Karume aleta faraja Zanzibar!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Uswidi yaridhishwa na siasa Zanzibar



Na Ali Suleiman, Zanzibar

SERIKALI ya Uswidi imesema imeridhishwa na hali ya kisiasa ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo amani na utulivu vimeimarika katika kipindi cha Serikali ya Rais Amani Abeid Karume.

Hayo yalisemwa juzi na Balozi wa Uswidi nchini, Bw. Steffan Herrstrom, alipozungumza na gazeti hili na kusema utulivu huo umeifanya nchi yake kuzidi kuimarisha uhusiano na misaada yake kwa Zanzibar.

Alisema Uswidi imefarijika na kuwapo amani na utulivu na sasa imejikita zaidi kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwamo elimu.

Alisema nchi yake itahakikisha inaimarisha sekta ya elimu ambayo umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa ni mkubwa huku lengo likiwa ni kuona vijana wanapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Uswidi tumejikita zaidi katika kutoa misaada yetu kwa Serikali ya Mapinduzi katika sekta ya elimu...sekta ya elimu tunaipa umuhimu wa kwanza," alisema Balozi Steffan.

Uswidi ni moja ya nchi ambazo zimekuwa zikitoa misaada kwa wingi katika sekta ya elimu kwa shule za Serikali Unguja na Pemba, ukiwamo mradi wa ujenzi wa shule za kisasa.

Imekuwa pia ikitoa mafunzo kwa walimu wa Chuo cha Ualimu cha Nkrumah nje kidogo ya mji wa Unguja kwa ajili ya maandalizi ya shule mpya za Unguja na Pemba.
 
kada pole sana kwa kuban, wenye kukaandamiza demokrasia popote washindwe
 
Well, Amani na utulivu wa Zanzibar hauko mikononi mwa Karume mwenyewe tu, na kutulia kwa munkari wa Maalim Seif na Chama chake ni mojawapo ya sababu za Zanzibar kutulia...

Hivyo basi wapongezwe wote!!! Maalim, Karume, CCM na CUF
 
Uswidi yaridhishwa na siasa Zanzibar




Imekuwa pia ikitoa mafunzo kwa walimu wa Chuo cha Ualimu cha Nkrumah nje kidogo ya mji wa Unguja kwa ajili ya maandalizi ya shule mpya za Unguja na Pemba.
Good news, SMZ nao wakifanyie matengenezo Chuo cha Ualimu...
 
Kada ulifanya kosa gani? ,hebu nielezee kidogo nijue bana maana wahenga walisema ukiona mwenzako ananyolewa?....(tumia hata lugha ya picha nitaelewa)

ndugu yangu mie sijui kwa nini, lakini niliweka intavyuu ya zitto tuanze kujadili, punde nikaona imewekwa recylce bin nijalalamika, ikaunganishwa sijui na thread gani kutahamaki watu wakaanza kulalamika kwa nini threads/post zinafutwa mwishowe nikasikia wameniban ! kwa hiyo siwezi nikasema ni kwa nini nilibaniwa ! yameisha lakini !
 
Uswidi yaridhishwa na siasa Zanzibar

Na Ali Suleiman, Zanzibar

SERIKALI ya Uswidi imesema imeridhishwa na hali ya kisiasa ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo amani na utulivu vimeimarika katika kipindi cha Serikali ya Rais Amani Abeid Karume.

Hayo yalisemwa juzi na Balozi wa Uswidi nchini, Bw. Steffan Herrstrom, alipozungumza na gazeti hili na kusema utulivu huo umeifanya nchi yake kuzidi kuimarisha uhusiano na misaada yake kwa Zanzibar.


Mkuuu wa Pwani,

Heshima mbele mkuu, ujumbe mzito sana!
 
huu ni wendawazimu eti akisema mzungu hata kama ni uongo tutakumbatia na kucheka meno yote 32 kisa? Mzungu huyo!

acha upuuzi zanzibar haijawa unavyotaka kutuaminisha, amani na utulivu ni mjumuiko wa mambo mengi yasiyohitaji karume tu!

hawa ndio wale tunaowaita wazandiki wasiopenda ukweli! amani hata chakula kikikosekana, hakuna amani sasa wewe hiyo amani kwa uchumi mgumu huu itoke wapi? huoni mawaziri wametapakaa mikoani wanalazimisha uzuri wa bajeti? kizuri daima hujiuza ila kibaya hujitembeza! je huko kwenu wamekuja?

angalia wanawatenga hawajui wanalolifanya nawe unaungana nao kushabikia kelele!

haya wewe wafagilie lakini uchumi unatubabua yangu macho tu, najua umbumbu wako hautakoma hivi karibuni ila sisi tutakusaidia uamke!

karamagi katika mkataba wa buzwagi aliwaona wazungu akawambia "jamani nyie ni wazungu tunaomba mfanye draft ya mkataba halafu sisi tutasaini tu. ilipokosewa kidogo karamagi alifuta kwa mkono ili awaridhishe! ndio nawe unayaleta hapa eti kisa balozi wa sweden amesema kweli! kwanza huyo ni mgeni bado hajui zanzibar ikoje. nakuacha lakini najua utaja kujua niyasemayo mwakani.
 
yaani kuna chuo kimoja tu cha ualimu kisiwa kizima ? nadhani ntu wa pwani atuambie !

kwa taarifa zanzibar ina vyuo ambavyo vinatoa stashahada ya elimu visivyopungua vitatu:

Zanzibar Muslim Coolege kikko Mazizini Zanzibar

Beit el Ras kiko hapo BEIt el raS au tunakiita NKurumah Training College.

pia tunacho pemba tunakiita Benjamin William Mkapa na pia tunacho chuo cha kiislam


vyuo vyenye kutoa degree ya kwanza

Zanzibar State University(SUZA)
Zanzibar College(kiko chukwani)


chuo kinachowaandaa maengineer wetu kwa stashhada na FTC
Mbweni Technical College.


tunacho chuo cha afya mbweni na sasa tuunakiimarisha ili kiwe na hadhi ya kupambana na karne ya 21.

kuna tawi la chuo kikuu huria unguja na pemba.


na tuzingatie idadi ya wazanzibar kwa ujumla ni karibu milioni moja.

na umuhimu wetu wa kwanza kwa sasa elimu kwa watu wetu. nnampongeza kwa dhati Mh Amani Abeid Aman Karume Rais wetu aliejitahidi kusimamia mazungumzo na CUF na kumuwezesha Maalim Seif kupata haki zake na kutulia.

wakati huo huo nnamshukuru kwa dhati maalim kuweza kuwadhibiti vitimba kwiri ktk chama chake ambao daima walikuwa wakitishia amani ya zanzibar.

ila kazi ni kubwa mbele yenu viongozi wetu kutuletea maendeleo, kwanza kuimarisha na kustawisha hali ya maisha ya wazanzibar japo hilo mmmejitahidi ila tatizo liko kwenye muungano na hapa tunawalaumu wazeee wetu waliingia kwenye muungano kwa pupa sana bila ya kuzingatia na waliofuata wakaanza kuizamisha zanzibar hatua kwa hatua.

leo hata vitega uchumi kwa coverage ya tanzania mnatakiwa msaini na kuomba bara, ila wao zanzibar wanaingia bila ya tabu mfano Zantel ilisaini Zanzibar ilipotaka kuweka coverage kote ilizuiwa, lkn Celtel Tigo ruhsa kufika zenji.

masuala ya baharini Marine sayansi pia wakuu hamna mamlaka nayo, serikali yetu tukufu ya mapinduzi leo haina madaraka yoyote nje ya visiwa na uwezo wa kujinyanyua kiuchumi ni mdogo mno.


kuna hili suala la mafuta nnakuombeni sana viongozi wangu nyote wa serikalini na upinzani mtangulize maslahi ya zanzibar kwanza, hao kina kara za mangi wasikuzidini maarifa, wao ndio mnaona walivyoitosa nchi yao.

madini na gesi sio vya pamoja na wao wenzetu mola aliwapa madini muda mrefu na wala ss hatukudai hata siku moja viorodhoshwe kuwa mali ya muungano, ila sasa wameona mafuta kwetu tena mengi ati mali ya muungano hawa ndugu zetu ila tujue vya kukaa nao.

pa maslahi hjidai sana udugu lkn maslahi yakiwa kwao zanzibar hakuna udugu, hili ukiliweza kidume amani tutakukumbuka milele na tutakupamba kwa mauwa.
 
kuna hili suala la mafuta nnakuombeni sana viongozi wangu nyote wa serikalini na upinzani mtangulize maslahi ya zanzibar kwanza, hao kina kara za mangi wasikuzidini maarifa, wao ndio mnaona walivyoitosa nchi yao.

Nchi yao wao na akina nani? Wewe siyo nchi yako?

Hivi leo hii serikali ikitangaza kuna mafuta Mafia, au Bagamoyo, au ruvuma unaweza kwa dhati kusimamia kauli yako kuwa Mafuta siyo suala la Muungano?

madini na gesi sio vya pamoja na wao wenzetu mola aliwapa madini muda mrefu na wala ss hatukudai hata siku moja viorodhoshwe kuwa mali ya muungano, ila sasa wameona mafuta kwetu tena mengi ati mali ya muungano hawa ndugu zetu ila tujue vya kukaa nao.

Una uhakika kwamba serikali ya Zanzibar haijapata fungu lolote litokanalo na mapato ya madini?

Hivi unataka kuniambia Serikali ya Zanzibar hainufaiki kutokana na mapato yatokanayo na gesi ya songosongo? gesi ya songosongo iko Zanzibar?

Hivi umeme wa Zanzibar unatoka wapi?.

Mtu wa Pwani:
Ukishamaliza kujibagua kwa kujiita wewe ni Mzanzibari na wao ni watanganyika unatenda dhambi ya Ubaguzi.

na dhambi ya ubaguzi haifi,

Baadaye utakuja kugundua kuwa kumbe nyinyi si wamoja, bali kuna WAPEMBA NA WAUNGUJA

Wapemba watasema ona! , Mafuta yapo kwetu lakini wanaonufaika ni Waunguja!, hatukubali!!
Hapo ndipo utakapokuja kugundua kwamba japo Muungano una baadhi ya Matatizo ni bora kuyatatua matatizo hayo kwa Mazungumzo na Mashauriano na si kwa kujibagua kwa Misingi ya UZANZIBARI nA UZANZIBARA
 
unashangaa nini ntu wa pwani ! huyu shalom sijui mtu wa wapi !

mshamba mmoja mbaye ninachukizwa sana na mafisadi haswa wapambe wao kama wewe kada unaniumiza sana roho. kwani bila mtu kama wewe mama zetu wasingekuwa wanakufa wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma ndogo kama hiyo, waatoto wetu wasingekuwa wanakufa chini ya umri wa miaka mitano, hata mama yako asingekuwa anadandiwa na wahuni kwa kisingizio cha kupanda dala dala. sasa hivikweli unapenda hiyo au unafiki wako umevuka mipaka kiasi hicho. hisia zangu wewe kada ni mtoto wa mlalahoi tu ila ni upungufu tu wa mawazo tafauti na mtu wa pwani ambaye ameshazoea kunywa damu ya watanzania kwa kutumia magari na majumba ya kifahari na kujiona wajanja(short run). nyie wenzetu hayo hamyaoni zaidi ya kuleta habari za kijinga kama aliyoweka huyo mtoto wa fisadi. hata mtoto mdogo ukimuuliza atakuwambia rais bomu kuliko wote duniani ni huyo unayetuletea habari zake, hata akiongea utajua tu. wazungu wameshatuana sisi ni kama nyani sasa ulitaka waseme kuwa mna rais bomu itabidi watudanganye kama hivyo.
 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi wa kisiwani Pemba, kuacha siasa za chuki na kuthamini maendeleo makubwa yaliyopelekwa na Serikali.

Akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 31 tangu kuzaliwa kwa CCM, Rais Kikwete alisema Pemba imepata mafanikio makubwa katika sekta za barabara, maji safi na salama na umeme.

Alisema barabara nyingi zimejengwa kisiwani humo zikiwemo za Mtuhaliwa-Chake, Chakechake ``Mkoani, Wesha Chakecheke na nyingine zipo katika mpango wa matengenezo kwa kushirikiana na wafadhili.

Alisema barabara hizo zinazojengwa zina urefu wa kilomita 123, ikiwemo ya Mzambarautakao ``Finya, Kuuyu Kangagani na Kojani Wete-Gando.

Alisema hivi sasa serikali ya Zanzibar imefanikiwa kutengeneza bandari za Wete na Mkoani ambazo zitatoa mchango mkubwa katika kukuza kipato cha wananchi na serikali.

Aliongeza kuwa, hivi sasa mradi mkubwa wa umeme kutoka Tanga hadi Pemba kupitia chini ya bahari, unaendelea kutekelezwa na kukamilika kwake kutamaliza tatizo sugu la uhaba wa huduma ya umeme kisiwani humu.

``Tuachane na watu wanaoeneza chuki, pale penye mafanikio, lazima tuseme kweli hata kama hatupendi,`` alisema.

Kuhusu mazungumzo ya kumaliza mpasuko wa kisiasa kati ya CCM na CUF, alisema dalili zinaonyesha yatafanikiwa.

Alisema jambo la msingi ni wana-CCM na CUF, kuwa na subira wakati viongozi wakiendelea kukamilisha hatua za mwisho za mazungumzo hayo.

Hata hivyo, alisema CCM sio chanzo cha tatizo lililopo na ndio maana ilikuwa ya kwanza kuamua kukaa pamoja kutafuta ufumbuzi wake.

Rais Kikwete alisema lengo kubwa la mazungumzo hayo ni kubadilisha mahusiano na kuondoa uadui na siasa za uhasama na badala yake kujenga misingi bora ya demokrasia.

Aliwakumbusha viongozi wa CCM kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama ili kujenga mazingira mazuri ya ushindi mwaka 2010.

Alisema serikali inakusudia kuimarisha uwajibikaji na kuwataka viongozi kuzingatia umuhimu wa maadili ya uongozi na kupiga vita vitendo vya rushwa.

Katika maadhimisho hayo, wanachama 1,000 kutoka mikoa miwili ya Pemba, walipewa kadi za CCM.

Alisema CCM itaendela kuimarika kwa kuwa na viongozi waadilifu na wajasiri.

Mapema, akimkaribisha, Rais Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, aliwataka wapinzani wakae chonjo katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kuwa CCM ina nafasi kubwa kuchukua viti kisiwani Pemba.

Alisema kwamba ni kweli katika uchaguzi uliopita, CCM haikufanikiwa kupata kiti kisiwani huko, lakini mahudhurio yaliyoonyeshwa na wananchi katika mkutano huo, ni dalili za ushindi wa chama hicho.

Viongozi mbalimbali walihudhuria sherehe hizo wakiwemo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Bw. Ali Juma Shamuhuna na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom