Karibuni!! Ufunguzi wa tawi jipya ccm luton,uk!!

VUVUZELA

JF-Expert Member
Jun 19, 2010
3,103
785

Baadhi ya Wadau waliohudhulia uzinduzi wa shina jipya la Luton wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Tawi la UK, Maina Owino.


Watanzania wengi walifurika Jiji la Luton Uingereza na kujiunga na chama cha mapinduzi katika ufunguzi wa shina jipya la Luton uliofanyika siku ya Jumapili Tarehe 12. 12. 2010 katika hoteli maarufu Chiltern UK.

Wengi wao wasema wana imani kubwa na CCM katika kuiongoza Tanzania kwa kuonyesha mwelekeo wa kuwa na imani na Vijana wasomi wachapakazi walioko ndani na nje ya nchi.

Ufunguzi huo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM – UK Ndugu MAINA OWINO kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama akiwemo Katibu Uenezi wa siasa Bwana Moses Katega. Pia Viongozi kutoka mashina ya Reading, Birmingham na Sehemu zote za London walijumuika pamoja.

Katika hotuba yake fupi Ndugu MAINA OWINO alitoa changamoto nyingi za mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya Uongozi wa Mwenyekiti CCM Taifa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE katika nyanja mbalimbali kama Madini,Elimu, ukusanyaji wa mapato ya serikali, waajiriwa wenye sifa za kukidhi nafasi za uongozi serikalini katika nyanja zote na ujasialiamali kwa watanzania wanaojitafutia maendeleo bila bugudha.

Changamoto kuhusu ushiriki wa vijana wasomi hapa UK kuingia katika mchakato wa siasa ndani ya chama ili kuleta mabadiliko yatakayozidi kukiimarisha chama kisera, mwelekeo na kuzidi kuwaletea watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali kupambana na kupambana na umasikini yalitolewa na Katibu wa shina jipya la Luton aliyechaguliwa siku Ndugu ABRAHAM SANGIWA na kuungwa mkono na wajumbe wote waliohudhuria ufunguzi huo

Viongozi Waliochaguliwa siku hiyo ni:

ALBERT NTMI – MWENYEKITI

ABRAHAM SANGIWA – KATIBU MKUU

JOHN MBWETE – MJUMBE

SAMMY MARTIN – MJUMBE

NORMAN WAGE - MJUMBE


 
Kuna msemo mmoja Mwalimu JKN alisema natumia neno zuri waji.......sisemi wapu..........Wapo kwa kweli tena wengi kweli. Kazi mnayo wandugu.
 
wamependeza sana katika hafla hiyo ya kujipongeza baada ya kazi ngumu za kuzibua vyoo wazifanyazo huko uk
 
NI KWA SABABU YA UCHAKACHUAJI ILIKUWA MAPANGA YATEMBEE SASA BORA KUBADILI MFUMO KULIKO KUUANA KAMA WAKENYA SIO VIZURI-SABABU NI NYINGI LAKINI KUBWA KUTOA AMANI YA KWELI MANAKE HAKUNA AMANI PASIPO HAKI, NA HIZI NYINGINEZOInakandamiza haki ya mgombea binafsi
2. Inatoa fursa ya kuwa na tume ya uchaguzi ya uchakachuaji
3. Inatoa fursa ya watawala kuwanyonya watanzania kwa kuficha mikataba
4. Inatoa fursa kwa rais wa nchi kuwakandamiza watanzania kwa maamuzi yasiyo na mpaka idadi ya wizara, teuzi mabalimbali
5. Inatoa fursa ya matumizi hovyo ya mali ya umma mfano kazi ya naibu waziri na mkuu wa wilaya v. Katibu wa wizara na mkurugenzi wa wilaya
6. Inavunja kanuni ya principle of separation of powers -mbunge anakuwa waziri, watawala wetu wengi wapo juu ya sheria
7. Inatoa fursa ya ufisadi kwa watawala wetu kwa kuzuia hatua yoyote dhidi yao
8. Ilitungwa kwa ajili ya chama kimoja na sasa ni vyama vingi
9. Katiba ya sasa ya tanzania haitambui zanzibar kama nchi
10. Katiba ya sasa inabeba sheria 40 za nyalali alizosema zifutwe
11. Katiba ya sasa inarusu uzandiki mwingi wa kuchakachua
 
Luton ndo TANDIKA YA UK. Kwa hiyo sishangai kuona walioko wanafungua tawi ls ccm.
 
Watoto wa mafisadi hao hata hawajui wazazi wao wamepataje pesa za kuwapeleka huko uk,kwanza owino sio mtanzania
 
CDM watafungua tawi U-DOM hivi karibuni na nyie wapiga box mnakaribishwa sio kazi kufungua matawi kwenye tandika au mabatini za uk(luton)....! Box limekua gumu mpaka mmeamua kukimbilia kwenye siasa afu kichaka mnachokimbilia kujifichia kimejaa SIAFU wengi kweli bora mrudi bongo tuu tuuze wote mitumba na kupiga debe maana najua wengi hamjasoma kama mimi kwani mlivyofika huko box liliwanogea mkakimbia shule...!
 
wanatekeleza haki zao za demokrasia

Yup uko sahihi kabisa.

Ila unaona unaweza kumshawishi mtu asiye nufaika kama mnavyonufaika nyie na hiyo ccm awe mwanachama,either mtu huyo nae aone ndio njia ya kutokea au iwe inamnufaisha kama ilivyo kwenu vinginevyo mtakuwa mnamcheka vijipembeni.

Lakini mbumbumbu wako so keepin it on
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom