Karma ipo, trust me: Ubaya unaoutenda kwa wengine huwa unajirudia sana

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
176
Kuna mambo mengi sana mabaya ambayo tuna wafanyia binadamu wenzetu tena kwa kujua kabisa kama tuna tenda ubaya.

Maisha yalivyokuwa magumu bado unadiriki kumdhulumu mtu mali yake au pesa ambayo uliazima kwa unyonge.

Wahenga walisema usimtendee mtu jambo baya usilopenda kutendewa, hata vitabu vitakatifu vimesisitiza hivyo.
Binafsi kuna mengi sana nmeona na kujifunza haswa linapokuja suala la kutenda wema kwa mtu wakati wa uhitaji. Baraka huwa zinarudi kwa njia tofauti na kwa wakati tofauti.

Inamaanisha jambo zuri au baya litalipwa kutokana na matendo yako uliyokuwa unafanya. Mfano kuna jamaa yangu huwa haendi wala hajishughulishi na misiba ya watu yeye anajali mambo yake tu. Sasa juzi hapa amefiwa na mtu wake wa karibu kabisa akaanza kutafuta watu waje wampe support msibani.

Lakini wachache wakatuma rambirambi kwenye simu na hawakutokea ikabidi apambane mwenyewe kwenye shughuli pamoja na nduguze.

Ndio nikakumbuka ule msemo wa uswahilini unaosema."Usipokuja kwenye sherehe ya mwanangu siji kwenye msiba wa baba'ako".

So ubaya huwa unajirudia sana tu.

Au vile kwenye shughuli za watu wewe hauchangiagi kitu unaona ni upuuzi. Wenzio wakituma michango kama ya harusi ww hujihusishi. Siku yakitokea kwako ndo vile mnapgaga sana simu mnalazimisha tupokee simu zenu.

Kumbukeni kuna karma.
 
Hata mimi naamini kuna Karma, tutalipwa kwa mazuri na mabaya tuliofanyia wenzetu. Tujitahidi kusaidia wenzetu na kutenda wema kama ambavo tungependa na sisi kufanyiwa, malipo ya wema wetu yataturudia in the most unexpected ways!
 
Karma ni formula ya asili. Kamwe katu, abadani hautawahi kwepa uliyoyatenda hapa duniani kama si wewe wanao watakula katika matendo yako na kunywa katika katika wema au uovu wako.
 
Kwaio Huenda nayopitia Membe ni karma.
Sasa kosa alifanya kipindi gani..
Duuu ngachoka.
 
Back
Top Bottom