Karume 'mpuuzi', lakini ukweli wake mchungu

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
TATHMINI YA MKUTANO MKUU WA CCM

Msomaji Raia | Raia Mwema Toleo la 270 | 28 Nov 2012

MAKALA hii itahitimisha tathmini yangu kuhusu Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM uliofanyika Dodoma tangu Novemba 11 hadi Novemba 14 mwaka huu.

Kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama dola, vimbwanga vyake huwa vinachanganya watu na kuamini kuwa kila baada ya Mkutano Mkuu, CCM huwa inazaliwa upya.

Imani hii imejengeka kutokana na ukweli kuwa, kabla ya Mkutano Mkuu, huwa kuna dalili za migawanyiko na mipango kadhaa ya makundi kutaka agenda zao zishinde.

Kutokana na udhibiti wa vyombo vya dola pamoja na ushabiki uliopitiliza, mipango hiyo huwa inakwama na kuwafanya watu wengi kuamini kuwa CCM ina wenyewe, na wenyewe hao huwa wanaifanya izaliwe upya kila baada ya Mkutano Mkuu!

Historia ya dhana hii ni ndefu, na wahanga (victims) wa mkakati huu kwa miaka ya karibuni ni Salmin Amour (Komandoo), Mzee John Malecela, Dk. Gharib Bilal, Samuel Sitta na sasa Edward Lowassa.

Kwa miaka ya nyuma wanakumbukwa Mzee Aboud Jumbe na Sharrif Hamad. Kwa sababu zilizo wazi, mkakati huu wa kuipa uhai mpya CCM huwa unawaathiri sana Wazanzibari kuliko Watanganyika.

Rais Karume na "upuuzi" wake

Kama Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake, rais mstaafu Amani Karume alikaribishwa kutoa nasaha zake siku ya kufunga mkutano. Alitoa hotuba, ambayo hivi sasa inaitwa ya kipuuzi huko Magogoni na mtaa wa Lumumba.

Hakuna aliyetarajia kuwa Karume angesema maneno aliyoyasema siku hiyo kiasi cha Mwenyekiti Jakaya Kikwete kukiri kuwa "hajawahi kumwona amefurahi kiasi hicho" kama alivyomwona siku hiyo.

Mara kadhaa hotuba yake ilikatishwa na watu waliomzomea na kumtaka amalize na kukaa. Hii ikakumbusha enzi za uenyekiti wa Benjamin Mkapa wakati wanamtandao wa Kikwete walipokuwa wakimzomea kila mtu aliyetaka kuhoji matumizi ya rushwa katika mkutano huo.

Mzee Joseph Butiku anaikumbuka hii na aliiandikia barua rasmi kwa Mwenyekiti Mkapa. Hii itukumbushe kuwa zomea zomea haikuanza na CHADEMA katika mikutano.

Alipozomewa sana, Rais Karume akawafananisha wazomeaji na vinywa vya samaki! Wapo waliodai, Rais Karume alikuwa kalewa sana konyagi siku hiyo. Awe alilewa au hakulewa; ni mpuuzi au si mpuuzi; kwangu mimi si habari. Habari muhimu ni yale aliyoyasema kwa dakika alizopewa.

Karume alizungumzia kadi yake ya ASP (Afro Shiraz Party); akaelezea madhumuni ya ASP; akamwuliza Dk. Shein ikiwa yeye anayo kadi yake ya ASP. Moja ya madhumuni ya ASP akakumbusha kuwa ni kulinda uhuru wa Zanzibar na watu wake. Ndipo akahoji wale wanaowazuia wenzao wasitoe maoni yao kuhusu Muungano.

Akamkumbusha Rais Kikwete kuwa alitoa ruhusa kila mtu aseme anachotaka wakati wa mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya. Akahoji iweje sasa wengine wanakamatwa kwa kutoa maoni yao. Karume akakumbusha jinsi CCM ilivyopoteza baadhi ya majimbo kwa sababu ya kupuuzia maoni ya wananchi. Akakumbusha suala la zamu kati ya mbunge na mwakilishi katika jimbo fulani. Wazomeaji hawakutaka kusikia haya wakamwimbia taarabu ya "uamsho uamsho".

Niseme wazi hata kama nilichoka nikakaa nje ya ukumbi wakati anaongea, Karume alisema mambo ya maana kuliko hotuba za masaa zilizotolewa na waheshimiwa wengine. Kwa muda mfupi, Karume aliuzodoa udikteta unaoabudiwa ndani ya CCM; alibainisha hatari zinazoukabili Muungano; alikumbusha habari za zamu za kuongoza nchi hii iliyotokana na nchi mbili; na zaidi sana alisema kutoka moyoni kuwa ASP haijafa kwa sababu waliokuwa wanachama wake wangali bado hai. CCM tumeze au tuteme, huo ndio ukweli kutoka kwa Karume, ambao sasa unaitwa ni upuuzi na akina Nape Nnauye.

Kulialia na kulalama kulizidi mno

Kwa siku tatu, Watanzania walishuhudia wajumbe zaidi ya 2000 wakilialia na kulalamika ndani ya ukumbi. Mwenyekiti alizindua uliaji huo na kupokewa na wajumbe kwenye vikao visivyo rasmi katika nyumba za kulala wageni na kwenye magari. Kivuli cha Chama cha Denokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliwatesa sana wajumbe na kuwafanya viongozi kupoteza mwelekeo na kuanza kutukana ovyo ovyo.

Haikutarajiwa kuwa Mwenyekiti naye angeingia katika mtego huo, pale alipojikuta anawatukana wapinzani na hasa CHADEMA kwa kuwaita "watu wazima ovyo", au pale ndani ya NEC alipojikuta anatumia muda mwingi kumpamba Nape Nnauye kwa kuwa anajua kutukanana na CHADEMA. Hata pale alipokumbushwa na rafiki yake kuwa kuitukana CHADEMA si lazima kuijenge CCM, yeye aliishia kusema "wamezidi acha Nape awashughulikie". Kazi inayomshinda yeye, anaona ni bora aifanye Nape. Kama Mzee Rashidi Kawawa alivyokuwa kwa Mwalimu, Nape ndivyo kwa Kikwete!

Mzee mkorofi kutoka Nyanda za Kusini alihoji, inakuwaje CHADEMA iwe tishio kwa CCM kuliko ufisadi na rushwa ulivyo tishio? CHADEMA inakuwaje tishio kuliko "unduguneizesheni" unaotafutiwa nafasi ya kutambuliwa kwenye katiba ya chama chetu?

Akasema, inakuwaje washauri wakuu wa Mwenyekiti wa chama chetu kuhusu masuala ya chama, si vikao bali ni wanausalama waliojaa fitina? Huyu naye alikuwa analalama sawa tu na wengi waliokuwa wanalalamika kwa siku tatu za mkutano.

Membe: Alimzamisha Mangula; Amemuibua tena.

Nafasi ya Bernard Membe kwa siasa za taifa hili kwa siku za usoni ilikuwa katika mtihani mgumu sana. Kambi ya rafiki yake wa zamani Edward Lowassa ilipania kumzamisha lakini akaokolewa na Kikwete na familia yake.

Kikwete alimsaidia kwa kubadili ratiba za upigaji kura, wakati familia yake (mkewe na mtoto wake) walihaha kila kona kumtafutia kura Bernard Membe. Taifa hili siku moja litadai kujua ukweli wa uhasama na urafiki wa watu hawa watatu – Membe, Kikwete na Lowassa. Jina Kikwete limekaa katikati kwa makusudi. Yeye ni ufunguo wa kitendawili hiki. Hili tuliache kwa sasa.

Mzee Philip Mangula, akaibuka ghafla kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara. Ni huyu huyu ambaye kundi la mtandao lililomwingiza Ikulu Kikwete lilidai alilitesa sana wakati wa kampeini na kuamua kumtosa mara baada ya Kikwete kuapishwa.

Yasemekana, Benard Membe, kachero mzoefu na kiini cha mikakati ya wana mtandao asilia, alimwambia Kikwete kuwa Mangula aliwapa taabu sana hivyo aondolewe kwenye nafasi ya ukatibu mkuu wa chama. Haikuishia hapo, Mzee Mangula alipojaribu kuibukia Iringa kama Mwenyekiti wa Mkoa alishughulikiwa vikali na kuangushwa na mtu asiyefanana na CCM kwa vigezo vyote.

Mzee Mangula alikiri baadaye kuwa ndani ya CCM uongozi uko mnadani na wapiga kura hawataki tena vipeperushi vya wagombea, bali wanataka "vipeperushwa". Mzee Mangula, kila anapokumbushwa harakati za wana mtandao, huwa anatania kuwa yeye aliponzwa na "faili maalumu".

Kuna habari kuwa Mzee Mangula kaibuka kwa mkono wa Membe. Kwamba, vikao kadhaa vilifanyika Makambako kati ya wawili hawa. Iwe kwa Membe kujituma au kutumwa, ni kwamba walikutana na agenda ilikuwa ni uchaguzi katika Mkutano Mkuu wa 8.

Aliombwa radhi au hakuombwa, hilo sasa si habari. Habari ni kuwa, Mkutano Mkuu umempitisha Mzee Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM lakini mshenga mkuu alikuwa Membe. Kama ushenga huu ulikuwa ni kwa manufaa ya chama au kwa manufaa ya mtandao wake anaouunda kwa ajili ya 2015, ni suala la wakati.

Ikiwa ni kweli, basi itakuwa vigumu kukemea mitandao ndani ya chama hiki kikongwe. Kama mtandao wa Membe ni halali, wa Lowassa hauwezi kuwa haramu. Kama Kikwete aliingia kwa mtandao, ni vigumu kuifikiria CCM na urais bila mtandao. Na tumejifunza kwa uchungu kuwa mtandao hauishii katika uchaguzi kwa sababu, baada ya mtu wao kuchaguliwa, kinachofuata ni kufaidi jasho na matunda ya kazi.

Kwa walioshindwa, kuna kazi ya kutathmini ni wapi wamekwama na kuazimia aluta continua. Ni ndoto kuambiana kuvunja makundi wakati anayeshinda na kuingia Ikulu anaendelea na kundi lake.

Jambo moja tu Mzee Mangula alizingatie. Membe anayedaiwa kumzamisha baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 mbele ya Kikwete, hawezi kugeuka leo na kumtetea kuwa ni mtu mzuri anayekifaa chama. Kwa nini hakufaa mwaka 2005 chini ya Mwenyekiti huyuhuyu? Membe ni yule yule, Mwenyekiti ni yule yule, chama ni kile kile na Mangula ni yule yule! Ni kitu gani kimebadilika kumfanya Mangula asiyefaa mwaka 2005, afae mwaka 2012?

Kinachoonekana lakini hakizumguziwi waziwazi, ni ukweli kuwa Kikwete na Membe wanamwona swahiba/hasimu wao Lowassa kuwa sasa ni zaidi ya mgombea urais wa CCM 2015. Kwao, Lowassa amegeuka kuwa chama; ameiteka CCM mbele ya macho yao na wanadhani Mangula atawasaidia kuiokomboa CCM iliyo mateka mikononi mwa Lowassa. Kikwete na Membe hawajiulizi ni kitu gani kimemjenga Lowassa na kumfanya kuiteka CCM.

Kitendo cha kumkimbilia aliyekuwa "adui" yao na chama chao kuwa aje kuwasaidia kukijenga chama walichokibomoa kwa mikono yao, hakieleweki. Wengi tulidhani, Mkutano Mkuu ungepata nafasi ya kutathmini hali hii, badala yake tukaambulia kulialia na vijembe visivyo na mpangilio. Tusubiri Mkutano Mkuu mwingine maalumu au ule wa 2017.
 
Umejitahidi kuandika but umenajisi maandishi yako kwa kumtaja Mzee Butiku alokuwa anatokwa na povu la njaa kila wiki ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere ,Jk alipompa ulaji wa Tume ya katiba Mpya pamoja na warioba na Salim sasa wamesahau rushwa,mtandao,ufisadi n.k that is why tunasema JK ni fundi wa siasa za kibongo bongo, Jk alimtumia Sitta na genge lake kumtoa Lowassa kwenye system na kuweka chaguo lake Pinda , Mkwerre huyu huyu akatumia genge la Lowassa kupitia kwa Andrew Chenge kumtoa Sitta na kuweka chagu lake Makinda sasa kwa style ile ile anamtumia Sitta na Lowassa kwa pamoja kuwang'oa wote ndo mana hakutaka Membe ang'oke mapema. JK anafata sera ya kimarekani ya No permanent Friends nor Enemies but permanet Interest, alipoingia wanamtandao walikuwa na nguvu sana wakajihisi wanaubia na Urais wake baada ya kujipanga wako wapi sasa Rostam, lowassa,Mzee Kingunge, Juma Akukweti,Sitta,Zakhia Meghji kawamwaga wote hawa akina membe walikuwa wapiga debe tu kwenye sekretariet ya wanamtandao hakujulikana, Misikiti,makanisa vyombo binafsi vya habari vimemuuza kwa nyakati tofauti yote kaipotezea? Haka katabia karithi toka kwa Nyerere mtu pekee aloanza nae na akamaliza nae japokuwa alimbania asiwe Rais ni Mzee Kawawa pekee ambae jk huyu membe ndo atakuwa kawawa Jr.
 
Imeshakuwa Novel au Historia ambayo huwezi itungia kitabu cha watoto wa Primary labda Tamthiliya ngoja nipite naisubiri Januari 2013, tutasikia majina ya CC kutoka kwa huyo Msomaji wa Raia
 
Umejitahidi kuandika but umenajisi maandishi yako kwa kumtaja Mzee Butiku alokuwa anatokwa na povu la njaa kila wiki ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere ,Jk alipompa ulaji wa Tume ya katiba Mpya pamoja na warioba na Salim sasa wamesahau rushwa,mtandao,ufisadi n.k that is why tunasema JK ni fundi wa siasa za kibongo bongo, Jk alimtumia Sitta na genge lake kumtoa Lowassa kwenye system na kuweka chaguo lake Pinda , Mkwerre huyu huyu akatumia genge la Lowassa kupitia kwa Andrew Chenge kumtoa Sitta na kuweka chagu lake Makinda sasa kwa style ile ile anamtumia Sitta na Lowassa kwa pamoja kuwang'oa wote ndo mana hakutaka Membe ang'oke mapema. JK anafata sera ya kimarekani ya No permanent Friends nor Enemies but permanet Interest, alipoingia wanamtandao walikuwa na nguvu sana wakajihisi wanaubia na Urais wake baada ya kujipanga wako wapi sasa Rostam, lowassa,Mzee Kingunge, Juma Akukweti,Sitta,Zakhia Meghji kawamwaga wote hawa akina membe walikuwa wapiga debe tu kwenye sekretariet ya wanamtandao hakujulikana, Misikiti,makanisa vyombo binafsi vya habari vimemuuza kwa nyakati tofauti yote kaipotezea? Haka katabia karithi toka kwa Nyerere mtu pekee aloanza nae na akamaliza nae japokuwa alimbania asiwe Rais ni Mzee Kawawa pekee ambae jk huyu membe ndo atakuwa kawawa Jr.

na wasi wasi na uwezo wako wa kuchambua hoja
 
Mie naona kama Karume kweli ni mpuuzi na siyo "mpuuzi" kwa vile alipokuwa madarakani akilindwa na kufadhiliwa na CCM hakuwa na ubavu wa kuyasema aliyosema. Kwanini ayaseme sasa? Angalia unafiki wa akina Karume. Leo kwa mfano maalim Seif amenyamaza akipigia makofi kila upuuzi wa CCM. Kesho akitemwa aanze kutema cheche tumuamini? Kuhusu zengwe la magamba hilo nakubaliana nalo. Ila la Karume kuwa mpuuzi asiyempuuzi sikubaliani nalo. Ni mpuuzi kweli anayepaswa kupuuziwa hata kama asemayo yana mashiko. Hana tofauti na Sumaye kulialia dhidi ya rushwa wakati alipokuwa madarakani hakufanya hivyo. Hata Lowassa na usongo wake wa ajira kwa vijana ni yale yale.
 
Ndio maana mimi nilisha baini mapema kuwa wewe songoro lazima utakuwa ni mtoto wa dhaifu au ndugu wa karibu. lakini kumbuka baada ya 2015 atamhitaji Lowassa sana kumlinda asiende jela maana amechezea sana fedha za watanzania kusafiri nchi za nje bila sababu za msingi, huo ni ufisadi mamboleo.mahakama inamsubiri.
 
Wewe FATHER OF ALL naona ulisoma shule za kikweli, maana kila mchango wako huwa unanifurahisha sana.una gonga mlemle!safi sana.
 
Ndio maana mimi nilisha baini mapema kuwa wewe songoro lazima utakuwa ni mtoto wa dhaifu au ndugu wa karibu. lakini kumbuka baada ya 2015 atamhitaji Lowassa sana kumlinda asiende jela maana amechezea sana fedha za watanzania kusafiri nchi za nje bila sababu za msingi, huo ni ufisadi mamboleo.mahakama inamsubiri.

Wewe bila ya shaka utakuwa mtoto wa yule mzinifu mpora wake za watu, kama umenipa udugu na jk kwa kumsifia vipi mwenyekiti wako alomsifia hadharani tupe utabiri nae ni nani wake? jaribu kujiuliza kwa nini siku hizi maandamano na migomo huisikii, umeshasikia kauli kali za maaskof kumshambulia jk kama walivyokuwa wanafanya? Kwa nini hufuati ushauri wa mwenyekiti wako alosema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hakuna kama jk, hujiulizi kwa nini leo hakuna mwenye ujasiri wa kusema hadharan hamtambui jk kama mlivyofanya baada ya uchaguzi 2010? Tafuta majibu utajuwa kwa nini tunasema Jk ni kungwi wa siasa za kibongo bongo!!
 
hapa watu wanacho jaribu kufanya ni kujitofautisha mwenye akili na asiye nazo. hawamfukuzi mwendawazimu aliye chukua nguo zao wakati wanaoga maana watu werevu watashindwa kutofautisha yupi ni yupi. essentially kama mtu anaambiwa umezidisha safari na hawezi kubaini hilo utaendelea kushauri? hapana, tumekosea wacha muda uamue kwani ni hapo 2015 tu anaondoka iwe isiwe.
 
Umejitahidi kuandika but umenajisi maandishi yako kwa kumtaja Mzee Butiku alokuwa anatokwa na povu la njaa kila wiki ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere ,Jk alipompa ulaji wa Tume ya katiba Mpya pamoja na warioba na Salim sasa wamesahau rushwa,mtandao,ufisadi n.k that is why tunasema JK ni fundi wa siasa za kibongo bongo, Jk alimtumia Sitta na genge lake kumtoa Lowassa kwenye system na kuweka chaguo lake Pinda , Mkwerre huyu huyu akatumia genge la Lowassa kupitia kwa Andrew Chenge kumtoa Sitta na kuweka chagu lake Makinda sasa kwa style ile ile anamtumia Sitta na Lowassa kwa pamoja kuwang'oa wote ndo mana hakutaka Membe ang'oke mapema. JK anafata sera ya kimarekani ya No permanent Friends nor Enemies but permanet Interest, alipoingia wanamtandao walikuwa na nguvu sana wakajihisi wanaubia na Urais wake baada ya kujipanga wako wapi sasa Rostam, lowassa,Mzee Kingunge, Juma Akukweti,Sitta,Zakhia Meghji kawamwaga wote hawa akina membe walikuwa wapiga debe tu kwenye sekretariet ya wanamtandao hakujulikana, Misikiti,makanisa vyombo binafsi vya habari vimemuuza kwa nyakati tofauti yote kaipotezea? Haka katabia karithi toka kwa Nyerere mtu pekee aloanza nae na akamaliza nae japokuwa alimbania asiwe Rais ni Mzee Kawawa pekee ambae jk huyu membe ndo atakuwa kawawa Jr.
mkuu nimeipenda sana comment yako pengine kuliko comment nyingi zilizowahi tokea humu. real I liked it.
 
Hotuba ya Rais mstaafu wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Zanzibar, Dk. Amani Karume, ambayo iliwaudhi baadhi ya watu lakini naamini ujumbe wake mzito uliosimama kwenye ukweli utakuja kukumbukwa na hao hao si miaka mingi kutoka sasa.
By: Ismail Jussa
 
He didnt mince a word, he said it as it is, he said the truth- yes truth! Only truth will set us free.
 
Attach hiyo hotuba tuione basi.

ALIYEKUWA Rais wa Zanzibar, Amani Abeid
Karume ametoa kauli
ambayo inaonekana
kukinzana na msimamo
wa chama chake na Serikali kuhusu hali ya
kisiasa Visiwani. Akiwaaga wana CCM wenzake baada ya
kustaafu nafasi ya Makamu Mwenyekiti
Tanzania Zanzibar juzi mjini hapa, Karume
alitoa hotuba yenye kuonesha msimamo wa
kutaka wanaotaka Muungano usio wa
Serikali mbili na wanaochochea vurugu, wasikilizwe na waachwe kuitwa majina ya
ajabu. Katika siku za karibuni, Zanzibar imekumbwa
na vurugu na fujo zinazodaiwa kufanywa na
Jumuiya ya Mihadhara maarufu kama Uamsho
na pia kumeibuka wanasiasa ndani ya CCM
wanaotaka Muungano wa Mkataba, kinyume
cha sera ya chama hicho inayotambua Muungano wa serikali mbili. Lakini juzi Karume mbele ya wana CCM zaidi
ya 2,000 kwenye Ukumbi wa Kizota, bila
kuwataja majina, alisema vurugu za Zanzibar
zinafanywa na wanaharakati na siyo
wanasiasa. Karume alikwenda mbali zaidi na kuwataka
wanachama wenzake kutokuwa na
wasiwasi na kitu walichokiunda wenyewe,
akimaanisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa
inayoundwa na CCM na Chama cha Wananchi
(CUF). Hakuishia hapo, akazungumzia maoni kuhusu
mfumo wa Muungano na kueleza, “Maneno
maneno madogo ya nini? Kila kitu kimo
katika Katiba. Wanatoa maoni yao,
tuvumiliane, nongwa ya nini sasa,” alisema
Karume. Katika hotuba yake ambayo wakati
mwingine alijikuta katika majibizano na
wajumbe wa mkutano huo, Rais huyo
mstaafu wa Zanzibar alitaka watu hao wenye
msimamo tofauti waache kuitwa majina ya
ajabu. Alisema majina hayo yanajulikana na yeye
hakuwa na sababu ya kuyataja. “Acheni
kuwaita majina ya ajabu. Halafu mnasema
ninyi ni ASP (chama kilichoungana na TANU
kuunda CCM), ASP gani?” Alihoji Karume
ambaye wakati wa hotuba yake alionesha kadi yake ya ASP aliyojiunga nayo mwaka
1970, kuonesha kuwa ni mwanachama wa
muda mrefu wa vyama hivyo. “Msiwatishe watu, fuateni Katiba kila mtu
anao uhuru wa kutoa maoni yake,” alisema
huku akiwaasa vijana kwamba wao ndio
wanaotakiwa kutumia hekima na busara
katika kuhakikisha chama hicho tawala
kinasonga mbele. Alihoji pia suala la kurudishwa kwa usultani
visiwani na kueleza kwamba hilo ni kitu
kisichowezekana kwa sababu Sultani
mwenyewe amekwishafariki dunia. Alisisitiza suala la kuvumiliana katika kutoa
maoni na mambo mengine, na ilifika mahali
wajumbe wa mkutano huo wakashindwa
uvumilivu kwake kutokana na kutumia muda
mwingi kutoa hotuba na pia pengine
kutokana na msimamo wake katika vurugu na siasa za sasa za Zanzibar.
Chanzo: Habarileo
 
Ahsnante mkuu. Ila hz ndio siasa za ccm. Hawapendi kusikia tofauti na wanachokitaka au kukiamini wao. Ila nmependa amefunguka vzr na sasa yuko huru.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom