Karibuni nitapata Shilingi milioni 100: Naomba ushauri wa namna ya kuiwekeza

Mar 23, 2021
51
125
Habari wadau!

Kuna mchongo nausikilizia wa milion 100, wazungu wanasema "easy money" sija-sweat sijui hata nitazifanyia nini masikini.

Itakuwa mbaya zaidi kama hundi ya pesa itadondoshwa harafu sijajua cha kufanya. Nipeni wazo niifanyie nini?

Uanze na kuweka million 50 UTT....den weka million 30 fixed deposit nbc wanapercent nzuri ya interest....alafu million 20 izungushe kwa businwss ulionayo kama huna business usianzishe business itaisha hyo pesa..kanunue ardhi uweke mifugo
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,453
2,000
Uanze na kuweka million 50 UTT....den weka million 30 fixed deposit nbc wanapercent nzuri ya interest....alafu million 20 izungushe kwa businwss ulionayo kama huna business usianzishe business itaisha hyo pesa..kanunue ardhi uweke mifugo
nifafanulie hapo kwny fixed deposit nbc wanatoa interest ngp na kwa muda gani?
 
Patroman

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
704
1,000
Tafuta eneo zuri lenye wakazi wa kutosha- ukipata heka moja au zaidi itapendeza - tengeneza parking ya magari- na vyoo vya kulipia- hata 100m yako haitaisha.
 
jaymoul

Member
Nov 29, 2020
52
125
Kaa mbali na huko ndugu yangu utafunguliwa faili milembe...bora ufanye kilimo uanze na mtaji mdogo na ufanye mwenyewe sio kilimo cha simu, upo mjini unawapigia vijana utalia!
Hivi kuna watu wanaofanya kilimo cha aina hii
 
MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
584
1,000
Kwa haraka sana ningefanya hivi. 100M nanunua Bond za miaka 25 hapa nauhakika wa kupata 15.95M kwa mwaka x miaka 25 na baada ya hapo principle amount inarudishwa. Ila pia kwa kununua tu hiyo bond naweza kuitumia kama dhamana kupata mkopo hawa wa 80% so naweza kukopa 80M nayo nikainunulia bond na nikatumia return za M100 na M80 kulipa mkopo na baada ya miaka michache nakuwa nimemaliza mkopo wote na kubaki na kipato cha 28M ambayo naweza kuwa nakula 2.3M kila mwezi bila kufanya kazi yeyte.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,906
2,000
Kwa mwaka 12%_14%
Duh.
Hii imenifanya nifikirie. Nikihamua kukopa pesa kwenye makampuni yanayo kopesha Ulaya. Mfano hapo chini moja ya supermarket kubwa ulaya wanakopesha kuanzia APR 2.9. Halafu nikaweka kwenye fixed akaunti hapa nyumbani nitakuwa ninalamba 12% mpaka 14%. Ni biashara nzuri.

Interest kwa mwaka ya mkopo wa £25,000 ni £ 289.24
Na fixed account uliyoweka £25,000 kwa 14% ni £3500.
Kwa hiyo £3500 - £289.24 = £3210.76(faida)

Lakini kuna vizingiti vyake. Mojawapo mkopo ni monthly instalments.
1DA44216-88E3-46C0-9D4B-44C6B5B3BD53.png
 
View attachment 1867687
Hapa ukirud
Tupia Jicho Government Bond.. Unapata Riba ya 15.95% kwa mwaka na hakuna kodi unayolipa ila kwa investment yyte chini ya 3yrs unafaa kulipa 10% kma withholding tax.
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,621
2,000
Hii ndio biashara gani mkuu??
Zipo nyingi vijana wataalamu wa IT wanazijua wanakuambia nipe hela tu halafu kwa mwezi utakuwa unatengeneza kiasi fulani...wengine wanafanya forex, cryptocurrency...unakuwa unapata hela tu bila kutoa jasho...ukiona hujazielewa hasa zinavyofanya kazi, wewe tulia tu jipe muda uelewe risk zake kabla ya kutumbukiza pesa ya kutosha
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,906
2,000
Tupia Jicho Government Bond.. Unapata Riba ya 15.95% kwa mwaka na hakuna kodi unayolipa ila kwa investment yyte chini ya 3yrs unafaa kulipa 10% kma withholding tax.
Asante mkuu. Nitaingia maktaba kujipatia elimu zaidi.
 
mapinduzi daima

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
1,675
2,000
Kwa haraka sana ningefanya hivi. 100M nanunua Bond za miaka 25 hapa nauhakika wa kupata 15.95M kwa mwaka x miaka 25 na baada ya hapo principle amount inarudishwa. Ila pia kwa kununua tu hiyo bond naweza kuitumia kama dhamana kupata mkopo hawa wa 80% so naweza kukopa 80M nayo nikainunulia bond na nikatumia return za M100 na M80 kulipa mkopo na baada ya miaka michache nakuwa nimemaliza mkopo wote na kubaki na kipato cha 28M ambayo naweza kuwa nakula 2.3M kila mwezi bila kufanya kazi yeyte.
Wazo bora... kabisa.
Nalitunza hili
2025 nita invest 75M
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,906
2,000
Zipo nyingi vijana wataalamu wa IT wanazijua wanakuambia nipe hela tu halafu kwa mwezi utakuwa unatengeneza kiasi fulani...wengine wanafanya forex, cryptocurrency...unakuwa unapata hela tu bila kutoa jasho...ukiona hujazielewa hasa zinavyofanya kazi, wewe tulia tu jipe muda uelewe risk zake kabla ya kutumbukiza pesa ya kutosha
Mkuu hii ninaelewa vizuri. Fraudster maarufu Bernard Lawrence Madoff ametutoa tongo tongo wengi.
Jana nimesoma kuna kijana ambaye ni stockbroker aliwashawishi wazee wa miaka 91 na mwingine miaka 81 wampe pesa kutoka kwenye savings zao aziwekeze. Akaenda kuziponda kwenye starehe. Na mzee mmoja amekufa…kuna watu wana roho za chuma!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom