Karume na mabinti wa kiarabu Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karume na mabinti wa kiarabu Zanzibar

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Rubabi, Mar 14, 2008.

 1. R

  Rubabi Senior Member

  #1
  Mar 14, 2008
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasikia Karume (original)alipokuwa raisi Zanzibar alilazimisha wasichana wa kiarabu kuolewa na waafrika?

  Hivi ni kweli?

  [​IMG]
   
 2. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama alifanya hivyo, ninampongeza sana kwa maana alikuwa na dhana ya kuondoa Uafrika na uarabu, pia kuondoa ile hali ya baadhi ya watu kujiona kuwa wao ni watu wa 'class' ya juu kuliko wengine. Asingeliuwawa, leo wa-zenj wote wangekuwa wanafanana, hata upemba na u-unguja usingelikuwepo.
   
 3. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Baada ya kulazimisha watu kuolewa na watu wasiowataka alipata nini?
   
 4. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ah Balahau we. Hakulazimisha Bwana. Alishawishi.Baadhi ya wakaazi wakashawishika. Zikafanyika ndoa za mchanganyiko. Na faida yake tunaiona leo baada ya miaka hiyo 40 Tembelea Zanzibar. Matunda ya ndoa hizo wengine ni viongozi- Hawe Uarabu wao na Uafrika wao, HAWAYUMBI.
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  NDIO NI KWELI

  na namsifu kwa amri ile
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Karume was a forceful bully presiding over a mostly illiterate people in eager glee of tasting the hitherto mysterious arab flesh.Far from being a uniter, he was actually a human rights abuser and mass rape organizer.

  There is evidence of rape and murder in the very Karume household.You can blame it on the Zeitgeist but I beg to differ.How this brutal dictator came to be hailed as a founding father of our nation and an East African statesman beats me.
   
 7. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  There is a reason why he was assassinated.
   
 8. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  alipata KIFO
   
 9. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,670
  Likes Received: 2,468
  Trophy Points: 280
  Duh watu humu akili zenu zina majibu utafikiri yametengenezwa kwa kompyuta.

  Tit for tat, the brutal,merciless dictator and human rights abuser got what he deserved...death by the GUN...
   
 10. w

  wendos Member

  #10
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karume hakulazimisha! aliwataka wazazi wawape watoto uhuru wa kuoa na kuolewa na wawapendao. Waarabu hawakutaka mabinti wao waolewe na waafrika ilihali wanawapenda. Pia watanzania tufanye utafiti wa historia siyo kila kinachoandikwa ni sahihi. Karume hakuwa Dikteta! ila hakupenda watu wavivu. Ni kiongozi gani asiye dikteta kama anaongoza katika misingi na mapenzi ya nchi? Mfano kati ya Hitler na Bush nani dikteta? Tafakari!
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  karume alilazimisha watoto wa kiarabu kuolewa na yeye karume. ukitizama wake zake wote apart from Fatma Karume ambae ni mtoto wa ndoa ya nje wa Mhindi na mswahili, walobakia wote waarabu (wake zake wanafika 5).
  na ushahidi wa kuwa alilazimisha ni kuwa alimuoa mwanamke mmoja Muarabu wa wete pemba, na akazaa nae mtoto anaeitwa AHADI KARUME. huyo mama wa ahadi baada ya karume kufa tu akakimbilia Oman na mwanawe Ahadi akikupa Business yake anajiita AHADI ALMISKIRI (kabila la mama yake) kuonyesha kuwa hakupenda kuzaliwa na karume kwa vile alilazimishwa.

  pili, ilikuwa karume ni dictator usipokubali kumpa mwanao anakufunga au unapotea kwneye upeo wa dunia.

  ni hayo tu machache

  ahsanteni
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Inabidi tuwe tunafanza utafiti na kile tunachoandika kwani bila hivo basi kila kile tuandikacho kitakuwa kimekosa mwelekeo.

  Ni wazi kabisa kwamba wenzangu wote tunaondika hapa kuhusu hayati Karume ama tunafanza makusudi kupotosha au bado tunakuwa hatufahamu kwa undani historia ya Zanzibar na matukio yaliyotokea kisiwani humo kabla na baada ya mapinduzi.

  Lakini si taabu kwani ni vizuri kuwa na mjadala ambao labda baadae unaweza kutoa mwanga juu ya nini hasa mzee huyu alikifanza kabla na baada ya mapinduzi.

  Zanziba kilikuwa ni kituo cha biashara ya utumwa na inajulikana wazi kwamba baada ya waarabu kutawala mahala pale mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, mwishowe walikuwa wanazaa na waafrika.

  Kwa mtazamo wangu ni kwamba baada ya zahama na shida kubwa ya waafrika kuwa manamba na vibarua katika mashamba ya karafuu na kwamba hata baada ya mapinduzi waarabu kuonekana bado wameneemeka kwa majumba ardhi na fwedha, hayati Karume (kwa akili yake) aliona jambo hilo na kwa mtazamo wake akaona kwamba ni lazima pawe na usawa kwa kila kitu na hapo ndio mzozo ulipoanza.

  Kwa hio kwa hatua hizo nzito za kuua watu, kufanza watu wapotee kusikojulikana, kulazimisha ndoa za waarabu na waafrika na kuwaandama wale ambao hawakuona kwamba mambo hayo yanastahiki kufanzwa, naona kwamba nnaweza kusema kwamba tuhuma zinazotolewa ni sahihi.
   
 13. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mi naona mambo hayo hayakustahiki kufanywa na kwa mtizamo wako wa hapo juu, tuhuma zinazotolewa ni sahihi.

  Hakuna kitu kinachoweza ku excuse kuua.
   
 14. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wakati ule madhali kulikuwepo na kambi kuu mbili zenye nguvu hapa duniani karume aliweza kufanya mauaji makubwa hata baada ya mapinduzi ya 1964 kwani kipindi kilichofuatia kilikuwa cha kuwalazimisha waarabu kuolewa na waafrika.Hili lilimpa shida sana Julius Nyerere lakini hata hivyo alifumba macho ili asimuudhi swahiba wake huyo katili mkubwa.

  Hakuna ubaya wa kuona makabila kwa hiari kwani hata kabla ya ndoa hizo za maguvu kulikuwapo na waafrika wachache waliokuwa na wake wa kiarabu.Wote hawa walikuwa Waswahili ila tatizo ni kutumia mabavu.
  Karume alivunja haki za binadamu na aliuawa si kwa ajili ya kuoa waarabu bali kwa kumuua mkwe wake Mwarabu na kisha kumdanganya shemeji yake kila alipokuwa akimuuliza kuhusu uhai wa baba yake.

  Matokeo shemeji huyo Lt.Humud alimimima risasi na kuhakikisha anamwondoa uhai shemeji yake KARUME.
   
Loading...