Karume ataka kumjua aliyempigia KURA YA HAPANA

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Naona baada ya vitimbi vya kura za CCM vitimbi vingine lazima hufuatia. Tafadhali soma zaidi hapa chini:

Karume amsaka aliyemnyima kura amkaribishe Ikulu

Na Salma Said, Zanzibar

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Visiwani, Amani Abeid Karume amesema anatamani kumfahamu mtu aliyempigia kura ya hapana kwenye uchaguzi kiti hicho wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

karume.jpg


Alisema anatamani kumfahamu mtu aliyempigia kura ya hapan na ikiwezekana amualike Ikulu, ili anywe naye chai na kufahamu kwa nini alimpigia kura ya hapana ili kama kuna mambo anayoyafanya ambayo hakupaliani nayo aweze kuyarekebisha.


Hata hivyo, Karume alisema wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu huo kuliibuka kundi la baadhi ya watu waliokuwa wakieneza siasa chafu dhidi ya wenziwao.


Karume alisema hayo�jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja wa Kisiwandui baada ya kupokewa na wanachama wa CCM wa mikoa mitatu ya Unguja akitokea Dodoma alikochaguliwa tena kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.


Alisema kwamba kundi hilo aliloliita la 'machepe' liliubuka Zanzibar zikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi na kuwapa wasi wasi wazee wa CCM na baadhi ya Mawaziri wake waliokuwa wakiwania nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho.


�Alisema kundi hilo lilitengeneza orodha maalumu ya wagombea wanaotakiwa washinde na wanaotakiwa kuangushwa katika uchaguzi huo na kwamba kutokana na hali hiyo wazee wa CCM walikutana naye na kumueleza hali hiyo, lakini aliwataka waondoe wasi wasi kwa vile mambo waliyokuwa wakiyafaya yalikuwa nje ya utamaduni wa chama hicho.


"Machepe waliandika orodha ambayo walitaka kuitumia katika uchaguzi huo wakati utamaduni huo ni mgeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi na walishindwa vibaya na wengine waliondoka alfajiri baada ya kusikia mambo ni mabaya kwao," alisema Karume.


Hata hivyo, alisema sasa uchaguzi umekwisha hivyo makundi yameisha na kazi moja iliyop mbele yao ni kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.


Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya chama hicho, kuliibuka makundi yanayojiandaa kuwania nafasi za urais 2010 na kila kundi lilikuwa likihangaika idadi kubwa ya wajumbe wa NEC na kusababisha kuibuka makundi mawili makubwa moja likiwa upande wa Rais Mstaafu wa SMZ Salmin Amour na lingine kwa Rais Karume.


Hata hivyo, mawaziri watatu waliangushwa ambao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir na Naibu Waziri wa Kilimo, Khatib Suleiman.


Alisema ushindi alioupata ni mkubwa hivyo atahakikisha wanautumia katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kuwataka viongozi waliochaguliwa wafanye kazi ya kusimamia na kutekeleza Ilani ya uchaguzi kwa bidii.


Rais Karume alisema hivi sasa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameanza kuwaelewa (CCM) kufuatia kauli yake ya kueneza umoja na mshikamano kwa Wazanzibari.

�

Naye Makamu wa Rais Dk Mohammed Shein alisema CCM Zanzibar itaendele akushinda milele kutokana na kazi kubwa walioifanya viongozi wake wakati wa uchaguzi.


Katika hatua nyingine, Waandishi Wetu kutoka Mwanza wanaripoti kuwa Mjumbe wa NEc, Christopher Mwita Ghachuma amepokewa na maandamano makubwa jijini hapa na kukiri ushindani ulikuwa mkubwe kutokana na kushughulikiwa kila kona .


Mjumbe huyo alipokewa jana na wanachama mbalimbali waliokuwa na magari zaidi ya 100, pikipiki zaidi 50 huku mabango ya kumpongeza yakiwa yamebandikwa kila mahali jijini hapa.


Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza majira ya saa 3.30 asubuhijana, msururu wa magari uliondoka uwanjani hapo kuelekea katika Kiwanda cha Coca Cola Cha Nyanza.


Akizungumza kiwandani hapo, Ghachuma alisema kuwa nafasi aliyokuwa ikiiwania ilikuwa mgumu kwa kuwa ilikuwa inagombewa na watu wengi, huku baadhi yao wakiwa maafisa wa ngazi za juu serikalini wakiwemo mawaziri.


Alisema kutokana na hali hiyo, hakuwa anategemea kuchaguliwa, lakini anaamini kwamba maombi ya wanachma waliokuwa wanamuunga mkono yalimsaidia kuchaguliwa.


"Ukweli ushindani ulikuwa ni mkali na hata wale ambao hawakuchaguliwa ni kura tu hazikutosha, mie mwenyewe nilikuwa naomba Mungu sana nikawa nasema hata kama nisipokuwa kwenye 10 bora niwe hata wa 18 kati ya watu 20 ili mradi niwemo.

Source link: Mwananchi.

---Je, sasa hivi nikipindi cha kutafutana na kujua wabaya wao?!


SteveD.
 
"Alisema anatamani kumfahamu mtu aliyempigia kura ya hapana na ikiwezekana amualike Ikulu, ili anywe naye chai na kufahamu kwa nini alimpigia kura ya hapana ili kama kuna mambo anayoyafanya ambayo hakupaliani nayo aweze kuyarekebisha."

Mkuu SteveD,

Heshima mbele, lakini this is very sad kwa demokrasia yetu, maana ni clear kuwa mkuu angependa kuwa Sultani Kipingo, yaani ni lazima achaguliwe kwa kura zote, hawa ndio viongozi wetu na haya ndio mawazo yao,

Hebu imagine just for once kungekuwa na mpinzani kwenye hicho kinyang'anyiro? Huyu amesahau kuwa kwenye uchaguzi wa urais alishindwa na Dr. Billali, then hakushangaa kuona Bilali akiondolewa na kupewa yeye aliyeshindwa, ila anashangaaa sasa kukosa kura moja tu!

Kweli hili taifa tuna safari ndefu sana mbele yetu kisiasa iwapo kiongozi wa nafasi kubwa kama ya huyu mkuu, anapoweza kusema haya mbele ya public ila hata ya aibu!
 
FM ES, hakika kabisa mkuu... naona usemi 'kura ni siri yako' hauna maana tena pahala pengine utumikapo!!

SteveD.
 
Kunywa naye chai isije ikawa na maana ya panga kukata koo kama enzi za babake.

Kwanini apoteze muda kumsaka mtu mmoja? Ushindi ni ushindi tu hata kama ni wa aslimia 40.

Madikteta utayaona mambo yao tu, yanataka ushindi wa asilimia 100. Hata watu waliotoka familia moja hawawezi kupatana wote, kwanini hawa wakuu wanataka wana CCM wote wawapigie kura za ndiyo?
 
Hawa ndio viongozi wetu,kwa kauli zao tu unapata picha ni watu wa namna gani. Wakati sisi tuko kwenye dunia hii,wao wako dunia nyingine kabisa kimawazo.
 
Nina wasi wasi kama kweli alipingwa kwa kura moja tu, hizo ni mbwembwe huenda alipingwa kwa kura lukuki ila ndo hivo wanataka sifa tuuuuu!!!

Demokrasia ndani ya CCM huwa haipo siku zote hata Baba wa taifa hilo naye lilimshinda kwa mara ya kwanza Maalimu alipo mbwaga Komandoo ikabidi aingilie demokrasia!
 
Sikutegemea haya! No wonder Zanzibar hapatulii, hivi ni jambo la kuongelea mbele ya watu, mbona huwaiti waliokukosesha zaidi ya 40% ya kura za uraisi unywe nao chai?
 
Ndugu Yangu Kitila,

Si unajua CHADEMA ndio chama mbadala,,, hivi mna mikakati gani? ya kujiimarisha kule Tanzania Visiwani?

Unajua napata shida sana kuona kwamba only CCM na CUF ndio wenye strong presence Tanzania visiwani,,, huwezi jua mkiwa na at least 10-20% ya Kura visiwa vile vyaweza tulia!!!

Nisaidie ndugu yangu kwa mikakati iliyopo, usisahau kusema mna wanachama na viongozi wa kutosha kule au vipi? na je ni kwa visiwa vyote au Unguja tu?
 
Huo ni udikteta. Kwa nini anataka kuhoji demokrasia? Kila mtu ana haki ya kuamua vile atakavyo bila kukiuka katiba ya nchi. Aliyempigia kura ya hapana naye alitumia demokrasia yake, sasa kwa nini atafutwe?. Karume aangalie alipojikwaa, sio alipoangukia.
Kamwe asikae akafikiri kuwa anapendwa na kila mtu, sio kweli. Hakuna mwanadamu anayependwa na kila mtu hapa duniani.
Asitafute mchawi.
 
KILITIME,

Tunahitaji ndugu yangu kujikita huko Zanzibar. Bado jazi ni kubwa lakini tunajitahidi. Hapa nilipo sina hizo takwimu za wanachama wangapi tunao huku Zanzibar. hata hivyo sisi CHADEMA ni watatu, yaani baada ya CUF, CCM halafu sisi.
 
@SteveD,

Mwambieni karume aache kuchemka!!! Majibu anayo!!! Kwa kumsaidia tu ni Dr.Gharib Bilali. Haya amuite huko ikulu wanywe kahawa na tende.
 
KILITIME,

Mbona huulizi CUF bara, Hata huko Visiwani CCM wenyewe kila mwaka wanakula mzinga tu.
Mambo ya vyama ni hiari kuchagua waende chama gani.Hizo sheria sizizo na kichwa wala miguu za kulazimisha eti mpaka upate wadhamini Zanzibar ndo uonekane chama cha siasa zina walakini.
 
hawa waheshimiwa wanaisi kils wafanyaro wako right 100% ata izo alizozipata hana budi kumshukuru Mungu,uendwe na watu wote umekuwa pesa aaaahhh!ajifunze kukubaliana na no!
 
Hilo suala la kutaka kunywa nae chai anakuchoreni tu! Anywe chai na nani? Pengine anamtafuta ili akamsute, amng'ong'e na kumwambia "yakhe, kiko wapi?"
 
wakuu, heshima mbele, mimi nilidhani usultani umeisha zanzibar kumbe bado, sasa kwa nini tuendelee kuwa na muungano wakuu, kama kuna watawala wanaodhani kuwa nkupigiwa kura ya hapana ni ajabu? hao si wanatamani watawale kama masultani wakuu, na hapo ni nchi ya Tanzania, inayodai kuwa na 'demokrasia' ya vyama vingi?
 
Hilo suala la kutaka kunywa nae chai anakuchoreni tu! Anywe chai na nani? Pengine anamtafuta ili akamsute, amng'ong'e na kumwambia "yakhe, kiko wapi?"

Na ukizingatia alishasema kuwa zile silaha za mwaka 64 zipo bado ni kiasi cha kuzitia mafuta tu!
 
wakuu, heshima mbele, mimi nilidhani usultani umeisha zanzibar kumbe bado, sasa kwa nini tuendelee kuwa na muungano wakuu, kama kuna watawala wanaodhani kuwa nkupigiwa kura ya hapana ni ajabu? hao si wanatamani watawale kama masultani wakuu, na hapo ni nchi ya Tanzania, inayodai kuwa na 'demokrasia' ya vyama vingi?


Kuna hoja ya muungano inaendelea mahali fulani katika JF, naomba ingia na uchangie mawazo yako.
 
Kitila,
hebu naomba unisaidie zaidi, hivi mlipata kura ngapi? au asilimia ngapi kule Tanzania visiwani? kwenye uchaguzi wa 2005?
 
Haya jamani hayo ni mambo ya wanasiasa,atasema alikuwa Dr Gharibu Bilal au Salmin Amour au.... Tunatakiwa tukubali kuwa kama binaadamu hatukubaliki kwa asilimia mia moja.Wapo wanao tukubali na wanao tukataa.
Kama kweli akiambiwa kile ambacho alimpigia kura ya hapana kinamchukiza ataweza kutekeleza kweli au mambo ya majukwaani tu.
Ashukuru kupata hizo kura chache.Mambo yanabadilika itafikia wakti atapata ata kura mia za hapana.
Ahsanten
 
KILITIME,

labda wamtume Mwanakijiji na wamstation huko visiwani akaimarishe CHADEMA maana hapa JF watu washamstukia !
(ila sijui ataingia kwa gia gani kule)
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom