hatimaye kutafuta njia za utatuzi huku viongozi wengi Afrika wakiabudu vita na miifarakano.

Kuchaguzliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU) ni alama tosha ya kuanza kwake kuchukua uzoefu aliouanzisha Tanzania wa kuvikutanisha vyama vya CCM na CUF katika meza ya mazungumzo yanayoendelea.

Muafaka wa kwanza kati ya CCM na CUF ulisukumwa kwa juhudi za Jumuiya ya Madola chini ya Katibu Mkuu wake Chief Emeka Anyaok huku viongozi waliokuwepo katika madaraka wakikana kuwa hakukuwa "mgogoro wa kisiasa Zanziabar" baada ya uchaguzi wa 1995.

Rais Kikwete akiwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Tanzania aliweza kutofautiana kimawazo na Balozi Mohamed Ramiya aliyekuwa waziri katika serikali ya Dk Salmain katika mkutano ulioitwa wa kimataifa juu ya Demokrasia (International Conference on Democracy) ambao ulifanyika katika ukumbi wa Bwawani Zanzibar pale aliposimama na kutamka wazi wazi kuwa kuna mgogoro unaohitaji kupatiwa utatuzi na suluhu.

Dk. Salmin hakuota kuunda serikali ya pamoja, Rais Aman Karume ndiyo huyo anamaliza muda wake akiwa hana hata waziri toka chama chochote cha upinzani huko Zanzibar ilhali nchi hiyo ikiwa na joto kubwa lililotanda la upinzani.

Mitafaruku imetokea katika zama ya utawala wa Rais Dk Salmin na pia Karume akiwa madarakani na kupelekea kile kilichoitwa muafaka na leo yakiendelea mazungumzo yanayotafuta muafaka mwingine wa tatu wa visiwa hivyo.

Balozi Karume bila shaka ameanza kuona mbali kisiasa, kauli yake inajiwekea akiba pia katika siku za usoni hata kama atashindwa katika uchaguzi wa Urais, lakini Rais mstaarab toka chama kitakachoshinda ni wazi ataona soni na kuamua kumchagua Balozi Ali katika kuunda serikali ya pamoja huko Zanzibar.

Matokeo ya uchaguzi nchini Kenya na vurugu zinazoendelea huku watu wasio na hatia wakipoteza maisha ni fundisho katika nchi yetu na mustakabali mzima wa siasa katika kujenga umoja na dhima ya kuamsha maelewano ya kisiasa.

Nchini Ethiopia watu hubaguana kwa ukabila kati ya Amharic na Tigray, wasomali wanauana kwa thamani na utukufu wa koo zao, wakenya leo wanachomeana nyumba kwasababu zinazotajika licha ya wizi wa kura, lakini kujitokeza kwa Ukikuyu na Uluo na pia tumeona kadhia ya Utusi na Uhutu huko Rwanda na Burundi.

Kauli yenye nia ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar kwa mtazamo wangu mdogo naiona ni kama taa yenye mwanga katika kiza kinene cha taharuki na kutoaminiana miongoni mwa wazanzibar wenyewe.

Wajumbe wa halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM, Kamati Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ndiyo wenye maamuzi kisiasa nani awe mgombea kutokana na kwasababu zile zile za mchakato wa kidemokrasia.

Mabadiliko si lazima yasubiri mgombea na mshindi toka nje ya CCM, ndani ya CCM anaweza kujitokeza kiongozi mwenye kupenda kufanya mabadiko na ikawa ni sehemu ya mabadiliko hayo na kisha historia ikajiandika.

Mzee Ali Hassan Mwinyi alipoingia madarakani 1985 alifanya mabadiliko ya sera za kuichumi ikiwa ni pamoja na kukubaliana na matakwa au masharti ya IMF,sera ya soko huria na maboresho katika sura ya Azimio la Arusha. Maduka ya Ushirika yakafa, RTC, NMC na ile adha na adhabu ya kujipanga kwenye misururu mirefu toka alfajiri ikaondoka na leo imebaki kuwa ni historia kana kwamba hilo jambo halikuwapo nchini.

Kimsingi mimi simtazami tu Balozi Ali katika asili ndani ya nyumba ya Mzee Karume, bali navutiwa na uwezo wake, taaswira aliyonayo katika uga wa siasa ikisukumwa na utashi wake katika kufikia mabadiliko ya kudumu na ya pamoja huko Zanzibar.

Kumnyima nafasi au kumbeza kwasababu ati ni mdogo wake Rais Aman na kupuuzia uwezo wake ni sawa na kumyima haki au kumtia msiba wa nakama kwa kuzaliwa katika familia ya Mzee Karume.

Akiwekewa "kauzibe" mwaka 2010 kwa sababu ati yeye ni mtoto wa Mzee Karume hata akitaka tena kuwania urais mwaka 2020 ataambiwa vile vile kuwa Kaka yake Amaan aliwahi kuwa Rais na hivyo hana nafasi.

Zanzibar na hasa CCM kwa upande huo inahitaji kumpata mgombea shupavu, mwenye mvuto, mbinu na uhodari katika kujenga hoja na kujibu kwa nguvu ya hoja kwenye viriri vya kisiasa na kwenye jukwaa la jumuiya kimataifa.

Mnaochambua na kukosoa masuala ya siasa hebu itazameni kweli katika kina cha tafakuri yakinifu katika kuficha batili isiyobebwa na uzito wenye mantiki kamili katika kuziba ufa kabla ya kujenga ukuta.

Mungu ibariki Afrika.
 
Ni Uamuzi Wa Watu Wa Visiwani Kumpitisha Karume Mdogo Kama Mgombea Wao Na Kama Raisi Wao Wao Ndio Wanaompenda Na Kumwelewa Vizuri Kuliko Sisi Wenyewe

Kwahiyo Chochote Kikitokea Ni Hulka Na Utashi Wa Watu Wa Visiwani Na Huo Ndio Ukomavu Wa Democrasia

Mbona Kuna Bush Baba Na Bush Mtoto

Kuna Kina Kghandi , Butto Wote Hawa Huwataji Unarukia Karume
 
Hata mimi sioni sababu ya msingi ya huyu mtu kutopewa nafasi kama:-
  • Wazanzibar wenyewe wanamkubali na kuona anawafaa.
  • Hata kama familia yote watapokezana ilimradi process ya uchaguzi wa kidemocrasia imetimia, tatizo ni pale CCM watakapo iba kura ili kumuweka madarakani hata kama ameshindwa.
  • Kama anaendesha nchi kwa kufuata misingi ya sheria na kuiletea maendeleo nchi.

Kama wenyewe wanamtaka hapewe nafasi.
 
Waridi,
Mkuu kuna tatizo kubwa sana na hii imezungumzwa sana na nchi za magharibi hasa ukitaka kuisoma vizuri tafuta kitabu kinachoitwa - The Africans!
Mkuu kifupi NDIVYO TULIVYO.. hatukuona ubaya walipomrudisha Sultan baada ya Uchaguzi wa 1963 na wengi hadi leo wanampa support kubwa sana...Na hatuoni Ubaya kuwepo kwa kina Karume kama watawala walioandaliwa na chombo kinachoaminiwa... Kwani hata hao Masultan machief wetu walipitia mitihani ya kuchaguliwa na watu wao kabla ya kukabidhiwa nchi..
Hata hayo Mapinduzi pia yalikuwa kumwondoa Sultan kumweka Sultan (Chief) mweusi kwani nsio tafsiri ya Uhuru wa nchi zote za Kiafrika..Kutawaliwa na mweusi mwenzetu - Zimwi likujualo!
Tunatafuta nguvu ya kutawala kama walivyotawala Wazungu na Waarabu ili kuipata hadhi ambayo ilikuwa ndoto kubwa ya mtu mweusi (mtumwa) kufikia class hiyo.
Uhuru wa kweli haujapatikana Zanzibar, na bara ndio tumeshapotea ktk maze moja ambayo haina ufumbuzi..
Tunatawaliwa kama nchi nyinginezo za Kiafrika!..Hivyo basi ukoo wa Karume unaweza kutokuwa na jina la Usultan lakini sidhani kama kuna tofauti kubwa kwani wote wanapikwa kabla ya kukabidhiwa Utawala.
 
Ni Uamuzi Wa Watu Wa Visiwani Kumpitisha Karume Mdogo Kama Mgombea Wao Na Kama Raisi Wao Wao Ndio Wanaompenda Na Kumwelewa Vizuri Kuliko Sisi Wenyewe

Kwahiyo Chochote Kikitokea Ni Hulka Na Utashi Wa Watu Wa Visiwani Na Huo Ndio Ukomavu Wa Democrasia

Mbona Kuna Bush Baba Na Bush Mtoto

Kuna Kina Kghandi , Butto Wote Hawa Huwataji Unarukia Karume

Uamuzi unafanywa Dodoma nafikiri unakumbuka ya 2000.
 
Waridi,
Mkuu kuna tatizo kubwa sana na hii imezungumzwa sana na nchi za magharibi hasa ukitaka kuisoma vizuri tafuta kitabu kinachoitwa - The Africans!
Mkuu kifupi NDIVYO TULIVYO.. hatukuona ubaya walipomrudisha Sultan baada ya Uchaguzi wa 1963 na wengi hadi leo wanampa support kubwa sana...Na hatuoni Ubaya kuwepo kwa kina Karume kama watawala walioandaliwa na chombo kinachoaminiwa... Kwani hata hao Masultan machief wetu walipitia mitihani ya kuchaguliwa na watu wao kabla ya kukabidhiwa nchi..
Hata hayo Mapinduzi pia yalikuwa kumwondoa Sultan kumweka Sultan (Chief) mweusi kwani nsio tafsiri ya Uhuru wa nchi zote za Kiafrika..Kutawaliwa na mweusi mwenzetu - Zimwi likujualo!
Tunatafuta nguvu ya kutawala kama walivyotawala Wazungu na Waarabu ili kuipata hadhi ambayo ilikuwa ndoto kubwa ya mtu mweusi (mtumwa) kufikia class hiyo.
Uhuru wa kweli haujapatikana Zanzibar, na bara ndio tumeshapotea ktk maze moja ambayo haina ufumbuzi.. Tunatawaliwa kama nchi nyinginezo za Kiafrika!..Hivyo basi ukoo wa Karume unaweza kutokuwa na jina la Usultan lakini sidhani kama kuna tofauti kubwa kwani wote wanapikwa kabla ya kukabidhiwa Utawala.

Nakubaliana na wewe, Mkandara! Tatizo la Tanzania ni kukosekana kwa demokrasia ya kweli. Ndiyo, ni muhimu kuwa na multi party system lakini haitoshi, maana ni lazima wananchi waelewe ya kuwa kwa kupiga kura wana uwezo wa kubadili uongozi. Pia demokrasia ndani ya vyama vya siasa ni muhimu! Kwa hiyo safari ni ndefu. lakini tusikate tamaa. I believe in the ability of people to change and to bring about change(I am channeling Obama!)
 
Waridi,
Mkuu kuna tatizo kubwa sana na hii imezungumzwa sana na nchi za magharibi hasa ukitaka kuisoma vizuri tafuta kitabu kinachoitwa - The Africans!
Mkuu kifupi NDIVYO TULIVYO.. hatukuona ubaya walipomrudisha Sultan baada ya Uchaguzi wa 1963 na wengi hadi leo wanampa support kubwa sana...Na hatuoni Ubaya kuwepo kwa kina Karume kama watawala walioandaliwa na chombo kinachoaminiwa... Kwani hata hao Masultan machief wetu walipitia mitihani ya kuchaguliwa na watu wao kabla ya kukabidhiwa nchi..
Hata hayo Mapinduzi pia yalikuwa kumwondoa Sultan kumweka Sultan (Chief) mweusi kwani nsio tafsiri ya Uhuru wa nchi zote za Kiafrika..Kutawaliwa na mweusi mwenzetu - Zimwi likujualo!
Tunatafuta nguvu ya kutawala kama walivyotawala Wazungu na Waarabu ili kuipata hadhi ambayo ilikuwa ndoto kubwa ya mtu mweusi (mtumwa) kufikia class hiyo.
Uhuru wa kweli haujapatikana Zanzibar, na bara ndio tumeshapotea ktk maze moja ambayo haina ufumbuzi..
Tunatawaliwa kama nchi nyinginezo za Kiafrika!..Hivyo basi ukoo wa Karume unaweza kutokuwa na jina la Usultan lakini sidhani kama kuna tofauti kubwa kwani wote wanapikwa kabla ya kukabidhiwa Utawala.

Nakubaliana na wewe, sana tu, isipokuwa hayo maneno mekundu.
Kwa kuongezea, zipo mbinu nyingi kuhakikisha candidate wa Uraisi anakubalika/anachaguliwa na wapiga kura. Wapo watu Tanzania wasiojua mbele wala nyuma kuhusu mambo ya siasa na uongozi, ukiwawekea mtoto wa Nyerere against Henry Daffa ...guess who they'll pick!

I berg to differ with you on one thing man, na nitaendelea kulisema maana hili lipo kwenye fikra za wengi na sehemu kadhaa kwenye hii forum limejitokeza. Unaposema "Ndivyo tulivyo" una maanisha waTanzania au sio?
Wapo wanaotumia maneno "NDIVYO TULIVYO.." bila kuyatafakari.
Generalization kwa kutumia maneno hayo haitujengi. Kwa maoni yangu kusema NDIVYO TULIVYO sio sahihi!

Ukisema "Watanzania wengi ni waoga", huenda ukawa sahihi. Hata hivyo, I would encourage a more optimistic view of a situation.
 
Lazydog,
hapana mkuu mimi nitaendelea kuamini - NDIVYO TULIVYO kama motisha ya kunijenga umahiri wa kukabiriana na matatizo yetu..
Kama nilivyokwisha sema huko nyuma kukataa maradhi siku zote kutatuongezea madhara kwa sababu kamwe hatutaweza kutafuta chanzo cha maradhi hayo ila kumlalamikia Mungu na kujenga imani kuwa magonjwa yote yamewekwa na Mungu..
NDIVYO TULIVYO ni hoja inayotusukuma sote kuanza kujiuliza inakuwaje sisi tukubali kina Karume waendelee kujipanga kushika madaraka kama vile wao ni Masultan..Na kama utataka changes basi tuanze na hilo la Ndivyo tulivyo!..
Inakuwaje kweli leo hii Karume mdogo aanze kupikwa kuwa rais wa Zanzibar na wananchi wasiweze kuliona hili kuwa ni tatizo kubwa la demokrasia!..wanashindwa uchaguzi, yet bado wanaendelea kushika madaraka kama kina Mugabe na wananchi tupo nyuma yao kuwapa kila heshima ya Usultan wao?
Umezungumzia swala la mtoto wa Nyerere kugombea na kuwataja hao watu WASIOJUA MBELE wala NYUMA ambao watamchagua mtoto wa Nyerere.. Hao wasiojua ndio pamoja na sisi tutakao mpa kura asilimia 80..Kulingana na demokrasia kura asilimia 80 zinawakilisha taifa zima ktk demokrasia ya kweli na hivyo kukamilisha msemo wa NDIVYO TULIVYO.. Hutaki, then let's change that..now utaanzia wapi kuleta changes ikiwa hukubali ndivyo tulivyo!

Tanzania leo hii inaitwa nchi maskini na wapo watu kama wewe wanaoweza kusema semeni baadhi ya Watanzania ndio maskini lakini sio kila mtu ni maskini. The truth remain Tanzania is a poor country hata kama tunajitakia.. Kwa kuelewa umaskini wetu na kukubali umaskini wetu ni rahisi kuweza kutafuta mbinu za kuondoka ktk umaskini huu..Umaskini ni maradhi yanayotakiwa kuwa sio tu kuatfuta virusi vyake bali hata mugonjwa kukubali anaumwa na anahitaji tiba.
Tatizo kubwa la viongozi wetu ni moja kati ya kundi linalokataa kuwa Tanzania ni nchi maskini kwa sababu wao kama Haile Selassie hawana hali hiyo.
 
Ulipozungumzia swala la mtoto wa Karume mbona nilikuwa upande wako mzee!?
Nimetofautiana nawe kwenye hayo maneno mawili tu! Sio zaidi.

Update:
Nimetambua kwamba wapo wanaoafiki kauli ya NDIVYO TULIVYO
I don't get it, perhaps I'm missing something.
Sikuwa nimeona hii thread kabla, Check it out!

Nime-save kwenye flash ntakwenda isoma yote.
 
lazydog,
Nimetumia swala la Karume ili kusherehesha yale yaliyoyangulia maanake sikusema NDIVYO TULIVYO pasipo sababu..

Mkuu nadhani kweli una miss the point hapa pamoja na kuzungusha kwangu kote..Ila basi jiulize mwenyewe kwa nini sisi Waafrika tumeshindwa kwenda mbele?.. haiwezeknai kila nchi duniani hata Vietnam leo wanapuyanga!... Na kama alivyosema mwalimu Adui yetu mkubwa ni Umaskini unaotokana na Uzembe na Kupuuza - Je, how many out there wanakubaliana na hili!.. Ukinambia leo hii wewe Mkandara ni Mzembe na Mpuuzi tayari ni tusi kwa mtu mwuesi hata kama kuna ukweli. sawasawa na mtu mwenye Ukimwi ukimwambia una Ukimwi tayari umetukana na hawezi kuelewa kabisa sababu zote utakazo jaribu kusema..

Labda changes zinaweza tokeo tu pale mwenye elimu kama huyo ndugu yetu watakapoweza kuandika vitabu maanake huwezi fafanua diagnosis ya maradhi haya ya Ndivyo Tulivyo bila kuwa na Phd..
 
mambo mengi ni ya kutia shaka ktk siasa zetu za kibongo,mimi naona bora ya huyo kasema wazi kungali mapema ili wenyewe waone kama ana wafaa au la,kuna mwingine jana alikuwa mbunge wa Mkuranga na leo ni mbunge wa huko visiwani unadhani na yeye kafuata nini kule? Wapiga kura wetu ndio waamuzi,lakini kwa zanzibar anayehesabu kura ndiye mwamuzi.
 
Mtu wa Pwani,
Ukienda Chadema na kugombea kiti cha mwenyekiti kuna uwezekano mkubwa ukachukua nafasi hiyo kwa sababu Mbowe hakupikwa na mkwewe kumtayarisha kuongoza Chadema.
Pili, unaonyesha kuwa na mawazo mazito ambayo yanaganda ndani ya jokofu la CCM isipokuwa wewe huelewi rehma uliyojaaliwa.
Na kibaya zaidi Ufalme haupewi mtu wa nje ya kizazi cha Mtawala..tena basi umenikumbusha kitu kimoja hilo Baraza la Mapinduzi sio kundi la watu fulani wanaojiona wao kama wale wa Mugabe kuwa wao pekee ndio wenye haki zaidi Zanziibar kuliko watu wengine wote!
 
Katika viongozi wote TZ ni Ali Karume pekee alietamka kuwa, iwapo atachaguliwa kuwa Prez Zanzibar ataanzisha serikali ya Mseto. Alisema hayo hata kabla ya Makubaliano ya Muafaka kuwekwa hadharani.
 
Katika viongozi wote TZ ni Ali Karume pekee alietamka kuwa, iwapo atachaguliwa kuwa Prez Zanzibar ataanzisha serikali ya Mseto. Alisema hayo hata kabla ya Makubaliano ya Muafaka kuwekwa hadharani.

Mhn.....makubwa haya.....mungu tuweke tuyaone
 
Rais ajaye Zanzibar ni Bilal, huyo Karume anatumika kuwakatisha tamaa hopefuls wengine, ni technique ya kawaida tu inaitwa "crowding the deck", waliitumia pia bara wakishirikiana na kina Patric Chokala na John Shibuda kuwavuruga kina Sumaye na Malecela.
 
Mhn.....makubwa haya.....mungu tuweke tuyaone

Haya ni maneno ya Ali Karume

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama suluhisho pekee la kumaliza misuguano ya kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Ushauri huo umetolewa jana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Karume, alipozungumza na waandishi wa habari visiwani hapa. Alisema vyama vikuu vilivyopo Zanzibar ni CCM na CUF ambavyo vina nguvu sawa.

Alisema Zanzibar bila ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, hali ya migororo haitaweza kuepukika, kutokana na kuwa CCM kimejikita zaidi katika Kisiwa cha Unguja na CUF kuwa na ngome yake kisiwani Pemba.

Balozi Karume alisema serikali ya umoja wa kitaifa pia itamaliza mpasuko wa kisiasa uliopo hivi sasa, kwani nchi imeshindwa kuwa na maendeleo kutokana na migogoro ya kisiasa isiyokwisha visiwani.

“Watu wengi hawapendi kusema ukweli, lakini ndio ukweli wenyewe ….hali ya kisiasa iliyopo katika visiwa vyetu ni ngumu sana, Pemba CUF ina nguvu sana na CCM ina nguvu Unguja, sasa suluhisho la yote haya ni kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisisitiza mwanadiplomasia huyo.
 
Kama nimemsoma vizuri huyu Karume ana maana moja mbaya sana.. Yaani kuigawa Zanzibar ktk utawala wa serikali mbili kutokana na mgogoro wa visiwani wenyewe. Huu ni mfano wa Marekani walivoigawa Iraq ktk majimbo ya kiutawala kidini ili wapate kuwatawala hali imeongeza chuki zaidi ktk serikali kuu.
Hivyo basi nawausia Wazanzibar kuwa nia ya Karume ni chafu sana, haihusiani na Muungano wa nchi hizi mbili (bara na visiwani) ila utawala wa serikali ya visiwa vya Zanzibar..
Nafasi ya Zanzibar Kitaifa hakuizungumzia..na ndilo tatizo kubwa la wananchi wapiga kura wa visiwa hivyo sio swala la Uongozi wa visiwa hivi viwili..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom