Karne hii bado watu wanabatizwa na kuita watoto wao majina ya kizungu?

Kutumia jina la kizungu Si issue kubwa sana, Kikubwa ni watu kuelewa umuhimu/Asili/Maana ya hayo majina..Ingawa kumekuwepo na hali ya kushamiri ya Majina ya kizungu, Bado suala la Jina linabaki kuwa uamuzi wa mtu mwenyewe pia si kwamba watoto hawapewi majina ya asili ya Nyumbani!! Wanapewa hayo Majina na Babu, Bibi, Shangazi zao ila utumikaji wke unakua Hafifu Sana pengine ni kutokana na mentallity ya USASA
 
Mkuu unavo wazugumzia wakiristu peke yao unakosea, pengine kuna sheria za kanisa zinazo shurutisha wakiristo wabatizwe kwa majina ya watakatifu wao mimi sijui.
Tatizo kubwa lipo kwa waislamu (mimi mojawapo).
UISLAAM, haumlazimishi muislam kutumia jina la kiarabu,masahaba wala majina ya manabii walio tangulia, lakini unakuja kukuta waislamtz, hawa tumia kabisa majina ya makabila asili na hayo yakiarabu wanayo tumia kwa kujilazimisha, wanayatamka visivyo, na mpaka sasa hivi wanadiriki kuamini majina ya kienyeji ni haramu kutumia na kuyaita ni yakikafiri
Hamna jina la kikristo wala kiislamu..
Dini haijaainisha mahala popote kwamba majina Haya ni kwa ajili ya watu wa Dini fulani, ni mazoea ya kifikra na tamaDuni ndio zimechangiak hali hii kuwepo...
nDio maana hata hao wanaosema majina ya kikafiri wanakua WANAPOTOKA,historia za watawala, viongozi wakuu wa Dini, wanaharakati kutokana na Dini walizokuwepo nDio watu wanashawishika pengine majina yko Based ktk Dini fulani
 
sasa mtoa mada unataka mwanangu nimuiteee masumbuko,shida,sikujua ,tatu,jumanne,kumaleja,sijaona kwanini nisimuite petro au yohana au albert swala la majina ni la mtu binafsi watu hutafuta majina mazuri kwa ajili ya watoto wao yenye utambulisho na kuakis maisha ya baadae, ni mara mia nimuite mwanangu emanuel kuliko masumbuko,kama ni usasa potelea mbali
 
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
badili id yako jiite la kiafrica wewe mwenyewe una uenzi uzungu huku nje unajifanya kuukataa shame on you
 
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
NAUNGA MKONO HOJA(ILA NA WEWE HILO LA KWAKO BADILISHA),HII ISHU YA UTUMWA WA KIFIKRA KTK KUWAPA WATOTO MAJINA MI NLISHAISTUKIA SIKU NYINGI,NINA WATOTO WANGU 3,WOTE NIMEBATIZA MAJINA YA KISWAHILI,NILISHAPIGA MARUFUKU MAJINA KIINGEREZA NYUMBANI KWANGU!ETI OOH! SIJUI IVAN,JUNIOR,BRIAN,BRIGHT,ANGEL,GRACE,GENEVIEVE,VANESSA, TUPA KULE, HAPA NI MWENDO TU WA MAJINA KAMA AMANI,FURAHA,TUMAINI,UPENDO,MALAIKA,MALKIA,FARAJA NA MENGINE YA KILUGHA KAMA KOKU,ISHIMWE,PALAMAGAMBA,TUNDU, NCHEMBA,NAPE,MPINDASIGULU, NA MENGINE KAMA HAYO,NDO MAJINA YETU JAMANI TUYAENZI!
 
Back
Top Bottom