Karibuni kwenye harusi yangu

Nimeamua niwapatie taarifa mapema ili kama humu huwa kuna utaratibu wa kuchangiana mnichangie aisee maana nataka nifanye bonge la sherehe ambayo haijawahi tokea hapa jijini Mbeya.


Wewe si useme umeshindwa kulipa kodi ya chumba!!
 
Hongera sana kwa kuoa ukiwa matured nina imani na mkeo mtarajiwa nae mkubwa pia wengine hata age yako hatujafika.. ila tumeshafunga ndoa at 27 na watoto na mpaka divorce zimetujia katika age wewe upo singo
Divorce! Daah
 
Hivi watu humu jf na hizi id mnawezaje kutambuana Kama huyu ni me na ke.. kweli watu mnatabu yaani mnasurubika hatari yaani mapenzi yanawatesa hatari. Kiufupi Mimi tangia nimeingia humu siijui hata ku pm mtu wa jf naanzaje zaidi ya kusoma thread na kukomenti.


All in all all the best sir nikumbuke katika kadi zako
 
Naona unajaribu kumrubuni huyu binti ajue upo siriazi kweli, mwisho umkule kimasihara!
 
Kumbe humu kuna ndoa sasa mimi mbona naogopa kutoa no ukute nishapotezaga bahati humu.
 
Hamjambo humu ndani?

Baada ya miaka 37 ya kutapatapa katika dimbwi la usingoboi hatimaye ndugu yenu natarajia kujipatia jiko mwaka huu mwezi wa 8 au wa 9 hivi. Karibuni sana.

Shemeji yenu nimempata humu humu JF...sikutaka kujitaabisha mpaka huko FB au insta kwa wafilisiti.

Nimeamua niwapatie taarifa mapema ili kama humu huwa kuna utaratibu wa kuchangiana mnichangie aisee maana nataka nifanye bonge la sherehe ambayo haijawahi tokea hapa jijini Mbeya.

Siku shemeji yenu akinipa jibu la Yes I do ntampost na ntamuweka hadharani ili uwe ushuhuda kwa wanaJF wote.
Mniombee sana ili anikubalie bila kinyongo.

Asanteni na niwatakie usiku mnono nyote.
Kwanza hongera kwa hatua hiyo nzuri, naamini unasema kweli kabisa. Nitakuwa wa kwanza kukuchangia utakapothibitisha kuwa ni kweli. Nikiwa mkaazi wa Mbeya aliyeko mbali na Mbeya kwa sasa, nakuahidi ushirikiano wa dhati. Utatumia hata kausafiri kangu kako hapo Mbeya siku ya harusi yako. Uendelee kutujuza mkuu. Mwezi ujao nitakuwa Mbeya na uniweke kwenye kamati.
 
Hii Marafiki iko sehemu gani pale Ilomba, nina muda kidogo sijafika Mbeya.
Stand ya Ilomba kwenda Uyole, kwenye kona unavyofuata barabara ya kwenda Isyesye, kushoto kwako utawaona vijana "wanaunguza" nyama. Ni maeneo hayo
 
Back
Top Bottom