TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Tumsifu Yesu Kristu na Asalaam alaykum ndugu zangu, sote tunafahamu siku ya leo ni kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha hayati Abeid Aman Karume.
Masikitiko yangu yapo hapo kwenye "kumbukumbu" kwani asilimia kubwa ya watanzania wamejijengea tamaduni ya kuziita 'sikukuu' yaani kutofanya kazi na kurelax kwao ni sikukuu. Inanisikitisha sana kwani idadi kubwa sana ya wananchi hawaijui historia ya nchi yao, siku kama ya leo ya kumbukumbu ingekuwa ni siku nzuri ya kujifunza kwa kina kuhusu kiongozi huyu na faida aliyoileta mpaka anafariki. Siku kama ya Nyerere watu huita sikukuu pia, tujenge tamaduni ya kujifunza kutoka kwa viongozi wetu waliokwishatangulia ili tujifunze uzalendo kutoka kwao kama hayati Abeid Aman Karume, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hayati Sokoine na wengine ili kwa pamoja tukaijenge nchi yetu kwa utashi...
Niwatakie siku njema ya kujifunza na kujitathmini kwa mapana zaidi.
Mtenga Gerald