Karne hii bado watu wanabatizwa na kuita watoto wao majina ya kizungu?

Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
THE UNKOWN NI NENO LA KISWAHILI? MKUU KABLA YA KUPOST NA WW JIANGALIE KWANZA
 
Juzi Juzi nililuwa Makete , mwenyeji alienipokea jina lake ni "Network Sanga"
 
Hakuna research ambayo imewahi kufanyika kuhusu majina.
Kumbuka research sio lazima ifanywe na wazungu hata wewe unaweza, angalia watoto wanao itwa FURAHA angalia sifa zao kisha watafute wanaoitwa SHIDA angalia sifa zao pia
 
Kuna.majina yakisafwa haya
SHIDA
MAWAZO
MATATIZO
MASUMBUKO

Sasa wakinga wanaiga majina ya kizungu km.haya

POOL TABLE MBILINYI
ESCROW SANGA
nk

Na wasukuma.nao majina ya kizungu

GOBOLE MASUNGA
KIBELIT
BUNDUKI MSOKWA
nk

Kazi kweli.kweli
Mkuu haya majinia ni ya kweli au unatania 2
 
Mkuu haya majinia ni ya kweli au unatania 2
Kwamba hujawasikia.moja majina.hayoo
Hayo.yakisafwa nenda MBEYA mjin unakutanayo.sana

Wasukuma wamevamia.kula.chunya wanahayo majina.pia

Tembea na.ukingani makete,makambako nk
Unakuta na hayo
Pool table
Given
Escrow
Common
Nk
 
Kuna.majina yakisafwa haya
SHIDA
MAWAZO
MATATIZO
MASUMBUKO

Sasa wakinga wanaiga majina ya kizungu km.haya

POOL TABLE MBILINYI
ESCROW SANGA
nk

Na wasukuma.nao majina ya kizungu

GOBOLE MASUNGA
KIBELIT
BUNDUKI MSOKWA
nk

Kazi kweli.kweli

Hahahaa bhebhe nkoi, acha kutania makabila ya watu...
 
We unaongelea majina. Watu wanalalamika kwa nini kiongozi wao hajui kuongea lugha ya wakoloni sawasawa sembuse majina?
 
Wakristo wanawapa watoto hata majina ya Kibantu Mfano Neema, Upendo, Vumilia, Baraka, Elisifa, Elineema, Faraja, Lulu, Aika, Sifaeli, n.k lakini huwezi kukuta waislamu na majina ya Kibantu.

Wakristo mpaka mavazi ni ya Kibantu lugha ya kuendeshea ibada ni ya Kibantu lakini uislamu hivyo vyote ni haramu na najisi.

Nimekaa nikautafakari uislamu nikaona uislamu ni mfumo kamili wa utamaduni wa mwarabu tu.

Nilisikia mufti hawezi kuchaguliwa kama majina yake manne sio ya kiarabu

Mkuu Chongchung
Sijui umesoma wapi kwamba kuendesha ibada kwa Kibantu Au kuvaa Kibantu NI haramu Na najis.
Kuraan Tukufu imeandikwa Kwa Kiarabu kutokana Na sheria za Dini LAZIMA isomwe kwa Kiarabu Ila tafsiri inatumika Kwa Lugha ya waumini.
Mavazi ya Kiarabu hayajalazimishwa unacho takiwa kuvaa NI nguo Safi Na yenye heshima
Majina ya Kiarabu hayajalazimishwa Lakini Lugha ya Kiswahili maneno mengi NI ya Kiarabu
Kwahiyo watu wengi tumechukua majina ya Kiswahili.Kipozoe,Juma,Jumanne Baraka Pili yako mengi tu.
Wako wataalam wengi watachangia wenye elmu kubwa ya Dini ya Kiislam.
 
Mkuu unavo wazugumzia wakiristu peke yao unakosea, pengine kuna sheria za kanisa zinazo shurutisha wakiristo wabatizwe kwa majina ya watakatifu wao mimi sijui.
Tatizo kubwa lipo kwa waislamu (mimi mojawapo).
UISLAAM, haumlazimishi muislam kutumia jina la kiarabu,masahaba wala majina ya manabii walio tangulia, lakini unakuja kukuta waislamtz, hawa tumia kabisa majina ya makabila asili na hayo yakiarabu wanayo tumia kwa kujilazimisha, wanayatamka visivyo, na mpaka sasa hivi wanadiriki kuamini majina ya kienyeji ni haramu kutumia na kuyaita ni yakikafiri

Mphingu kabla ya kuandika mambo yasio Na ukweli Tafadhali ulizia wasomi wa Dini Au soma Mwenyewe.WaislamTz uliuliza watu wangapi au sheikh gani au ulisoma wapi?Huwezi kuandika "WaislamTZ" wakati umeongea Na rafiki zako kijiweni
 
kweli kabisa mimi nitapenda kutumia majina yetu ya asili kuliko ya kizungu au kiarabu maana tumekua watumwa mpaka tume pitiliza aise na hizi dini ndiyo zimetufanya kuwa vipofu kabisa aise
 
Mkuu Chongchung
Sijui umesoma wapi kwamba kuendesha ibada kwa Kibantu Au kuvaa Kibantu NI haramu Na najis.
Kuraan Tukufu imeandikwa Kwa Kiarabu kutokana Na sheria za Dini LAZIMA isomwe kwa Kiarabu Ila tafsiri inatumika Kwa Lugha ya waumini.
Mavazi ya Kiarabu hayajalazimishwa unacho takiwa kuvaa NI nguo Safi Na yenye heshima
Majina ya Kiarabu hayajalazimishwa Lakini Lugha ya Kiswahili maneno mengi NI ya Kiarabu
Kwahiyo watu wengi tumechukua majina ya Kiswahili.Kipozoe,Juma,Jumanne Baraka Pili yako mengi tu.
Wako wataalam wengi watachangia wenye elmu kubwa ya Dini ya Kiislam.
Pole sana kwa kushindwa kutambua na kujua dini yako inakutaka uweje.

Kwanza nikupe homework ni hivi kwa mujibu wa dini yako wakati marehemu yako mwanandani pale muda mfupi baada ya kuzikwa.

Atatokea malaika mmoja atakuja kumuhoji maswali kuhusu matendo yake ulimwenguni na quran inaeleza wazi huyo malaika hatambui lugha yoyote zaidi ya kiarabu na endapo utashindwa kuongea kiarabu malaika yule atakupiga sana haijalishi ulikua unatenda mema au mabaya na mwisho utaenda jehanamu.

Katika mamia niliyonayo kuhusu imani yako nimeona nikupe hiki kidogo ukakifanyie kazi kwa mashehe wako na wasomi wa kiislamu kisha urudi hapa nikuongeze.

Chengine ni kwamba quran unasema ndugu wa muislamu ni muislamu mwenzie tu hata kama ni mama yako dini tofauti haupswi kushirikiana naye kwa lolote sababu sio ndugu yako.
 
Mkuu unavo wazugumzia wakiristu peke yao unakosea, pengine kuna sheria za kanisa zinazo shurutisha wakiristo wabatizwe kwa majina ya watakatifu wao mimi sijui.
Tatizo kubwa lipo kwa waislamu (mimi mojawapo).
UISLAAM, haumlazimishi muislam kutumia jina la kiarabu,masahaba wala majina ya manabii walio tangulia, lakini unakuja kukuta waislamtz, hawa tumia kabisa majina ya makabila asili na hayo yakiarabu wanayo tumia kwa kujilazimisha, wanayatamka visivyo, na mpaka sasa hivi wanadiriki kuamini majina ya kienyeji ni haramu kutumia na kuyaita ni yakikafiri
Una uhakika na usemacho?
 
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
Uhuru wa kiuchumi, Science etc. Ebola iko Africa, dawa wamegundua Canada. Hilo halikuumi. Unalilia majina. Zika inatafitiwa dawa USA, hilo halikuumi, kuwa matatizo yetu tuyakabili kuliko kuwapa wazungu. Hilo hulioni. achana majina ni upuuzi. Wazungu are superior. Hiyo internet unayokalia wakifunga, mtandao huu utakufa instantly, hilo halikuumi kuwa tunabidi tuwe na system za kwetu. Umekalia majina!!!!
 
Mimi baba yangu alikuwa muafrika huru wanae Wateja katupa majina ya asili yani Mwanzoni shuleni nilikuwa nashangawa sana hata na Walimu ila badae wakanizoea tu na nalipenda jina langu sana because I am unique
 
Uhakika ninao, wewe hapo ulipo first name, middle name na last yako yote ni yakiarabu na pengine hata ndugu na jamaa zako ni hivo.
TUSIDANGANYANE, waislamu tz tumeacha kutumia majina yetu ya asili, badala yake tunatumia majina ya kiarabu wakati dini yetu hailazimishi kutumia majina ya kiarabu wala haiharamishi kutumia majina yetu ya asili ya kibantu
 
mbona unazungumzi

Mbona unazungumzia majina ya kikristu tu ya kiislamu huzungumzii kwa nini?
majina ya kiislam asilimia kubwa ya maana ya kiswahili mf.amina, mwanaisha,Mwajuma, Mohammed nk. Kiswahili kinatokana na kiarabu kwa asilimia nyingi hivyo majina ya waislam yana maana ya kiswahili
 
Back
Top Bottom