Karne ya hii,wanaume wanaolialia na Mapenzi wanashangaza sana.

Mapenzi unayozungumzia wewe hayana future ndio maana unachukulia mambo kirahisi sana. Lakini kama mtu umepanga mambo muhimu na yenye future na mwenzake na huyo mwingine akachukulia kirahisi kama wewe lazima kulia kupo.
 
Kwanza kabisa mtoa mada umesema mtu anatukanwa ukiona hivyo jua huyo jamaa ni muhuni hivyo kashtukiwa na njama yake
 
Sawa mimi nakubaliana nawe kiasi lakini kitu kinachonishangaza ni kwa nini wahanga wawe wanaume siku zote? kwa mfano unakuta mtu anadai kwamba anaangalia future kama unavyodai, ila utakuta mwanaume na mwanamke wote wana hela ila wakiwa pamoja siku zote mwanaume ndo anagharamia kila kitu.Tena usikute kipato chake kidogo zaidi sasa future za namna hiyo shida tupu. Au kama ishu ni future, kwa nini yeye akutukane na sometime kukudhalilisha?(unakuta mwanaume kwa mfano analalamika kwamba demu wangu tukiweka apointment mimi naenda yeye ananizungusha, ila jamaa anakomaa tu) yeye hiyo future haitaki? na kama haitaki wewe unaing'ang'ania ya nini? Huu ni muda wa kuwa straight! mkuu.
 
Yaani kwa kweli inashangaza sana sana,

Karne hii , unakuta mwanaume analia lia eti ananyimwa na mkewe. Ajabu sana!
Karne hii , eti mwanaume anamtongoza mwanamke miezi 5, mwaka hadi miaka. Ni ajabu sana!
Eti karne hii , mwanaume unapigwa vizinga vya hela ndefuuu na mademu ambao una uhakika huna future nao na unatoa halafu unalia lia kuwa maisha magumu. Ni ajabu sana.
Eti zama hizi, wanaume unahonga miezi sita mfululizo kwa lengo la kupiga tu mzigo. Hahahaha! aiseee! hurumaaa!
Eti zama hizi unakuta mtu hakutaki, unataka kwa mfano umpe hela (au kitu chochote kwa nia nzuri tu) halafu anajifanya hazitaki nawe unafanya kazi ya kumng'ang'anizia ili azichukue. hatari sana.


Zama hizi ni zama za kazi tu kwenye kila kitu. Ukiona mtu anakuletea mbwembwe za kijinga tunza hela yako vizuri wekeza kwa biashara.Shauri yako!. Tafuta sehemu ambayo unaweza kupata kitu bora kwa gharama nafuu na usumbufu kidogo! .Ni lazima kwanza ujue unataka nini na ili nini. Mtu unamfuata kistaarabu na kwa nia njema kabisa anajifanya anatukanaa, mara hivi mara vive nawe unakomaa tuu. Ya nini sasa! tubadilikeni wakuu.

YOU CAN SAY THAT AGAIN.....
 
Kama umewahi kushiriki ngono zembe na mabinti tofauti jiulize kwa nini ulikwama kwa huyo uliyenae hadi sasa hayo yaliyokunasa kwake ni siri yako hayo ndio mapenzi
 
Mleta mada hajakuwa kiumri na wala si mstaarabu
akasome vitabu vya Dini atakutana na jamaa aliyechunga kondoo miaka 7 akapewa bint mkubwa kwani yy alitaka akaambiwa aongeze miaka mingine 7 ili ampate amtakaye.
hakuna mapenzi ya kizamani
 
Namnukuu Daata
Mapenzi unayozungumzia wewe hayana future ndio maana unachukulia mambo kirahisi sana. Lakini kama mtu umepanga mambo muhimu na yenye future na mwenzake na huyo mwingine akachukulia kirahisi kama wewe lazima kulia kupo.
Umeongea ukweli...mtupu yaani mtu ulimuweka moyoni then akakuzingua utatamani hata ufe tuuu....yam mapenzi haya dahhhh....mungi atusaidie aseee!!!!
 
Kama unakutana na hawa wa barabarani sawa ila katika serious relationship kuwekeza si jambo la ajabu kwa %nyingi.
 
unapaswa kutofautisha kati ya wavulana na wanaume, ukishajua ndio useme...!!!
 
Back
Top Bottom