Karume na mabinti wa kiarabu Zanzibar

Rubabi

Senior Member
Nov 30, 2006
170
11
Nasikia Karume (original)alipokuwa raisi Zanzibar alilazimisha wasichana wa kiarabu kuolewa na waafrika?

Hivi ni kweli?

20050714-4_071405kj-0122jpg-3-515h.html
 
Karume was a forceful bully presiding over a mostly illiterate people in eager glee of tasting the hitherto mysterious arab flesh.Far from being a uniter, he was actually a human rights abuser and mass rape organizer.

There is evidence of rape and murder in the very Karume household.You can blame it on the Zeitgeist but I beg to differ.How this brutal dictator came to be hailed as a founding father of our nation and an East African statesman beats me.
 
Karume hakulazimisha! aliwataka wazazi wawape watoto uhuru wa kuoa na kuolewa na wawapendao. Waarabu hawakutaka mabinti wao waolewe na waafrika ilihali wanawapenda. Pia watanzania tufanye utafiti wa historia siyo kila kinachoandikwa ni sahihi. Karume hakuwa Dikteta! ila hakupenda watu wavivu. Ni kiongozi gani asiye dikteta kama anaongoza katika misingi na mapenzi ya nchi? Mfano kati ya Hitler na Bush nani dikteta? Tafakari!
 
karume alilazimisha watoto wa kiarabu kuolewa na yeye karume. ukitizama wake zake wote apart from Fatma Karume ambae ni mtoto wa ndoa ya nje wa Mhindi na mswahili, walobakia wote waarabu (wake zake wanafika 5).
na ushahidi wa kuwa alilazimisha ni kuwa alimuoa mwanamke mmoja Muarabu wa wete pemba, na akazaa nae mtoto anaeitwa AHADI KARUME. huyo mama wa ahadi baada ya karume kufa tu akakimbilia Oman na mwanawe Ahadi akikupa Business yake anajiita AHADI ALMISKIRI (kabila la mama yake) kuonyesha kuwa hakupenda kuzaliwa na karume kwa vile alilazimishwa.

pili, ilikuwa karume ni dictator usipokubali kumpa mwanao anakufunga au unapotea kwneye upeo wa dunia.

ni hayo tu machache

ahsanteni
 
Wakuu,

Inabidi tuwe tunafanza utafiti na kile tunachoandika kwani bila hivo basi kila kile tuandikacho kitakuwa kimekosa mwelekeo.

Ni wazi kabisa kwamba wenzangu wote tunaondika hapa kuhusu hayati Karume ama tunafanza makusudi kupotosha au bado tunakuwa hatufahamu kwa undani historia ya Zanzibar na matukio yaliyotokea kisiwani humo kabla na baada ya mapinduzi.

Lakini si taabu kwani ni vizuri kuwa na mjadala ambao labda baadae unaweza kutoa mwanga juu ya nini hasa mzee huyu alikifanza kabla na baada ya mapinduzi.

Zanziba kilikuwa ni kituo cha biashara ya utumwa na inajulikana wazi kwamba baada ya waarabu kutawala mahala pale mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, mwishowe walikuwa wanazaa na waafrika.

Kwa mtazamo wangu ni kwamba baada ya zahama na shida kubwa ya waafrika kuwa manamba na vibarua katika mashamba ya karafuu na kwamba hata baada ya mapinduzi waarabu kuonekana bado wameneemeka kwa majumba ardhi na fwedha, hayati Karume (kwa akili yake) aliona jambo hilo na kwa mtazamo wake akaona kwamba ni lazima pawe na usawa kwa kila kitu na hapo ndio mzozo ulipoanza.

Kwa hio kwa hatua hizo nzito za kuua watu, kufanza watu wapotee kusikojulikana, kulazimisha ndoa za waarabu na waafrika na kuwaandama wale ambao hawakuona kwamba mambo hayo yanastahiki kufanzwa, naona kwamba nnaweza kusema kwamba tuhuma zinazotolewa ni sahihi.
 
Mi naona mambo hayo hayakustahiki kufanywa na kwa mtizamo wako wa hapo juu, tuhuma zinazotolewa ni sahihi.

Hakuna kitu kinachoweza ku excuse kuua.
 
Wakuu,

Inabidi tuwe tunafanza utafiti na kile tunachoandika kwani bila hivo basi kila kile tuandikacho kitakuwa kimekosa mwelekeo.

Ni wazi kabisa kwamba wenzangu wote tunaondika hapa kuhusu hayati Karume ama tunafanza makusudi kupotosha au bado tunakuwa hatufahamu kwa undani historia ya Zanzibar na matukio yaliyotokea kisiwani humo kabla na baada ya mapinduzi.

Lakini si taabu kwani ni vizuri kuwa na mjadala ambao labda baadae unaweza kutoa mwanga juu ya nini hasa mzee huyu alikifanza kabla na baada ya mapinduzi.

Zanziba kilikuwa ni kituo cha biashara ya utumwa na inajulikana wazi kwamba baada ya waarabu kutawala mahala pale mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, mwishowe walikuwa wanazaa na waafrika.

Kwa mtazamo wangu ni kwamba baada ya zahama na shida kubwa ya waafrika kuwa manamba na vibarua katika mashamba ya karafuu na kwamba hata baada ya mapinduzi waarabu kuonekana bado wameneemeka kwa majumba ardhi na fwedha, hayati Karume (kwa akili yake) aliona jambo hilo na kwa mtazamo wake akaona kwamba ni lazima pawe na usawa kwa kila kitu na hapo ndio mzozo ulipoanza.

Kwa hio kwa hatua hizo nzito za kuua watu, kufanza watu wapotee kusikojulikana, kulazimisha ndoa za waarabu na waafrika na kuwaandama wale ambao hawakuona kwamba mambo hayo yanastahiki kufanzwa, naona kwamba nnaweza kusema kwamba tuhuma zinazotolewa ni sahihi.

Wakati ule madhali kulikuwepo na kambi kuu mbili zenye nguvu hapa duniani karume aliweza kufanya mauaji makubwa hata baada ya mapinduzi ya 1964 kwani kipindi kilichofuatia kilikuwa cha kuwalazimisha waarabu kuolewa na waafrika.Hili lilimpa shida sana Julius Nyerere lakini hata hivyo alifumba macho ili asimuudhi swahiba wake huyo katili mkubwa.

Hakuna ubaya wa kuona makabila kwa hiari kwani hata kabla ya ndoa hizo za maguvu kulikuwapo na waafrika wachache waliokuwa na wake wa kiarabu.Wote hawa walikuwa Waswahili ila tatizo ni kutumia mabavu.
Karume alivunja haki za binadamu na aliuawa si kwa ajili ya kuoa waarabu bali kwa kumuua mkwe wake Mwarabu na kisha kumdanganya shemeji yake kila alipokuwa akimuuliza kuhusu uhai wa baba yake.

Matokeo shemeji huyo Lt.Humud alimimima risasi na kuhakikisha anamwondoa uhai shemeji yake KARUME.
 
karume alilazimisha watoto wa kiarabu kuolewa na yeye karume. ukitizama wake zake wote apart from Fatma Karume ambae ni mtoto wa ndoa ya nje wa Mhindi na mswahili, walobakia wote waarabu (wake zake wanafika 5).
na ushahidi wa kuwa alilazimisha ni kuwa alimuoa mwanamke mmoja Muarabu wa wete pemba, na akazaa nae mtoto anaeitwa AHADI KARUME. huyo mama wa ahadi baada ya karume kufa tu akakimbilia Oman na mwanawe Ahadi akikupa Business yake anajiita AHADI ALMISKIRI (kabila la mama yake) kuonyesha kuwa hakupenda kuzaliwa na karume kwa vile alilazimishwa.

pili, ilikuwa karume ni dictator usipokubali kumpa mwanao anakufunga au unapotea kwneye upeo wa dunia.

ni hayo tu machache

ahsanteni
Kwamba ulitaka kusema Fatma Karume ni mtoto wa nje wa karume wa kwanza???!! Uliwapa tango pori og!
 
Usichanganye madawa mkuu. Kuna Fatma Karume mke wake Karume, Na kuna Fatma Karume Mjukuu wa kaeume ambaye ndie huyu tulonae sasahivi.
 
Hiyo story ina ukweli fulani. Nasikia alikuwa anasema kama wao walivyokuwa wanakula dada zetu na sisi ni zamu yetu.
 
Nadhani mzee karume hakutaka ubaguzi uendelee ktk jamii yake hivyo akaona njia nyingine ni kuwaruhusu watu kuoa race yoyote ile

pia ikumbukwe Zanzibar ilikuwa na asilimia nyingi tu ya waarabu hivyo isingekuwa vyema kuwaacha waarabu waendelee kukaa kivyao vyao huku umeshawaulia ndugu na jamaa zao ni hatari zaidi ilibidi iwe hivyo hakukuwa na namna nyingine kwa wakati huo..

Alafu vitu vingine tukubali tu (maarifa ya jana ni ujinga wa leo)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom