Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
Uswidi yaridhishwa na siasa Zanzibar
Na Ali Suleiman, Zanzibar
SERIKALI ya Uswidi imesema imeridhishwa na hali ya kisiasa ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo amani na utulivu vimeimarika katika kipindi cha Serikali ya Rais Amani Abeid Karume.
Hayo yalisemwa juzi na Balozi wa Uswidi nchini, Bw. Steffan Herrstrom, alipozungumza na gazeti hili na kusema utulivu huo umeifanya nchi yake kuzidi kuimarisha uhusiano na misaada yake kwa Zanzibar.
Alisema Uswidi imefarijika na kuwapo amani na utulivu na sasa imejikita zaidi kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwamo elimu.
Alisema nchi yake itahakikisha inaimarisha sekta ya elimu ambayo umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa ni mkubwa huku lengo likiwa ni kuona vijana wanapiga hatua kubwa ya maendeleo.
"Uswidi tumejikita zaidi katika kutoa misaada yetu kwa Serikali ya Mapinduzi katika sekta ya elimu...sekta ya elimu tunaipa umuhimu wa kwanza," alisema Balozi Steffan.
Uswidi ni moja ya nchi ambazo zimekuwa zikitoa misaada kwa wingi katika sekta ya elimu kwa shule za Serikali Unguja na Pemba, ukiwamo mradi wa ujenzi wa shule za kisasa.
Imekuwa pia ikitoa mafunzo kwa walimu wa Chuo cha Ualimu cha Nkrumah nje kidogo ya mji wa Unguja kwa ajili ya maandalizi ya shule mpya za Unguja na Pemba.