Karne hii bado watu wanabatizwa na kuita watoto wao majina ya kizungu?

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,326
2,000
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
 
Nyamanoro

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
648
1,000
mbona unazungumzi

Mbona unazungumzia majina ya kikristu tu ya kiislamu huzungumzii kwa nini?
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?

Focus yetu ni maisha, majina ni utambulisho sasa katika kuchagua jina kila mtu anachagua utambulisho wa mtoto kuendana na mazingira yaliyomzunguka.

kukumbatia asili sana wakati mwingine kunaonekana kutokuwa na kumfanya aliyekumbatia asili kutoendana na maisha mfano waangalie masai waliokumbatia mila yao sana uniambie kama wanaonekana wa maana leo? zipo jamii zimeng'ang'ania kuendelea kuishi maisha ya porini.

kuna haja labda ya kuyatazama majina yetu ya asili ili tuyafanye yaendane na wakati au tutafute tafsiri ili mtu ajue jina hilohilo kwa asili ni linatamkwa je, kwa kiswahili linatamkwaje na kwa kizungu ili mtu asihangaike kuita mtoto majina mengi bali jina hilo moja linatafsiriwa kulingana na lugha.
 
MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Mkuu unavo wazugumzia wakiristu peke yao unakosea, pengine kuna sheria za kanisa zinazo shurutisha wakiristo wabatizwe kwa majina ya watakatifu wao mimi sijui.
Tatizo kubwa lipo kwa waislamu (mimi mojawapo).
UISLAAM, haumlazimishi muislam kutumia jina la kiarabu,masahaba wala majina ya manabii walio tangulia, lakini unakuja kukuta waislamtz, hawa tumia kabisa majina ya makabila asili na hayo yakiarabu wanayo tumia kwa kujilazimisha, wanayatamka visivyo, na mpaka sasa hivi wanadiriki kuamini majina ya kienyeji ni haramu kutumia na kuyaita ni yakikafiri
 
Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
910
500
Focus yetu ni maisha, majina ni utambulisho sasa katika kuchagua jina kila mtu anachagua utambulisho wa mtoto kuendana na mazingira yaliyomzunguka.

kukumbatia asili sana wakati mwingine kunaonekana kutokuwa na kumfanya aliyekumbatia asili kutoendana na maisha mfano waangalie masai waliokumbatia mila yao sana uniambie kama wanaonekana wa maana leo? zipo jamii zimeng'ang'ania kuendelea kuishi maisha ya porini.

kuna haja labda ya kuyatazama majina yetu ya asili ili tuyafanye yaendane na wakati au tutafute tafsiri ili mtu ajue jina hilohilo kwa asili ni linatamkwa je, kwa kiswahili linatamkwaje na kwa kizungu ili mtu asihangaike kuita mtoto majina mengi bali jina hilo moja linatafsiriwa kulingana na lugha.
Sijawahi ona Mzungu akaitwa Ntamaholo.kwa nini wewe uitwe Mr Grey.
 
MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Jina ni kitambulisho kinacho kutambulisha wewe ninani, wa inchi gani na kabila gani.
mfano, I'D "MPHINGU"ninayo tumia hapa JF, baadhi ya watu wanaweza wakanijua, mimi ni mtu wa kabila fulani na Mkoa fulani
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
hii hata mi huwa najiulizaga sana.. hivi hekima, utashi na busara zetu zinapimwa kwa kujilinganisha na wazungu na waarabu? kwanini sisi wenyewe tunajiona inferior zaidi kwenye mambo mengi? kwanini sisi waafrika (hasa Tanzania) hatujizingatii kama ni werevu kwa asili yetu? kwanini... kwanini... kwanini...?
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
1,744
2,000
Kuna kitu nimegundua watu wengi sana especially sisi waafrika linapokuja suala la cultural alienation tunazitolea macho tamaduni za kimagharibi na kusahau pia utamaduni umeathiliwa pia na watu wa mashariki ya kati kwa mfano kiukweli nikiangalia wanzanzibar naona kabisa ni watu waliopoteza identity ni waafrika wanaishi kiarabu na wanalaumu wazungu wanataka kuharibu utamaduni wao bila kujua kwamba hata ule pia sio utamaduni wao
 
silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,356
2,000
Waafrika alieturoga ametuweza.

Hadi miaka hii bado tunaamini majina ya kizungu ni bora zaidi kuliko majina ya kiafrika.

Sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kizungu, watu wengi wanaobatizwa wanabatizwa majina ya kizungu.

Kwani kuna mahala katika vitabu vya dini palipoadikwa ni lazima ubatizwe jina la kizungu au lililo katika vitabu hivyo?

Cha kushangaza watu hao hao wanaowapa majina ya lizungu watoto wao na wao wenyewe unakuta wanapiga kelele kua wanataka Africa iwe huru, uhuru upi wakati wewe mwenyewe hauko huru kifikra?

Miaka michache ijayo majina ya Kiafrika hasa hapa Tanzania yatakua yametoweka.

Waafrika tuna matatizzo gani?
Nadhani kujikomboa kiuchumi ndio la msingi. Kama hayo majina mababu zetu walikuwa nayo, faida yake ni nini kiuchumi?
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
kuna wakati inabidi tupige chabo hata kwa majirani zetu Afrika Kusini, Nigeria hata Waganda kiasi mbona wao wanapenda vya kwao? Afrika Kusini wanaishi na wazungu kabisa kwa karne kama ya 3 lakini kwa 60% wanatumia vitambulishi vyao, mila na tamaduni ambazo hubeba misingi ya maisha yao. wengi wana majina ya kizulu, kixhosa na ya kisan hata wazimbambwe wengi wana majina ya kindebele na kishona na wanajivunia kuwa hivyo... tatizo letu sisi lipo wapi? mbona tunashindwa kutumia elimu tunayoipata kujitathmini kuonyesha thamani yetu mbele ya wengine? wahindi, wachina, wathai, wakorea, wajapani wote na mataifa mengine yaliyoendelea wala hawana shobo na majina ya kizungu au kiarabu ila sisi.. kwaninin? sichelei kukubali mtu mweusi hasa mtanzania amelaaniwa kwa kweli mana hata yeye mwenyewe anajikataa!
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
sitaki kuamini.. kiimani kwa kutumia majina ya kizungu tunaenda mbinguni.. sitaki kuamini... kitaaluma kwa kutumia majina ya kizungu tunaonekana wasomi sana... sitaki kuamini... kijamii kwa kutumia majina ya kizungu tunaonekana wastaarabu sana... sitaki kuamini... kisanaa tukitumia majina ya kizungu au kiarabu tunaonekana masupastaa wajanja... nipo KAGERA kwa mwaka mzima, nilichogundua kimojawapo kutoka kwa wahaya, wahangaza, washubi na wasubi ni kuwa hawataki tena kuitawa kina kaijage, mwesigwa au izimbya au kaiyoza... huku majina ya kilatini yametawala yani utadhani tuko BUCHAREST ya watu weusi.. utakuta kila mtoto wa kiume jina lake mwishoni linaishia na "US", mara Priscus, Livinus, Beatus, Speratus, Orestus, Projestus, Canisius, Akasius, Avitus... Yani majina yao ya asili waliyobaki nayo ni hawa watu maarufu wa sasa hivi tu kina Mwesiga Baregu ila kizazi kijacho hakuna watakachojivunia kama watu wa kagera.. nawapa HEKO kubwa WASUKUMA ni majasiri kwa hakika.. pongezi kwako mleta uzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom