Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 234
Bw. Karume anatoa taarifa kwa wanahabari kuwa Wapemba hawakumchagua ndio maana hakuwapanga katika wizara na sehemu nyengine nyeti za Serikali ya Zanzibar, Ivi nani anaushahidi kuwa Karume kachaguliwa na CCM zanzibar? Ivi si Mkapa nde aliemlazimisha kwa vitisho Dr. Ghraib Bilal kuachia ngazi? ambae ndie alikuwa chaguo la CCM Zanziabar! Sasa karume leo hii anasema utumbe kama ule haoni kuwa anawadhalilisha wazanzibari na kuwakejeli? Sasa kama wapemba hawakumchagua kwa nini haachani nao na kuwapa uhuru wao? Hii ndio demokrasia ya CCM? Wanakjidai kuwa eti! wameondoa wakoloni, Tanganyika leo hii si Mkoloni kwa Zanzibar? wakati nyerere ndie alietoa fikra za kuanzisha ASP na kupanga mapinduzi ya tar 12 Januari? Wakuja ndio waliofanya mauaji kwa Wasomi na wazanzibari wasio na hatia?
Vipi leo hii wapemba wasipewe haki yao ya kimaumbile kuchagua watakalo? Hata karafuu yao hawaruhusiwi kuuza watakapo, lakini watanganyika kule kila siku madege yanaruka na kutua kusafirisha samaki na pamba na mali za machimbo yao raha mustarehe. Sisi wazanzibari yaani hatujui kufanya biashara hizo, hatujui wapi tukauze biashara zetu? Ivi huu ndio usawa wa serikali ya Muungano? Hii ndio demokrasia ya CCM na Usawa kwa watanzania wote?
Jamani tuamkeni tujue nini tunahitaji na nini halitufai! Waachieni wapemba wachague wapi waende, Ndio! Visiwa vya Zanzibar havina historia ya kuungana, kwa hivyo ni rahisi kutengana kwa sababu hakuna mkataba wowote uliopo kama vimeungana. Kama havijaungana balaa inakuwa hivi mwasema haviwezi tengana je kama vimeungana kama Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ingekuwa Vipi? Si Balaa na nakama?