Karume alia mbele ya Kikwete

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Karume alia mbele ya Kikwete

NA Saed Kubenea.

Rais wa Zanzibar Aman Abeid Karume, alilia katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijijini Butiama wakati akipinga kuwepo Serikali ya pamoja kati ya chama chake na Chama Cha Wananchi (CUF).

Akiongea kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Karume alisema muafaka utaua historia na hasa juhudi za baba yake Abeid Aman Karume za kuasisi mapinduzi visiwani.

Hii ilikuwa wakati wa kujadili hoja ya kuunda serikali ya pamoja kati ya CCM na CUF kufuatia mapendekezo ya Rais Jakaya Kikwete ya kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

Karume ni mmoja wa wachangiaji katika vikao vya Butiama ambao walilia sana, kushawishi na kutoa tahadhari kuwa muafaka wa kuunda Serikali ya pamoja na CUF utaua maana halisi ya mapinduzi Zanzibar.

"Mnataka kuvunja historia" amesema mpasha habariakimnukuu Karume "baba yangu alipigania jambo hili (mapinduzi) na alikufa kwa kupigania jambo hili. Kukubali CUF kuingia serikalini, mnataka kufuta historia" alimnukuu Karume akisema.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya vikao zinasema, kilio cha Karume kilikuwa mwanzo wa vilio vingine vya wajumbe wa Zanzibar ambao, mmoja baada ya mwingine, walieleza wasiwasi wa kupoteza jina "Serikali ya MApinduzi Zanzibar SMZ"

Ni Karume, ambaye kwa kutumia ujanja na nafasi yake, alipenyeza hija ya kura ya maoni katika taarifa ya Kamati ya Rais Kikwete hata kabla haijawasilishwa katika kamati kuu (CC)

Hoja ya Karume ilikuwa ni pamoja na kutaka ushirika serikalini, kama utakuja iwe baada ya uchaguzi wa 2010 jambo ambalo tayari CUF wamelikataa kwa kishindo.

Kutokana na ushawishi wa Karume wajumbe watatu wa kamati ya Rais upande wa CCM ambao ni Yusuph Makamba, Kingunge Ngombale-Mwiru ana Ali Ameir Mohamed, walipenyeza mawazo ya kura ya maoni bila kujadiliwa ndani ya kamati ya pamoja.

Chozi la Karume katika CC ndilop linasadikiwa kumlainisha Rais na Mwenyekiti Kikwete, kusahaulisha ahadi yake na huenda kumbadilisha mawazo kuhusu umuhimu wa kumaliza hara mpasuko Zanzibar.

Kikubwa zaidi ambacho wajumbe walililia ni "kupoteza madaraka" Visiwani. Wengi waliona kushiriki kwa CUF katika utawala kutaweka chama hicho karibu na ushindi na hatimaye kukumba madaraka na kuizamisha CCM.

Mjumbe mmoja alikaririwa akiloloma "kulikoni?kuna nini ndani ya CCM? Viongozi wetu mmetufikisha wapi?Utaratibu wetu unasema bwana, ninyi (CUF) hamna chenu"

Mjumbe huyo ambaye ametajwa kuwa Mustapha Ahmada wa Kaskazini Ungua, alihoji "Tunajadili nini hapa?Mnaturudisha nyuma, Wapinzani Zanzibar hawana wanachotambua; kwao mapinduzi ni haramu, ... mnatupeleka wapi?"

Alisema "wanatuita wahafidhina, mahafidhina. Watasema ... tumeishawaweza. Leo sisi CCM, haki ya Mungu na Mtume, hatutashika tena madaraka Zanzibar" akimaanisha iwapo CUF watashiriki utawala.

Kwa sauti ya juu na kuhema, Ahmada alisema "Wafahamu (CUF) kuwa hatuko tayari. Kama mmeshachoka (akiamanisha Viongozi wa CCM) acheni turudi na ASP Zanzibar".

ASP - Afro- Shiraz Party - ndicho chama kilichoungana na Tanganyika African Union (TANU) kuunda CCM 5 February 1977.

Mjumbe mwingine kuchangia hoja ya kuwa serikali shirikishi Zanzibar alisema kwa kuwa CCM pamoja na kura ya maoni, sharti CUF wakubali masharti kadhaa.

Aliyataja mashari hayo kuwa ni kutamka hadharani kwamba wanautambua uchaguzi mkuu wa 2005 kuwa ulikuwa halali, kwamba wanatambua kuwa Rais kuwa aliyeko madarakani Zanzibar ni halali na amechaguliwa kihalali.

Mjumbe huyo akichangia hoja ya kuweka uwanja linganifu wa kisiasa Pemba alisema "Na Pemba ukiwapa uhuru wa mambo hayo, haki ya Mungu CCM itashindwa mwaka 2010. Hatuponi"

Hata hivyo mjumbe huyo baada ya kutoa uwanja sawa na CUF kukiri na kutambua serikali , kamati ya mazungumzo ya CCM ipeleke mapendekezo yake katika Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar kabla ya kufikishwa kwenye CC.

KAtka suti ya ushwasishina kuonyesha wasiwasi, mjumbe huyo alisema, "Bila kufuata haya, sisi wenyewe CCM tutakuwa tumejisokota"

Akigeukia wajumbe wote na kukazia macho kwa Mwenyekiti, alisema "Mnatuacha wenzetu" manatuacha! Leo Sief(Shariff Hamad) huyuhuyu, ambaye hataki mapinduzi, mnakaa naye eti kuridhisha wafadhili?Mimi sikubali hili. Mapinduziiiiiiiii.

Hoja ya kuwa serikali ya pamoja ilizua ubishi wa chinichini na hatimaye mlipiko wa ubishi na kung'aka kwa baadhi ya wajube.

Hali hiyo ilianzia kwa Kingunge Ngombale-Mwiru alipoanza kutoa mapendekezo aliyoyaita ya kamati ya Rais ambayo yalikuwa tayari amefanyiwa marekebisho na CC.

Ilikuwa pale wajumbe walipoanzisha zogo na kumkatisha Kingunge mara kadhaa, Kikwete aliingilia kati ili kurejesha utulivu.

Akijaribu kuwatuliza wajumbe Kikwete alisema tayari mapendekezo ya kamati yake yamefanyiwa kazi sana na CC na kuongeza kuwa hata nafasi ya makamu wa pili wa Rais mbaye ni msimamizi wa shughuli za serikali atatoka katika chama cha Rais.

Wakati kamati ya Rais ilipendekeza chama kilichopata ushindi wa pili kitoe Waziri Kiongozi(msimamizi wa serikali) CC ilipeleka NEC pendekezo la kuwa na makamu wawili wa rais.
Kwa kuzingatia hoja ya "Kuipiku" CUF, Kikwete alisema pendekezo la CC linataka makamu wa pili wa Rais ndie awe msimamizi wa shughuli za serikali huyo atatoka chama alichotooka Rais na ndie atachukua nafasi ya Rais wakati Rais hayupo.

Alifafanua kuwa idadi ya mawaziri kwa kila chama itazingatia uwiano na viti vya baraza la wawakilishi.
Katika hali ya sasa ambapo CCM ndiocho chama kilichotoa Rais ,kama kungekuwa na Serikali ya pamoja basi makamu wa kwanza wa Rais ambaye anatoka CUF angekuwa "picha tu" Hana majukumu yanayoeleweka.

Mchangiaji Mwanamke alitahadharisha CCM kuwa wakishindwa watapigwa mawe alisema "Mmmeaa mmejadili yote haya, mnasema ni mambo mazuri Haya!LAkini tusije tukapigwa mawe njiani"

Tarehe 30 December 2005, Rais Kikwete aliahidi Watanzania na Dunia kwamba atamaliza "pasuko wa kisiasa Zanzibar"

Kamati yake imekutana mara 21 ndani ya miezi 14 na kutumia karibu shilingi billioni 2 kwa kazi ambayo kutokana na mapendekezo ya Butiama ndio kwanza immeanza upya.

NAyo CUF imeitisha maandamano nchi nzima kupinga kuwepo mapendekezo mapya ambayo yanatibua kazi nzima na kufanya mabilioni ya fedha za umma na wafadhili yaliyotumika kuwa kama yamechomwa moto.

Maandamano ya CUF yataanzia Zanzibar Jumamosi ijayo ambako kumbukumbu za mauaji ya Januari 26 na 27 2001 zingali hai.

Source: Mwanahalisi

Eng Mohamed UPO???? Watu wanalia wanaona muafaka kuiingiza CUF maslahi yao yatakuwa hatarini soma kwa kituo kisha tafakari. Tunajua mpo wengi humu mnapewa pesa zetu tunazokatwa kwenye kodi kupunguza speed lakini hamtaweza kamwe Aluta.....

Sokomoko.
 
Makanjanja hao kwa kuflip flop utawaweza.

Ukisoma between the lines utaona kama hayo ni mapishi
 
Hivi Karume alikufa katika mapinduzi ama baad ya mapinduzi ? Ina maana sasa zanzibar itakuwa mali ya ukoo wa karume? Vipi Ali Karume anaye advocate Muafaka na power sharing yeye Baba yake ni mtofauti na baba yake huyu wa madarakani ?
 
Akiongea kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Karume alisema muafaka utaua historia na hasa juhudi za baba yake Abeid Aman Karume za kuasisi mapinduzi visiwani.

Hivi zanzibar kumbe inaongozwa kwa juhudi za mtu mmoja??? Hata kama hayo mapinduzi yamepitwa na wakati???

Hivi ana maana gani anaposema muafaka utaua historia ya mapinduzi??? Ina maana mapinduzi ni kukandamiza demokrasia upande wa pemba???

Karume alia mbele ya Kikwete

Mjumbe mmoja alikaririwa akiloloma "kulikoni?kuna nini ndani ya CCM? Viongozi wetu mmetufikisha wapi?Utaratibu wetu unasema bwana, ninyi (CUF) hamna chenu"

Mjumbe huyo ambaye ametajwa kuwa Mustapha Ahmada wa Kaskazini Ungua, alihoji "Tunajadili nini hapa?Mnaturudisha nyuma, Wapinzani Zanzibar hawana wanachotambua; kwao mapinduzi ni haramu, ... mnatupeleka wapi?"

Alisema "wanatuita wahafidhina, mahafidhina. Watasema ... tumeishawaweza. Leo sisi CCM, haki ya Mungu na Mtume, hatutashika tena madaraka Zanzibar" akimaanisha iwapo CUF watashiriki utawala.

Sasa kama CCM wanataka kutawala milele huko zanzibar, kuna haja gani ya kuruhusu vyama vya kisiasa na kufanya uchaguzi??? Kwa nini SMZ isitamke waziwazi kuwa zanzibar ni nchi ya chama kimoja???
 
makanjanja hao kwa kuflip flop utawaweza.

ukisoma between the lines utaona kama hayo ni mapishi

Haki ya Mungu makanjanja wanawakosesheni usingizi CCM na vibaraka wake. Hivi nyie watu hamuoni hata aibu? hivi kweli kuna mtu anaweza kuzuia Tsunami? basi JF na wanaJF wenye kupembua mambo wenye kuchuja mambo ni kama Tsunami mnatuogopa na bado tunasema na tutaendelea kusema kila ovu na kila zuri litakalo semwa hatupo hapa kuwakwaza au kukebehi yanayofanywa na serikali kama ikifanya mazuri tutawapa 5 wakikosea tutawasema! uhuru tunao! haki tunayo na nia pia tunayo ya kuijenga TZ yenye watu wa kuuliza mambo sio watu wa kufanywa mazezeta.

Ahsante sana mtu wa pwani umetimiza post 2000 kwa kupost vitu visivyo useful kwenye JF TUNAJUA MPO WENGI ILA JUENI SISI HATUNUNULIKI KWANI WE DONT HAVE PRICE TAGS. NA HUWEZI JUA KATI YETU SISI NDIO TUNAOFAIDIKA NA CCM KUSHINDA NYIE MTUMWAO HUMU NDANI! ILA TUMECHOKA TUNASOMA ALAMA ZA NYAKATI.
ALUTA........
SOKOMOKO.

NB:
MTU WA PWANI KWA MATAZAMO WANGU WEWE BEI ULIONUNULIWA HAIZIDI YA SIGARA NYOTA!
 
Swahiba pole kama huna price tag maana uko chini ya sigara nyota.

Ila ukweli ambao unatakiwa kuutambua kuwa hio habari imepikwa twna sana ww ukisoma kwa umakini kama ulivyomta eng mohamaed utaona kuwa kuna mengi mapishi.

Simaanishi kuwa ccm zanzibar hawakupinga lkn si kwa lugha iliotumiwa kwenye makala uliotuletea
 
Karume ni mmoja wa wachangiaji katika vikao vya Butiama ambao walilia sana, kushawishi na kutoa tahadhari kuwa muafaka wa kuunda Serikali ya pamoja na CUF utaua maana halisi ya mapinduzi Zanzibar.

"Mnataka kuvunja historia" amesema mpasha habariakimnukuu Karume "baba yangu alipigania jambo hili (mapinduzi) na alikufa kwa kupigania jambo hili. Kukubali CUF kuingia serikalini, mnataka kufuta historia" alimnukuu Karume akisema.

Hoja ya Karume ilikuwa ni pamoja na kutaka ushirika serikalini, kama utakuja iwe baada ya uchaguzi wa 2010 jambo ambalo tayari CUF wamelikataa kwa kishindo.

karume acha kuchezea amani Zanzibar, upo wakati utalia ile kikweli kweli, acha uroho.

Historia ya Zanzibar haijasemwa iwe ni ya chama kimoja au iwe in ya mambo yaliyopita pekee. Historia ni baina ya mambo yaliyopita, ya sasa na hata yajayo; hii ndiyo maana halisi ya historia mkuu.

Unataka iwe 2010 kwa sababu utakuwa umemaliza awamu yako siyo? ili ajaye akutane na CUF siyo? OK na kama CUF watashinda huo utaratibu wa ku-share madaraka uendelee tu? Hapana, you must be with a big problem in your head mkuu.
 
swahiba pole kama huna price tag maana uko chini ya sigara nyota.

ila ukweli ambao unatakiwa kuutambua kuwa hio habari imepikwa twna sana ww ukisoma kwa umakini kama ulivyomta eng mohamaed utaona kuwa kuna mengi mapishi.

simaanishi kuwa ccm zanzibar hawakupinga lkn si kwa lugha iliotumiwa kwenye makala uliotuletea

1.Sina price tag kwasababu utu wangu haununuliwi!
2.Nashukuru kwa kusema kuwa habari imepikwa ila mie jukumu langu kuwapa habari wenzangu kwani katiba ya nchi yangu japo kandamizi imeainisha haki hiyo! Na kwa taarifa yako ule mkutano nusu uvunjike!hawa CCM znz sio watu wazuri hawa.
3.Nimefurahi kusadikisha kuwa CCM Zanzibar walikataa lakini umesema sio kwa lugha hiyo tunaomba utuambie lugha waliyoitoa mie naliamini sana MwanaHalisi na waandishi wake kina Saed Kubenea japo mnawaita makanjanja lakini mie kwangu ni heros.
 
karume acha kuchezea amani Zanzibar, upo wakati utalia ile kikweli kweli, acha uroho.

Historia ya Zanzibar haijasemwa iwe ni ya chama kimoja au iwe in ya mambo yaliyopita pekee. Historia ni baina ya mambo yaliyopita, ya sasa na hata yajayo; hii ndiyo maana halisi ya historia mkuu.

Unataka iwe 2010 kwa sababu utakuwa umemaliza awamu yako siyo? ili ajaye akutane na CUF siyo? OK na kama CUF watashinda huo utaratibu wa ku-share madaraka uendelee tu? Hapana, you must be with a big problem in your head mkuu.

Wanataka kuifanya zanzibar shamba lao angalia Thread ya "Ukistaajabu ya Edward Lowasa utayaona ya Karume" wanataka akitoka mtoto wa Karume aje mtoto wa Mwinyi then Mahamoud Thabit Kombo anajiandaa pengine akimaliza mtoto wa Mwinyi ataingia Mahamoud Thabit Kombo the watoto wa kina Ally Ameir nawao wataingia basi yaani hii Zanzibar wao ndio wanahati miliki wengine hawaruhusiwi!

Thanks mkuu kwa kuliona hilo.
 
umekusudia mwaka huu ufikishe posts ngapi?manake naona yayo kwa yayo tu wayarejea.
 
Sasa hamtaki kujibiwa munataka museme nyinyi tu
nini maana ya hii forum? jaribuni kuwa wastaarabu kidogo.

Hawa ndivyo walivyo ila wajue hakuna lenye mwanzo likakosa m wisho na mwisho wao umekaribia!!!
 
umekusudia mwaka huu ufikishe posts ngapi?manake naona yayo kwa yayo tu wayarejea.

Angalia mie nina reason out wewe unapost swali dogo tu na linakuwa counted as a post hilo swali linakuhusu zaidi wewe mie nakusudia kutoa habari na kusoma yale nisiyojua kwani JF ni darasa tosha. Ahsanteni sana mashushu na hongereni ila nina wasiwasi kama m taweza kuuzima moto wa JF kazi mnayo!

All in all "KARUME ALIA MBELE YA KIKWETE" thats the topic kama unaweza changia laa huwezi bora uvute uradi.
 
Wazungu wanaiita 'emotional blackmail', lakini mara kwa mara hufanywa na wanawake!

ingependeza kama ungesema kuwa hiyo 'emotional blackmail' ni kwa baadhi ya wanawake though naheshimu mawazo yako na nakubaliana na wewe kuwa emotional blackmail baadhi ya watu na hasa watoto wanaitumia sana.
 
Wazungu wanaiita 'emotional blackmail', lakini mara kwa mara hufanywa na wanawake!

Na wewe ulichokifanya wazungu wanakiita misogyny. Mimi nakupinga wewe, na nawapinga Wazungu kwamba ni chuki ya Wanawake. Nakiita unafiki, kwa sababu nahakika unampenda Mama yako.

Nimeapa kupigana na ubaguzi wa aina zote!
 
Ndugu Kuhani Mkuu:
Fahamu kuwa Asili haibadiliki; labda kitokee kitu ambacho kinaitwa kwa Kimombo "Mutation".
 
Wahenga walisema bora "busara" kuliko "akili"!

Karume, kulia mbele za watu tena kwa jambo lisilokuwa na sababu ya kulia hiyo ni kukosa "busara", amejaribu kutumia akili kuliko busara. Sidhani kama Karume alikuwa na uchungu huo, mpaka kulia!
 
Karume alia mbele ya Kikwete

NA Saed Kubenea.

Rais wa Zanzibar Aman Abeid Karume, alilia katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijijini Butiama wakati akipinga kuwepo Serikali ya pamoja kati ya chama chake na Chama Cha Wananchi (CUF).

Akiongea kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Karume alisema muafaka utaua historia na hasa juhudi za baba yake Abeid Aman Karume za kuasisi mapinduzi visiwani.

Hii ilikuwa wakati wa kujadili hoja ya kuunda serikali ya pamoja kati ya CCM na CUF kufuatia mapendekezo ya Rais Jakaya Kikwete ya kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

Karume ni mmoja wa wachangiaji katika vikao vya Butiama ambao walilia sana, kushawishi na kutoa tahadhari kuwa muafaka wa kuunda Serikali ya pamoja na CUF utaua maana halisi ya mapinduzi Zanzibar.

"Mnataka kuvunja historia" amesema mpasha habariakimnukuu Karume "baba yangu alipigania jambo hili (mapinduzi) na alikufa kwa kupigania jambo hili. Kukubali CUF kuingia serikalini, mnataka kufuta historia" alimnukuu Karume akisema.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya vikao zinasema, kilio cha Karume kilikuwa mwanzo wa vilio vingine vya wajumbe wa Zanzibar ambao, mmoja baada ya mwingine, walieleza wasiwasi wa kupoteza jina "Serikali ya MApinduzi Zanzibar SMZ"

Ni Karume, ambaye kwa kutumia ujanja na nafasi yake, alipenyeza hija ya kura ya maoni katika taarifa ya Kamati ya Rais Kikwete hata kabla haijawasilishwa katika kamati kuu (CC)

Hoja ya Karume ilikuwa ni pamoja na kutaka ushirika serikalini, kama utakuja iwe baada ya uchaguzi wa 2010 jambo ambalo tayari CUF wamelikataa kwa kishindo.

Kutokana na ushawishi wa Karume wajumbe watatu wa kamati ya Rais upande wa CCM ambao ni Yusuph Makamba, Kingunge Ngombale-Mwiru ana Ali Ameir Mohamed, walipenyeza mawazo ya kura ya maoni bila kujadiliwa ndani ya kamati ya pamoja.

Chozi la Karume katika CC ndilop linasadikiwa kumlainisha Rais na Mwenyekiti Kikwete, kusahaulisha ahadi yake na huenda kumbadilisha mawazo kuhusu umuhimu wa kumaliza hara mpasuko Zanzibar.

Kikubwa zaidi ambacho wajumbe walililia ni "kupoteza madaraka" Visiwani. Wengi waliona kushiriki kwa CUF katika utawala kutaweka chama hicho karibu na ushindi na hatimaye kukumba madaraka na kuizamisha CCM.

Mjumbe mmoja alikaririwa akiloloma "kulikoni?kuna nini ndani ya CCM? Viongozi wetu mmetufikisha wapi?Utaratibu wetu unasema bwana, ninyi (CUF) hamna chenu"

Mjumbe huyo ambaye ametajwa kuwa Mustapha Ahmada wa Kaskazini Ungua, alihoji "Tunajadili nini hapa?Mnaturudisha nyuma, Wapinzani Zanzibar hawana wanachotambua; kwao mapinduzi ni haramu, ... mnatupeleka wapi?"

Alisema "wanatuita wahafidhina, mahafidhina. Watasema ... tumeishawaweza. Leo sisi CCM, haki ya Mungu na Mtume, hatutashika tena madaraka Zanzibar" akimaanisha iwapo CUF watashiriki utawala.

Kwa sauti ya juu na kuhema, Ahmada alisema "Wafahamu (CUF) kuwa hatuko tayari. Kama mmeshachoka (akiamanisha Viongozi wa CCM) acheni turudi na ASP Zanzibar".

ASP - Afro- Shiraz Party - ndicho chama kilichoungana na Tanganyika African Union (TANU) kuunda CCM 5 February 1977.

Mjumbe mwingine kuchangia hoja ya kuwa serikali shirikishi Zanzibar alisema kwa kuwa CCM pamoja na kura ya maoni, sharti CUF wakubali masharti kadhaa.

Aliyataja mashari hayo kuwa ni kutamka hadharani kwamba wanautambua uchaguzi mkuu wa 2005 kuwa ulikuwa halali, kwamba wanatambua kuwa Rais kuwa aliyeko madarakani Zanzibar ni halali na amechaguliwa kihalali.

Mjumbe huyo akichangia hoja ya kuweka uwanja linganifu wa kisiasa Pemba alisema "Na Pemba ukiwapa uhuru wa mambo hayo, haki ya Mungu CCM itashindwa mwaka 2010. Hatuponi"

Hata hivyo mjumbe huyo baada ya kutoa uwanja sawa na CUF kukiri na kutambua serikali , kamati ya mazungumzo ya CCM ipeleke mapendekezo yake katika Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar kabla ya kufikishwa kwenye CC.

KAtka suti ya ushwasishina kuonyesha wasiwasi, mjumbe huyo alisema, "Bila kufuata haya, sisi wenyewe CCM tutakuwa tumejisokota"

Akigeukia wajumbe wote na kukazia macho kwa Mwenyekiti, alisema "Mnatuacha wenzetu" manatuacha! Leo Sief(Shariff Hamad) huyuhuyu, ambaye hataki mapinduzi, mnakaa naye eti kuridhisha wafadhili?Mimi sikubali hili. Mapinduziiiiiiiii.

Hoja ya kuwa serikali ya pamoja ilizua ubishi wa chinichini na hatimaye mlipiko wa ubishi na kung'aka kwa baadhi ya wajube.

Hali hiyo ilianzia kwa Kingunge Ngombale-Mwiru alipoanza kutoa mapendekezo aliyoyaita ya kamati ya Rais ambayo yalikuwa tayari amefanyiwa marekebisho na CC.

Ilikuwa pale wajumbe walipoanzisha zogo na kumkatisha Kingunge mara kadhaa, Kikwete aliingilia kati ili kurejesha utulivu.

Akijaribu kuwatuliza wajumbe Kikwete alisema tayari mapendekezo ya kamati yake yamefanyiwa kazi sana na CC na kuongeza kuwa hata nafasi ya makamu wa pili wa Rais mbaye ni msimamizi wa shughuli za serikali atatoka katika chama cha Rais.

Wakati kamati ya Rais ilipendekeza chama kilichopata ushindi wa pili kitoe Waziri Kiongozi(msimamizi wa serikali) CC ilipeleka NEC pendekezo la kuwa na makamu wawili wa rais.
Kwa kuzingatia hoja ya "Kuipiku" CUF, Kikwete alisema pendekezo la CC linataka makamu wa pili wa Rais ndie awe msimamizi wa shughuli za serikali huyo atatoka chama alichotooka Rais na ndie atachukua nafasi ya Rais wakati Rais hayupo.

Alifafanua kuwa idadi ya mawaziri kwa kila chama itazingatia uwiano na viti vya baraza la wawakilishi.
Katika hali ya sasa ambapo CCM ndiocho chama kilichotoa Rais ,kama kungekuwa na Serikali ya pamoja basi makamu wa kwanza wa Rais ambaye anatoka CUF angekuwa "picha tu" Hana majukumu yanayoeleweka.

Mchangiaji Mwanamke alitahadharisha CCM kuwa wakishindwa watapigwa mawe alisema "Mmmeaa mmejadili yote haya, mnasema ni mambo mazuri Haya!LAkini tusije tukapigwa mawe njiani"

Tarehe 30 December 2005, Rais Kikwete aliahidi Watanzania na Dunia kwamba atamaliza "pasuko wa kisiasa Zanzibar"

Kamati yake imekutana mara 21 ndani ya miezi 14 na kutumia karibu shilingi billioni 2 kwa kazi ambayo kutokana na mapendekezo ya Butiama ndio kwanza immeanza upya.

NAyo CUF imeitisha maandamano nchi nzima kupinga kuwepo mapendekezo mapya ambayo yanatibua kazi nzima na kufanya mabilioni ya fedha za umma na wafadhili yaliyotumika kuwa kama yamechomwa moto.

Maandamano ya CUF yataanzia Zanzibar Jumamosi ijayo ambako kumbukumbu za mauaji ya Januari 26 na 27 2001 zingali hai.

Source: Mwanahalisi

Eng Mohamed UPO???? Watu wanalia wanaona muafaka kuiingiza CUF maslahi yao yatakuwa hatarini soma kwa kituo kisha tafakari. Tunajua mpo wengi humu mnapewa pesa zetu tunazokatwa kwenye kodi kupunguza speed lakini hamtaweza kamwe Aluta.....

Sokomoko.

Picha ya karume akilia tafadhali
 
Back
Top Bottom