COMFORT JAFFER
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 214
- 94
Waafrika alieturoga ametuweza.
Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.
Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.
Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?
Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?
Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.
Waafrika tuna matatizzo gani?
mimi mwanangu nimempa jina "Ngunyema"