Karibuni nitapata Shilingi milioni 100: Naomba ushauri wa namna ya kuiwekeza

Tafuta shamba pembezoni mwa Jiji la Dar es salaam.
Hasa upande wa Kongowe, Vikindu, Mwasonga ambapo ni karibu na Jiji la Dar. Au Msanga Kisarawe.
Hapo hukosi ekari 10-20, kwa Tsh, 50m.
Then wekeza hapo.

Au liache baada ya miaka miwili unaliuza 150m.
10m fukia Mashimo.
40 weka Benki utafakari cha kufanya.

NB
Shamba nunua kwa Serikari ya Kijiji. Sio kwa mtu.
 
Asante mkuu..!
Jiji la Dar linakua kwa kasi sana, ukiamua kifuga Nguruwe au Mbuzi au kuku ktk Shamba la Ekari 10 hadi 30, ni uwekezaji mkubwa sana.

Na ni wa uhakika. Inatakiwa kudril kisima na kupata maji ya uhakika tu, hapo jihesabie kuwa ni milionea.

Unafuga nguruwe na unalima Maboga humohumo ndo chakula chao Kikuu.

Ukiona soo unaliuzilia mbali kwa faida mara dufu
 
Mi natafuta Ekari 5 tu, pembezoni mwa Jiji la Dar.
Nikizipata najihesabia millionea.
Sigara Club Temeke Chang'ombe pana Ekari Nne tu.
Kuna viwanja viwili vya footbal, kimoja cha Basketball na ukumbi wa starehe.
Wajuzi mmenielewa.
Kila la kheri mkuu.
 
Fanya vitu vya maana,achana na vitu vya kijinga! ihamishie Breweries Nyumbani.
Kama hujajua ,nenda NMB au bank ya posta kaulize bei ya fixed deposit.Tupia huko wakati unapata akili nini cha kufanya.

Sikia hela huwa ni za ajabu huwa zinawazoea waliozizoea.kama hujawahi kuwa hata na m40 kwenye account yako,Hiyo m100,ikitua tuu kwenye account yako utapoteza fahamu,utakuja kuzinduka pale zitapobaki lile salio ulilolizoea.Atawatamkia watu uchawi wa chuma ulete kumbe issue ni wewe mwenyewe
 
Asante mkuu wazo zuri sana,natakiwa kutenga kiasi gani maana hela unapoipata ni lazima akili kwanza ikae sawa ndio upange matumizi
Hizo trip mbili za Dubai na mastates ukienda ukirudi,utabaki na chenji ya shilingi 120,000. itatosha kununua sub-woofer,uanze kupigisha disco toto hapo uwani kwako,hutakosa kuokoteza miambili miambili ambazo si haba.
 
Back
Top Bottom