Karibuni kwenye kongamano la uchangiaji wa damu salama na chanjo ya Uviko19 kwa vijana waishio mazingira hatarishi (vijana wa mtaani)

MwanaWA Ebrania

JF-Expert Member
Oct 6, 2017
207
250
HELLO
WAHESHIMIWA HABARI ZA LEO

MIMI KIJANA WENU NAITWA JAMES YUSTAR
NATOKA TAASISI YA YA VIJANA WA MTAANI YA JAMES FOUNDATION ILIYOPO DAR ES SALAAM TANZANIA

MIMI NI KATI YA VIJANA AMA BINADAMU WASIO NA HISTORY NZURI KTK MAISHA YAO.

James mimi Nilitupwa Jalalani baada ya kuzaliwa, nikiwa mtoto mchanga wa siku moja.
Kwa Wema wa MUNGU , Niliokotwa na Mama Mmoja msamaria Aitwaye Yusta, Ndio Maana naitwa James Yustar

Kwa bahati mbaya nilipofika umri wa miaka 7 Yule mamaangu aliyeniokota Alifariki Dunia. Baada ya kifo chake, maisha yangu yalibadilika, nilifukuzwa pale Nyumbani nilipokuwa naishi na kuanza kuishi mitaani.

Safari ya maisha ya Mtaani ilikuwa Ngumu saana. Namshukuru MUNGU mwaka 2013 Nilikutana na Boss Ruge Mutahaba (RIP) yeye alinifanya upya maisha yangu na kuirejesha ndoto yangu iliyokufa.

Boss Ruge alinitoa mtaani wakati huo nilikuwa naosha Magari kule posta, hukunikiwa nalala Nje, yeye alinipangia Nyumba kinondoni na kunipeleka shule.

Lkn zaidi ya yooote aliniandikia kitabu ambacho kilihusu Maisha yangu na vijana wengine waishio mitaani ili kupeleka ujumbe kwa Jamii.

Lkn pia alinisaidia kufungua Taasisi hii ya JAMES FOUNDATIONIli iweze kusaidia kupunguza na kutokomeza hongezeko la vijana na watoto waishio mtaani.... Hivyo kongamano hili la Uchangiaji wa Damu na utoaji wa Chanjo ya UVIKO19 linaumuhimu mkubwa saana kwa jamii hii ya vijana waishio Mazingira Hatarishi.

Hivyo nawakaribisha saana Kuungana pamoja nami ktk kuwasindikiza vijana waishio MAZINGIRA HATARISHI ktk swala la kijamii la UCHANGIAJI WA DAMU SALAMA NA CHANJO YA UVIKO19 KWA VIJANA NA WATOTO HAO.

ITAKAYO FANYIKA TAREHE21/11/2021 0CEAN ROAD HOSPITAL.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom