Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,403
- 1,241
Naona baada ya vitimbi vya kura za CCM vitimbi vingine lazima hufuatia. Tafadhali soma zaidi hapa chini:
---Je, sasa hivi nikipindi cha kutafutana na kujua wabaya wao?!
SteveD.
Source link: Mwananchi.Karume amsaka aliyemnyima kura amkaribishe Ikulu
Na Salma Said, Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Visiwani, Amani Abeid Karume amesema anatamani kumfahamu mtu aliyempigia kura ya hapana kwenye uchaguzi kiti hicho wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
![]()
Alisema anatamani kumfahamu mtu aliyempigia kura ya hapan na ikiwezekana amualike Ikulu, ili anywe naye chai na kufahamu kwa nini alimpigia kura ya hapana ili kama kuna mambo anayoyafanya ambayo hakupaliani nayo aweze kuyarekebisha.
Hata hivyo, Karume alisema wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu huo kuliibuka kundi la baadhi ya watu waliokuwa wakieneza siasa chafu dhidi ya wenziwao.
Karume alisema hayo�jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja wa Kisiwandui baada ya kupokewa na wanachama wa CCM wa mikoa mitatu ya Unguja akitokea Dodoma alikochaguliwa tena kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Alisema kwamba kundi hilo aliloliita la 'machepe' liliubuka Zanzibar zikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi na kuwapa wasi wasi wazee wa CCM na baadhi ya Mawaziri wake waliokuwa wakiwania nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho.
�Alisema kundi hilo lilitengeneza orodha maalumu ya wagombea wanaotakiwa washinde na wanaotakiwa kuangushwa katika uchaguzi huo na kwamba kutokana na hali hiyo wazee wa CCM walikutana naye na kumueleza hali hiyo, lakini aliwataka waondoe wasi wasi kwa vile mambo waliyokuwa wakiyafaya yalikuwa nje ya utamaduni wa chama hicho.
"Machepe waliandika orodha ambayo walitaka kuitumia katika uchaguzi huo wakati utamaduni huo ni mgeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi na walishindwa vibaya na wengine waliondoka alfajiri baada ya kusikia mambo ni mabaya kwao," alisema Karume.
Hata hivyo, alisema sasa uchaguzi umekwisha hivyo makundi yameisha na kazi moja iliyop mbele yao ni kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya chama hicho, kuliibuka makundi yanayojiandaa kuwania nafasi za urais 2010 na kila kundi lilikuwa likihangaika idadi kubwa ya wajumbe wa NEC na kusababisha kuibuka makundi mawili makubwa moja likiwa upande wa Rais Mstaafu wa SMZ Salmin Amour na lingine kwa Rais Karume.
Hata hivyo, mawaziri watatu waliangushwa ambao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir na Naibu Waziri wa Kilimo, Khatib Suleiman.
Alisema ushindi alioupata ni mkubwa hivyo atahakikisha wanautumia katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kuwataka viongozi waliochaguliwa wafanye kazi ya kusimamia na kutekeleza Ilani ya uchaguzi kwa bidii.
Rais Karume alisema hivi sasa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameanza kuwaelewa (CCM) kufuatia kauli yake ya kueneza umoja na mshikamano kwa Wazanzibari.
�
Naye Makamu wa Rais Dk Mohammed Shein alisema CCM Zanzibar itaendele akushinda milele kutokana na kazi kubwa walioifanya viongozi wake wakati wa uchaguzi.
Katika hatua nyingine, Waandishi Wetu kutoka Mwanza wanaripoti kuwa Mjumbe wa NEc, Christopher Mwita Ghachuma amepokewa na maandamano makubwa jijini hapa na kukiri ushindani ulikuwa mkubwe kutokana na kushughulikiwa kila kona .
Mjumbe huyo alipokewa jana na wanachama mbalimbali waliokuwa na magari zaidi ya 100, pikipiki zaidi 50 huku mabango ya kumpongeza yakiwa yamebandikwa kila mahali jijini hapa.
Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza majira ya saa 3.30 asubuhijana, msururu wa magari uliondoka uwanjani hapo kuelekea katika Kiwanda cha Coca Cola Cha Nyanza.
Akizungumza kiwandani hapo, Ghachuma alisema kuwa nafasi aliyokuwa ikiiwania ilikuwa mgumu kwa kuwa ilikuwa inagombewa na watu wengi, huku baadhi yao wakiwa maafisa wa ngazi za juu serikalini wakiwemo mawaziri.
Alisema kutokana na hali hiyo, hakuwa anategemea kuchaguliwa, lakini anaamini kwamba maombi ya wanachma waliokuwa wanamuunga mkono yalimsaidia kuchaguliwa.
"Ukweli ushindani ulikuwa ni mkali na hata wale ambao hawakuchaguliwa ni kura tu hazikutosha, mie mwenyewe nilikuwa naomba Mungu sana nikawa nasema hata kama nisipokuwa kwenye 10 bora niwe hata wa 18 kati ya watu 20 ili mradi niwemo.
---Je, sasa hivi nikipindi cha kutafutana na kujua wabaya wao?!
SteveD.